Ndugu zangu Watanzania,
Rais wa umoja wa mabunge Duniani ambaye pia ndiye speaker wa bunge la Tanzania na mbunge wa Mbeya mjini ,kwa uchungu mkubwa, hisia kali , maumivu makubwa na masikitiko makubwa ametoa kwa unyenyekevu salamu za pole kwa wananchi wote wa Hanang hasa eneo la kateshi waliopata na msiba mkubwa wa kupoteza na kuondokewa na wapendwa wao ambapo mpaka sasa kunaripotiwa kuwa na vifo zaidi ya 63.
Rais huyo wa IPU ameendelea kuwaombea mejeruhi wote ili wapone haraka ,lakini pia amepongeza juhudi za serikali yetu, wananchi,wadau, mashirika,taasisi mbalimbali kwa namna zilivyojitoa na kujitolea katika zoezi zima la uokoaji pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu.
Ikumbukwe ya kuwa Rais huyu wa IPU amerejea nchini siku chache tu tangia atoke mashariki ya kati alikofika kwa ajili ya kujionea uharibifu mkubwa uliotokana na mgogoro na vita vinavyoendelea huko na kufanya nao mazungumzo.
lakini pia alitoa maagizo mazito kwa pande zote mbili juu ya kumaliza mgogoro huo ambao umesababisha vifo vya raia wasio na hatia hasa watoto ,akina mama na wazee. lakini pia alisema kuwa kamati ya wabunge wa IPU inayoshughulika na masuala ya mashariki ya kati itakwenda haraka akishaondoka huko.
Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.