Mzee umeongea kweli ingetokea kama Tundu lissu akasema kesho kutwa atafanya maandamano na raia kudai katiba mpya huko manyara kuanzia leo asubuh wangekuwa wamesha deploy troops za kwenda kuzuia, simply kwasababu kwasababu awareness wanayotaka kutengeneza ni threat kwa utawala uliokuwepo, yan watawala wengi wa Africa wao huwa wanaangalia maslai yao tu na maaskari wengi wanaendeshwa kama mang’ombe sijui kwanini ? Askari wetu hawafanyagi reasoning hata kidogo, sijui ni mambo ya shule sijui ni nini. Tanzania kuna magari mengi yale ya kumwagia maji ya upupu kuzuia maandamano kuliko magari mengi ya maji yale ya fire ya kuzimia moto, chakushangaza sasa likitokea janga la moto huoni zile gari za maji ya upupu kuja kusaidia kumwaga maji, mambo mengi yanafikirisha hapa kwakweli…
 
Maelezo safi sana. Reasoning ya wanajf inazidi kushuka kila uchwao.
Wana Jf wanazidi kuonekana wajinga kwa sababu ya watu kama hao Sasa sijui mleta mada alitaka askari wa FFU asiye na mafunzo ya uokoaji afanye nini
 
Haya mambo ni vema tukawaomba akina Dr Mshana jr watutazamie Katika Ulimwengu wa roho pia.

Yaani Wataalam wote wa Tabia Nchi Hata wale wa mchongo wakiwa safarini Ndio Janga Kubwa kabisa linatokea huku nyumbani.

Mungu wafanyie Wepesi Watu wa Katesh.
Mnakuwaga wapuuzi kwenye mambo ya kisayansi mnaleta elimu zenu za kienyeji. Mshana Jr sio mtaalamu wa jiografia wala hali ya hewa, hawezi kukusaidia lolote katika hili. Uko Hanang hakuna waganga wa kienyeji? Mbona hamna kitu walisema.

Badala mpendekeze TMA kuongeza wataalamu, iongezewe bajeti, vifaa na utoaji taarifa nyinyi mnaleta uganga. Badala kuhoji ofisi ya Waziri Mkuu utayari wa uokoaji kwenye matukio kama haya mnaleta ramli. Ndio walewale mlikuwa mnadhihaki taarifa za TMA mkisema ni waongo.
 
Jumuiya mbalimbali za Kimataifa zasikitishwa na Mafuriko yaliyouwa zaidi ya Watu 50 Manyara nchini Tanzania na yamesema yatatuma Ujumbe wa Wataalamu

Source BBC news
hatari sana ile ni landslide balaa sana watupe misaada jamaniii sema ndo watu watapita na helaa za msaada humo humoo
 
Nilisema mwaka huu hamna elnino serikali iache kuwaandaa watu kwa kitu ambacho hakipo, wamewaambia watu kutakuwa na elnino wahame mabondeni matokeo yake huko walipokimbilia milima inaanguka.
Nakuona kwenye nyuzi kadhaa za haya mafuriko ukiilalamikia Serikali na bado sijakuelewa point yako ni ipi hasa! Elnino maana yake si ukame!Elnino ni Mvua kali zinazoangamiza mazao badala ya kuyakuza!Kosa la serikali kuwatoa watu mabondeni lilikuwa ni lipi ikiwa Serikali ilitabiri kutakuwa na mvua kali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…