Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 80 na Majeruhii 133
Hiyo ni landslide! Volcano ni mlipuko wa matope ya moto na landslide ni maporomoko ya mlima uliozidiwa na maji kutokana na mvua!
Labda mudslide au mud flood. Landslide si ndio ardhi inamomonyoka kanisa watu wanazama?
 
Menejimenti na Watumishi wa APRM Tanzania tunaungana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutoa salamu za pole kwa Wahanga wote wa maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Hanang katika kijiji cha Katesh.
IMG-20231205-WA0005.jpg
 
ujinga tu wa watanzania hadi leo tunashangaa kifo ikiwa ni Nature tayari ipo toka dunia kuumbwa na Mungu aliye hai. fungua ubongo huo acha ujinga
nasema wakifa ukoo wako wote itakuwa ndo wachache kijana.. hawa wengine hata akifa mmoja ni wengi
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wa umoja wa mabunge Duniani ambaye pia ndiye speaker wa bunge la Tanzania na mbunge wa Mbeya mjini ,kwa uchungu mkubwa, hisia kali , maumivu makubwa na masikitiko makubwa ametoa kwa unyenyekevu salamu za pole kwa wananchi wote wa Hanang hasa eneo la kateshi waliopata na msiba mkubwa wa kupoteza na kuondokewa na wapendwa wao ambapo mpaka sasa kunaripotiwa kuwa na vifo zaidi ya 63.

Rais huyo wa IPU ameendelea kuwaombea mejeruhi wote ili wapone haraka ,lakini pia amepongeza juhudi za serikali yetu, wananchi,wadau, mashirika,taasisi mbalimbali kwa namna zilivyojitoa na kujitolea katika zoezi zima la uokoaji pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu.

Ikumbukwe ya kuwa Rais huyu wa IPU amerejea nchini siku chache tu tangia atoke mashariki ya kati alikofika kwa ajili ya kujionea uharibifu mkubwa uliotokana na mgogoro na vita vinavyoendelea huko na kufanya nao mazungumzo.

lakini pia alitoa maagizo mazito kwa pande zote mbili juu ya kumaliza mgogoro huo ambao umesababisha vifo vya raia wasio na hatia hasa watoto ,akina mama na wazee. lakini pia alisema kuwa kamati ya wabunge wa IPU inayoshughulika na masuala ya mashariki ya kati itakwenda haraka akishaondoka huko.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Usiwafanyie dhihaka na siasa zako kwa ndugu zangu. Shika adabu yako.
 
Usimsogelee lakini 😂😂
Nimsogelee kufanya nini .mimi naendelea kumuombea Dr Tulia wakati wote kama alivyotuhitaji wananchi kuendelea kuwaombea viongozi wetu. Naona unawasilisha ujumbe wa mchungaji matsai .

Mimi muda wote lazima niwaombee Dr Tulia pamoja na Rais wetu mpendwa mama Samia pamoja na viongozi wetu wetu ili Mungu aendelee kuwalinda na kuwatetea katika majukumu yao ya kututumikia watanzania.
 
Tupewe siku 1 ya mapumziko kwa Taifa zima Ili tupate kutubu kwa Mungu wa mbinguni na kumuomba atufanyie wepesi Katika maisha yetu haya

Basi Yesu akasema " hii haitoki ila kwa kuomba na kufunga" Mathayo 17:21

Ahsanteni sana!
Tatizo sio kufunga tatizo unafunga nini??
 
Nimsogelee kufanya nini .mimi naendelea kumuombea Dr Tulia wakati wote kama alivyotuhitaji wananchi kuendelea kuwaombea viongozi wetu. Naona unawasilisha ujumbe wa mchungaji matsai .

Mimi muda wote lazima niwaombee Dr Tulia pamoja na Rais wetu mpendwa mama Samia pamoja na viongozi wetu wetu ili Mungu aendelee kuwalinda na kuwatetea katika majukumu yao ya kututumikia watanzania.
Amina bwashee 😄
 
Back
Top Bottom