Maoni yangu kuhusu Vita ya Urusi Kama Magharibi Au NATO watalazimika kuhusika moja Kwa moja

Maoni yangu kuhusu Vita ya Urusi Kama Magharibi Au NATO watalazimika kuhusika moja Kwa moja

Mkuu, kwa bahati mbaya au nzuri nilipofungua tu, nikaona hiyo mistari hapo niliyokwoti kabla sijaenda kule juu. Nikasema ngoja nimalizane na hili kwanza.
Hakuna asiyekemea uvamizi wa nchi yoyote juu ya nyingine, hasa ukiwa ni uvamizi wa kuonea tu, au kwa maslahi ya pembeni zaidi yasiyohatarisha nchi inayoivamia nyingine
Lakini inabidi pia uangalie kwa makini sana tatizo lililopo hapa kati ya Urusi na washirika wa nchi iliyovamiwa.
Ni hivi: ni kama ile vita baridi ilikuwa bado haijaisha. Hawa jamaa wa magharibi ni kama walijikuta kama vile kuna kitu hawakukimalizia kabisa ili roho zao zitulie. Urusi yenye nguvu, hata kama imejiunga katika mfumo huo huo wa kidunia unaohimizwa na hawa walioshinda vita ya baridi, bado haiwapi utulivu juu ya Urusi yenye nguvu katika eneo hilo la Ulaya.

Bado hawa wakubwa wa Ulaya, wakiongozwa na mkuu wao, wanakuwa na wasiwasi na hili li-nchi kubwa la Urusi lenye nguvu, na ambalo pamoja na lenyewe kukubali kuendesha shughuli zake kama zinavyoendeshwa huko Magharibi, bado hawana utulivu wa moyo juu yake (kuhusu usalama wao, baadae, sijui?); lakini wanaliogopa sana li-nchi hili.

Zaidi ya hayo, huyu mkubwa kabisa aliyebaki kama kinara wa dunia, hata yeye hataki hadhi yake hiyo itiliwe mashaka. Isihojiwe na yeyote awaye. Akikataa jambo, kila mtu aingie mstarini. Ni hulka ya kibinaadam hiyo. Ususi yenye nguvu kila mara itakuwa upande wa pili. Unaikumbuka ilivyokuwa Syria? Au hukufuatilia sinema hiyo.

Nisiende mbali sana na jambo hili, lakini wewe jiulize. Vita Baridi wamekwishashinda. Mpinzani wao mkuu amekwishasambaratika. Kuna haja gani tena ya kwenda kumbanabana kwa kujitanua mpaka mlangoni kwake? Anawaomba 'guarantee' ya usalama wake, mnamzungusha kiujanjaujanja na uongo mwingi.

Jamaa kaweka mstari mwekundu chini, usiuvuke, wao wanadhani anatania!
Halafu ona sasa wanavyozidi kumchochea huyu kibaraka waliyemtoa kama sadaka. Watu wake wanaumizwa, wao wanazidi kuchochea kuni hao watu waumizwe zaidi kwa kutoa silaha na kumpa matumaini kibaraka yasiyokuwepo, kiasi kwamba hata mazungumzo ya kusitisha vita anakuwa hana msimamo wake thabiti wa kuwahurumia raia zake.

Mrusi anapigania usalama wake. Wanambanabana hadi wamtoe roho? Walijaribu kuihadaa Chrchinia, wakakwama, sasa wanatafuta njia za kuendelea kulegeza mrusi kwa wasiwasi wao tu usiokuwa na msingi.

Ni hayo tu mkuu, ngoja nikasome huko juu.
kuna matango pori ulimezeshwa ndo unayatema , unaeza kuta ni mtu mzima ila akili yako haiko free kuchambua mambo , Kwann mnailazimisha hii ionekane ni vita kati ya Urusi vs West , hv hamuoni madudu anayoyafanya Urusi kwa mashriki ya ulaya ? hv ungekuwa ww ndo raia wa ulaya ya mashariki ungeendelea kuwa upande wa Urusi ? waafrika hatupend kuumiza vichwa vyetu , ushawai jiuliza kwann hayo mataifa ya mashariki ya Ulaya yanataka kujiunga na NATO ? je NATO imewai kuivamia nchi yyte ya Mashariki ya Ulaya ili kuiforce ijiunge na NATO ? ss jiulize kwnn wanakubali kumwaga damu ili kujiunga na NATO basi juwa kuwa Yapo mabaya mengi Urusi kawafanyia pia Usisahau kuwa nchi masikini za Ulaya zilikuwa upande huo mpk zilipojitenga zikapiga hatua kidogo licha ya Urusi amekuwa kikwazo kwenye maendeleo ya hizo nchi na ni kituko kuwa Urusi haiheshimu uhuru wa ndani wa hizo nchi na sio Ukraine tu bali hata majirani wengine , So hizo nchi zinaamini kuwa Kumwangusha mrusi ndo hatua yao muhimu ktk kuanza kuiandika historia yao mpya , ila Urusi anapaa excuse ya misaadaya WEST ambapo wapuuz wanabadili uhalisia na kuifanya ionekane kuwa ni WEST vs Urusi ingawaje still Russia bado ana kosa huez amka na kumvamia jiran yako
 
kwa sasa Putin kaamua kujimegea bandari za mauripol & odesa halafu kamuachia cimedian Kyiv yake
 
Hao vijana hawawezi kujua nguvu ya USSR.

1. Ulikuwa muunganiko wenye UZALENDO WA HALI JUU MNO.

2. Hapa ndo palikuwa na ujamaa haswa.

3. Jeshi na Inteligenc ya Russia hawa ndo waliisuka na kuifanya iwe bora kama hivi ilivyo leo.

Vijana wa sasa hawajui kuwa licha ya uzalendo uliotukuka wa USSR, CIA iliipasua hiyo USSR.

Toka ilipopasuliwa mambo yakabadilika mno, viongoz wa juu wa Russia, hasa akina Putin na Medved, wakatengeneza makundi ya kirafiki ambayo ndio yanaendesha Russia.

Haya makundi ni rafiki za Putin na familia zao, yana pesa chafu mno, pesa nyingi sana kupitia resources za Russia. Vijana wa sasa hawaelewi kuwa ule uzalendo ulokuwa USSR haupo tena ndani ya Russia. Ukichukua askar 1,000 wa Russia waliopo Ukraine, ukauliza wangapi hamtaki kupigania Taifa leo ktk hii vita? Naamini hawatapungua vijana 900 wataopinga hii vita.

Wengi mpaka sasa tunaamini kuwa NATO imekosea mno na imejikaanga yenyewe kuhusu uvamizi wa Russia. Vijana hawa wa hovyo hawajui kuwa hakuna shirika bora la Intelligenc ulimwengu kama CIA. Hawa wanajua 40 yearz mbele nini kifanyike kwa Taifa flan endapo lipo against nao. Hawa jamaa walishamsoma Russia muda sana, usifikiri kuwa hawakupiga hesabu cos za kumvamia Russia, walijua wakigomea gas nini kitatokea, kuna kitu wanakitafuta Russia, ni ngumu kukitambua ila upo wakati kitafahamika, wameona proa ni kubwa zaidi ndo maana wakaruhusu Ukraine aingie vitani pia.

Vita ni pesa, vita ni uchumi. Russia mbele ya mabeberu ni wa kawaida mno, nchi ndogo kieneo kama UK, Japan, France, German n.k zimemuacha parefu Mrusi. US usimuweke hapo kiuchumi dhidi ya Russia.
Uluanza vizuri ukamaizia na unazi hapo ndio ukaharibu kabisa
 
Dr..pamoja kwamba uelewa wangu mdogo kwenye maswala vita,lakini hapa unanipa shaka kidogo juu ya uwelewa wako kuhusu haya mataifa km Urusi na Marekani kwenye nguvu za kijeshi walizonazo,kwa sababu ikitokea wakubwa hawa wakaingia vitani sidhani km vita hii itachukua zaidi ya week moja bila kupata majibu ya nan kashinda na nani ameshindwa..kwani tusitegemee kuona Ak 47 wala wanajeshi wa jeshi Fulani kuingia sehem fulan,hapa tutegemee kuona ulimwengu unafunikwa na Giza zito na madhara yake itakuwa hadithi ambayo haikuwahi kutokea kabla..kwahiyo swala la nchi kuwa na uchumi mdogo au mkubwa halina nafasi hapo.
kwenye maisha yako yote hicho unachowazia hakitakuja kutokea , Putin ataangushwa na watu wa karibu yake , na analijua hilo na ndio maana kaanza kuboresha ulinz wake
 
Wewe ni mjinga
Kwa nn unampinga mwenzako eti hiyo vita "haitachukua muda mrefu kama unavyo dhani"
Unasema itachuka"saa kadhaa"
Mpumbavu kweli we nan amekupa hiyo guarantee ya kusema hivo??
We ni mtu wa ovyo huna uhakina na unachosema halafu unampinga mwenzako as if upo sahihi asilimia zote

Hayo ni maon ya mtoa mada tena kwa facts zake
Wewe nawe toa maon yako kwa facts zako
Halafu tulia
Hiyo vita ikitokea sisi ndiyo tutarudi kwenye huu uzi nakupima nani alikua na facts zenye ukweli

Next time hata ukianzisha uzi watu wana subscribe kabsaaa maana wanajua wewe ni mtu unaye tema madini vitu venye kueleweka

Mfano@Pascall kuna uzi alileta 2014 akisema mtu fulan atakuwa rais akatoa facts zake,ila alianza kusema ni tetesi tuu

Mtu Kama huyu akileta mada yake hapa siwez acha kumsoma maana najua ndani kuna madini mengi ya kufikirisha

Plz tuheshimu maon ya mtu sio kuanza kusema oooh ushoga mara hivi.......,!!!!!!
Achen utoto
wewe nawe huwezi kuwrka hoja zako bila kukashifu?
 
Mkuu trust me, ikitikokea leo Nato an US wakapigana na Urusi, vita haitachukua muda mrefu. Ndani ya muda mfupi vitaitaisha na hapatakuwa na mshindi.

Si hizo facts za bajeti/uchumi labda jwa hizi operation kama ya Urusi kwa Ukraine.
Ila US vs Russia makombora yatakuwa yanapishana angani tu
akili za muvi hizo , wenzio wapo real
 
sio kweli kuwa jf members wanadai may be Russia au USA kuna atakayeshinda mwenzie.....
USSR kama ambavyo kila mtu anakiri wazi kuwa lilikuwa taifa kubwa, na kusambaratika kwake zinaonekana kila dalili kuwa nguvu zile asilimia kubwa ziko restored asilimia kubwa na RUSSIA,,,
Albert Einstein "I don't know what the third world war will fought, but i know the fouth world war will fought with stones and stick " kwa kauli hii nadhani alimaanisha kama vita ya tatu itatokea basi huenda hakuna maisha baada ya hapo ambapo itabidi dunia iishie hapo na viumbe wapya waje kutokea huko mbelen alafu waanze maisha upya na technology mpya ambayo itaanza na viboko na mawe.......
nataka kusema aliyesema marekan ni ya kwanza kijeshi ni marekani na aliyesema Russia ya pili ni USA, China ya tatu ni USA, India, Israel etc....
kwa kuhitimisha vita ya tatu hakuna, na ikitokea hakuna maisha baada ya hapo,

USA and Russia wote wanadhan za maangamizi zaidi ya tujuavyo hapa jukwan, Ukraine sio kipimo sahihi ya silaha zitakazotumika kama ww3 itatokea
Great!!
 
Wewe lazima utakuwa moja katika hao vijana wanaosemwa hapa...

Eti unajiita babu na mjukuu...!

Mwingine huyu... masikini DENLSON ...!

Naam, ni kweli...Marekani si binadamu wa kawaida!

Kwa ufahamisho tu...Wapo Wamarekani wadengereko, warusi, wahindi, wasukuma, waswahili, wakikuyu, waitaliano, wachina, wapogoro, waibo, waarabu, wapagani, wakatoliki, wabudha, waislamu, wakristo, walatino, wanubi...

Kwa kifupi kila kinachopatikana duniani hapa utakipata Marekani. Kila rangi, jinsia, kabila, tabia, tamaduni, lugha, mila...utaipata Marekani.
Hiki ndio;kinakufanyauione marekani siyo ya kawaida?.
Mnaijua mareakani kwa sababu ni watu wa KUJIONYESHA na hamuijui Russia kwa sababuni watu wa KUFANYA MAMBO YAO KIMYA KIMYA ndio maana mnaona marekani sio wa kawaidasababu hamjui kiundani what is going on with Russia.
 
Hawa ndo Dr lwaitama aliowasema....wanamiliki tecno na Shule Hamna ila kwa ubishi sasa lol....hapo kishaweka bando lake la 500 anabisha kila kitu asalaleee fungu la kukosa
20220427_081529.jpg

we ni mjinga samahani lakini
 
hivi tunavyojadili ..kitambo makachero wa CIA na KGB wako field.
wamesha calulate risks kupigana direct...Mwenye kuamua hatma ya vita ya 3 ni US....Kadiri anavyopiga hatua za kuisogelea ndio anikairibia risk. Anachofanya US ni kuirefusha vita ya UKRAINE ni ili Russia andelee kudhoofika kiuchumi bila kujali uhai wa raia wa UKRAINE.
US asingeamua kukomaa vita hii ingeisha.
Kama vita 3 itatokea basi US ndiye wa kulaumiwa bila kuweka ushabiki.

Sijjajua kwa nn UKRAINE imekuwa muhimu kiasi hicho kwa US hadi kukubali uharibufu mkubwa hivyo uendelee,..!. Yaani Europe ikose gas..!, uchumi wa dunia uvurugike..! Germany avunje policy yake ya kivita ..! nk. Kuna agenda nyuma zaidi ya haki ya kujiunga na NATO..
Iweje Syria walifunga mizigo na kuamua kuondoka lakini UKRAINE inafanyika campaign ili Ulaya na dunia ziungane.
Kuna AJENDA ambayo US anataka kuifikia kidunia na pengine muda mwingi anaona kikwazo anayemzuia ni RUSSIA.
US alishaikamata ULAYA, AMERIKA, ASIA . si muarabu si muisrael si mjapan si nani ..amewakamata...
Mchina na India wao wako tu buisy na uchumi wake na wala sio kitisho kijeshi .

Siamini kwa intelligence ya US kuwa eti haya yanatokea tu..Huyu Zelensky huenda ni calculated ama kwa kujua au kutokujua....Acha tuendelee kutazama na kujadili '' FILM'
 
Nimepitia mijadala kadhaa ya vijana mbali mbali nimeona Tatizo ama lipo katika syllabus tunayotumia kuwafundishia masuala ya kidipomasia ya mataifa mbali mbali ,vijana wengi sana hawana ufahamu Kabisa , vita wanaijadili kama Mpira kwamba yeyote anaweza kupigwa, Vita inajadiliwa kama hadithi za abunuasi , vita imejadiliwa Kwa mzaha sana , watu wanakurupuka tu humu,kwanza nataka mjue Urusi iko vizuri sana kijeshi tena kwenye rank za kidunia yupo namba mbili nyuma ya Marekani , lakini leo hii akiingia vitani hata na China ambaye yuko namba tatu atapigwa kwasababu ya uchumi wake mdogo, vita ni bajet yako kijeshi unavyo wekeza kwenye technology ya silaha na udadisi (intelligence). Na Muda katika kupigana vita ya mataifa makubwa hauwi week moja Au mbili ni miezi zaidi ya minne mpaka saba! Hapa lazima uwe vizuri kiuchumi ili uweze kuendesha mambo yote mawili Kwa wakati mmoja , Yaan vita iendelee huku shughuli zako za kiuchumi zisikwame!

Vijana tumekosa kujisomea maandiko mbali mbali na kudadis kupitia makala na scientific research mbali mbali .

Kuna comments moja niliiona sehemu kijana anasema eti alisema ''China itategea kipindi ambacho US ametingwa na uvamizi fulani wa nchi kubwa nyingine, alafu yeye ndo atatumia muda huo kuivamia Taiwan na ataichukua kwasababu kwasasa China yupo mbali sana kijeshi''
Nilimuelewesha mambo mengi sana akaonekana kukubaliana namimi,

Hata hapa JamiiForums sikuwa Mwanachama Nina miezi Kama minne ninejiunga ila napitia masuala kadhaa ya wachambuzi wa siasa zetu Kama kijana Au Mdogo wangu Pascal Mayalla ana makala nyingi sana hapa JamiiForums Kama wangekuwa wanawalipa wana makala basi angepata namba kuna wengine Kama Kiranga Kalamu1 Mag3 sijaona wakichambua masuala haya ya kimataifa na ningetegemea kuona mtizamo wao katika haya

Basi nawaambia kwamba

Watu wanaibeza sana US katika nyanja za vita, US hawana gwaride kuonyesha vifaa vyao ila vita vikianza utaona mengi ambayo macho hayajawahi kuona... Au Kama inafanyika inafanyika katika namna ambayo ni Siri sana !

Pia hatupaswi kuipuuza Urusi katika nyanja za kijeshi, lakini ni upuuzi kudhani Urusi inaweza mess up na Washington na Moscow ikabaki kama ilivyo... tunakosea sana! Hakuna Muungano ulikuwa unatisha kama USSR wadogo ninyi wengi humu !
Hakuna Taifa lilikuwa linatisha Kama Iraq ya Sadam Hussein! Au UMOJA wa waarabu chini ya Sadath wa Misiri. Lakin walikwama sehemu moja tu intelligence na uchumi…

Us kwa uchumi wake na teknolojia lazima Urusi itakuwa katika hali ngumu Kwa Urusi kusema iingie vitani nayo ibaki salama!!

Hata Asia ina safari ndefu kujifunza kutoka America na Ulaya kuanzia military technology,

Nitaendelea kwanini tunapaswa Kukataa vita! Maana nilivyoandika hapa kuna watakaosema natetea maovu Au vamizi za US kwingine Hapana nakemea sana kama nilivyokemea Afghanistan, LIBYA na sasa Nakemea Uvamizi wa Urusi Kwa Ukraine!!

Mimi Dr. Lwaitama
Naunga mkono hoja 100%, na nitakuwa nafuatilia mawazo yako hapa., watu hufikiria kwa vile US hana maonyesho ya silaha hivyo ni weakened
 
Waweza ishusha Urusi ktk nyanja zoote ujuazo eg uchumi sijui nini lakini usije thubutu kufanya hivyo kwenye vita na hili wakubwa kuliko wewe wanalijua ndo maana hata wao walianza na vikwazo na wakasema Urusi haiwezi kudumu vitani ndani ya mwezi cha ajabu muda unavyozidi kwenda ndivyo mashambulizi mazito yanazidi fanywa na Urusi na sasa hesabu zimegoma hata propaganda ya kwamba Urusi watu wanalala njaa haziwezekani tena kila nchi muda si mrefu itaanza kutetea maisha ya watu wake badala ya porojo za US.

Kuna watu wanaikosoa Russian kwakuwa ni undemocratic kitu ambacho ni kweli lakini wakumbuke kuwa nchi zote duniani zilizoingia mapigano na NATO pona yao ni kusaidiwa na urusi kama si hivyo hiyo nchi lazima eteketee hivyo ni nchi nyingi sana zilikuwa ni makoloni zilipata uhuru kwa msaada wa AK47 hata Julius Malema aliwahi sema hili.

Kikubwa ktk vita ni mipango na siyo kukariri uchumi kwani ilikuwaje Israel akazishinda nchi zaidi ya 5 kwenye vita?
NATOA ONYO BILA KUJALI UNA UCHUMI MKUBWA KIASI GANI USIJE VAMIA URUSI UKIAMINI UCHUMI UTAKUOKOA UTAKUFA KATIKATI YA MANOTI YAKO NA YASIKUSAIDIE CHOCHOTE.
 
Naona kama Uzi haujashiba!Kwa Tambo ulizoanza nazo basi nikajua Uzi utakuwa na content ila nimekuwa disappointed!
 
kuna matango pori ulimezeshwa ndo unayatema , unaeza kuta ni mtu mzima ila akili yako haiko free kuchambua mambo , Kwann mnailazimisha hii ionekane ni vita kati ya Urusi vs West , hv hamuoni madudu anayoyafanya Urusi kwa mashriki ya ulaya ? hv ungekuwa ww ndo raia wa ulaya ya mashariki ungeendelea kuwa upande wa Urusi ? waafrika hatupend kuumiza vichwa vyetu , ushawai jiuliza kwann hayo mataifa ya mashariki ya Ulaya yanataka kujiunga na NATO ? je NATO imewai kuivamia nchi yyte ya Mashariki ya Ulaya ili kuiforce ijiunge na NATO ? ss jiulize kwnn wanakubali kumwaga damu ili kujiunga na NATO basi juwa kuwa Yapo mabaya mengi Urusi kawafanyia pia Usisahau kuwa nchi masikini za Ulaya zilikuwa upande huo mpk zilipojitenga zikapiga hatua kidogo licha ya Urusi amekuwa kikwazo kwenye maendeleo ya hizo nchi na ni kituko kuwa Urusi haiheshimu uhuru wa ndani wa hizo nchi na sio Ukraine tu bali hata majirani wengine , So hizo nchi zinaamini kuwa Kumwangusha mrusi ndo hatua yao muhimu ktk kuanza kuiandika historia yao mpya , ila Urusi anapaa excuse ya misaadaya WEST ambapo wapuuz wanabadili uhalisia na kuifanya ionekane kuwa ni WEST vs Urusi ingawaje still Russia bado ana kosa huez amka na kumvamia jiran yako
Ninakusikitikia sana mkuu 4by94, kwa kukosa ufahamu wa mambo ya dunia kama haya.

Sitapoteza wakati wangu zaidi hapa kufafanua chochote nilichokwishakiandika humu kwa maana naona huna uwezo wa kuelewa kilichoandikwa.
Unauliza kama NATO alishavamia nchi yoyote (ya ulaya), kwani ni ulaya pekee ndiko kuna nchi? Hii inaonyesha wazi huna ufahamu wa kutosha juu ya mambo haya.
 
Nimepitia mijadala kadhaa ya vijana mbali mbali nimeona Tatizo ama lipo katika syllabus tunayotumia kuwafundishia masuala ya kidipomasia ya mataifa mbali mbali ,vijana wengi sana hawana ufahamu Kabisa , vita wanaijadili kama Mpira kwamba yeyote anaweza kupigwa, Vita inajadiliwa kama hadithi za abunuasi , vita imejadiliwa Kwa mzaha sana , watu wanakurupuka tu humu,kwanza nataka mjue Urusi iko vizuri sana kijeshi tena kwenye rank za kidunia yupo namba mbili nyuma ya Marekani , lakini leo hii akiingia vitani hata na China ambaye yuko namba tatu atapigwa kwasababu ya uchumi wake mdogo, vita ni bajet yako kijeshi unavyo wekeza kwenye technology ya silaha na udadisi (intelligence). Na Muda katika kupigana vita ya mataifa makubwa hauwi week moja Au mbili ni miezi zaidi ya minne mpaka saba! Hapa lazima uwe vizuri kiuchumi ili uweze kuendesha mambo yote mawili Kwa wakati mmoja , Yaan vita iendelee huku shughuli zako za kiuchumi zisikwame!

Vijana tumekosa kujisomea maandiko mbali mbali na kudadis kupitia makala na scientific research mbali mbali .

Kuna comments moja niliiona sehemu kijana anasema eti alisema ''China itategea kipindi ambacho US ametingwa na uvamizi fulani wa nchi kubwa nyingine, alafu yeye ndo atatumia muda huo kuivamia Taiwan na ataichukua kwasababu kwasasa China yupo mbali sana kijeshi''
Nilimuelewesha mambo mengi sana akaonekana kukubaliana namimi,

Hata hapa JamiiForums sikuwa Mwanachama Nina miezi Kama minne ninejiunga ila napitia masuala kadhaa ya wachambuzi wa siasa zetu Kama kijana Au Mdogo wangu Pascal Mayalla ana makala nyingi sana hapa JamiiForums Kama wangekuwa wanawalipa wana makala basi angepata namba kuna wengine Kama Kiranga Kalamu1 Mag3 sijaona wakichambua masuala haya ya kimataifa na ningetegemea kuona mtizamo wao katika haya

Basi nawaambia kwamba

Watu wanaibeza sana US katika nyanja za vita, US hawana gwaride kuonyesha vifaa vyao ila vita vikianza utaona mengi ambayo macho hayajawahi kuona... Au Kama inafanyika inafanyika katika namna ambayo ni Siri sana !

Pia hatupaswi kuipuuza Urusi katika nyanja za kijeshi, lakini ni upuuzi kudhani Urusi inaweza mess up na Washington na Moscow ikabaki kama ilivyo... tunakosea sana! Hakuna Muungano ulikuwa unatisha kama USSR wadogo ninyi wengi humu !
Hakuna Taifa lilikuwa linatisha Kama Iraq ya Sadam Hussein! Au UMOJA wa waarabu chini ya Sadath wa Misiri. Lakin walikwama sehemu moja tu intelligence na uchumi…

Us kwa uchumi wake na teknolojia lazima Urusi itakuwa katika hali ngumu Kwa Urusi kusema iingie vitani nayo ibaki salama!!

Hata Asia ina safari ndefu kujifunza kutoka America na Ulaya kuanzia military technology,

Nitaendelea kwanini tunapaswa Kukataa vita! Maana nilivyoandika hapa kuna watakaosema natetea maovu Au vamizi za US kwingine Hapana nakemea sana kama nilivyokemea Afghanistan, LIBYA na sasa Nakemea Uvamizi wa Urusi Kwa Ukraine!!

Mimi Dr. Lwaitama
Dr.

Shukurani sana kwa mada na asante kwa kunitaja.

Mimi jana nilikuwa nafuatilia mjadala mmoja wa vita hivi (inawezekana tulikuwa tunafuatilia pamoja mjadala huu huu), nikamwambia rafiki yangu mmoja maneno kama hayo uliyoyaandika, kabla hata sijasoma maandiko yako haya. Mpaka mfano nilitumia huo huo wa ushabiki wa Simba na Yanga.

Niliandika kwamba kuna Watanzania wanajadili vita ya Urusi na Ukraine ambayo inaweza kwenda kwenye vita vya dunia ya nyuklia, lakini kwa ushabiki ambao utafikiri wanajadili Simba na Yanga.

Na mara nyingine, watu wanaotaka mijadala ya tija, ya data, ya kuelimishana, wanaweza kuepuka mijadala ya hivi.

I think there is a Mark Twain quote "Never argue with stupid people. They will drag you down to their level and beat you with experience".

I am not interested in that.
 
Nitaendelea kwanini tunapaswa Kukataa vita! Maana nilivyoandika hapa kuna watakaosema natetea maovu Au vamizi za US kwingine Hapana nakemea sana kama nilivyokemea Afghanistan, LIBYA na sasa Nakemea..
Upo sahihi kabisa Dr.
 
Back
Top Bottom