Maoni yangu kuhusu Vita ya Urusi Kama Magharibi Au NATO watalazimika kuhusika moja Kwa moja

kuna matango pori ulimezeshwa ndo unayatema , unaeza kuta ni mtu mzima ila akili yako haiko free kuchambua mambo , Kwann mnailazimisha hii ionekane ni vita kati ya Urusi vs West , hv hamuoni madudu anayoyafanya Urusi kwa mashriki ya ulaya ? hv ungekuwa ww ndo raia wa ulaya ya mashariki ungeendelea kuwa upande wa Urusi ? waafrika hatupend kuumiza vichwa vyetu , ushawai jiuliza kwann hayo mataifa ya mashariki ya Ulaya yanataka kujiunga na NATO ? je NATO imewai kuivamia nchi yyte ya Mashariki ya Ulaya ili kuiforce ijiunge na NATO ? ss jiulize kwnn wanakubali kumwaga damu ili kujiunga na NATO basi juwa kuwa Yapo mabaya mengi Urusi kawafanyia pia Usisahau kuwa nchi masikini za Ulaya zilikuwa upande huo mpk zilipojitenga zikapiga hatua kidogo licha ya Urusi amekuwa kikwazo kwenye maendeleo ya hizo nchi na ni kituko kuwa Urusi haiheshimu uhuru wa ndani wa hizo nchi na sio Ukraine tu bali hata majirani wengine , So hizo nchi zinaamini kuwa Kumwangusha mrusi ndo hatua yao muhimu ktk kuanza kuiandika historia yao mpya , ila Urusi anapaa excuse ya misaadaya WEST ambapo wapuuz wanabadili uhalisia na kuifanya ionekane kuwa ni WEST vs Urusi ingawaje still Russia bado ana kosa huez amka na kumvamia jiran yako
 
kwa sasa Putin kaamua kujimegea bandari za mauripol & odesa halafu kamuachia cimedian Kyiv yake
 
Uluanza vizuri ukamaizia na unazi hapo ndio ukaharibu kabisa
 
kwenye maisha yako yote hicho unachowazia hakitakuja kutokea , Putin ataangushwa na watu wa karibu yake , na analijua hilo na ndio maana kaanza kuboresha ulinz wake
 
wewe nawe huwezi kuwrka hoja zako bila kukashifu?
 
akili za muvi hizo , wenzio wapo real
 
Great!!
 
Hiki ndio;kinakufanyauione marekani siyo ya kawaida?.
Mnaijua mareakani kwa sababu ni watu wa KUJIONYESHA na hamuijui Russia kwa sababuni watu wa KUFANYA MAMBO YAO KIMYA KIMYA ndio maana mnaona marekani sio wa kawaidasababu hamjui kiundani what is going on with Russia.
 
hivi tunavyojadili ..kitambo makachero wa CIA na KGB wako field.
wamesha calulate risks kupigana direct...Mwenye kuamua hatma ya vita ya 3 ni US....Kadiri anavyopiga hatua za kuisogelea ndio anikairibia risk. Anachofanya US ni kuirefusha vita ya UKRAINE ni ili Russia andelee kudhoofika kiuchumi bila kujali uhai wa raia wa UKRAINE.
US asingeamua kukomaa vita hii ingeisha.
Kama vita 3 itatokea basi US ndiye wa kulaumiwa bila kuweka ushabiki.

Sijjajua kwa nn UKRAINE imekuwa muhimu kiasi hicho kwa US hadi kukubali uharibufu mkubwa hivyo uendelee,..!. Yaani Europe ikose gas..!, uchumi wa dunia uvurugike..! Germany avunje policy yake ya kivita ..! nk. Kuna agenda nyuma zaidi ya haki ya kujiunga na NATO..
Iweje Syria walifunga mizigo na kuamua kuondoka lakini UKRAINE inafanyika campaign ili Ulaya na dunia ziungane.
Kuna AJENDA ambayo US anataka kuifikia kidunia na pengine muda mwingi anaona kikwazo anayemzuia ni RUSSIA.
US alishaikamata ULAYA, AMERIKA, ASIA . si muarabu si muisrael si mjapan si nani ..amewakamata...
Mchina na India wao wako tu buisy na uchumi wake na wala sio kitisho kijeshi .

Siamini kwa intelligence ya US kuwa eti haya yanatokea tu..Huyu Zelensky huenda ni calculated ama kwa kujua au kutokujua....Acha tuendelee kutazama na kujadili '' FILM'
 
Naunga mkono hoja 100%, na nitakuwa nafuatilia mawazo yako hapa., watu hufikiria kwa vile US hana maonyesho ya silaha hivyo ni weakened
 
Waweza ishusha Urusi ktk nyanja zoote ujuazo eg uchumi sijui nini lakini usije thubutu kufanya hivyo kwenye vita na hili wakubwa kuliko wewe wanalijua ndo maana hata wao walianza na vikwazo na wakasema Urusi haiwezi kudumu vitani ndani ya mwezi cha ajabu muda unavyozidi kwenda ndivyo mashambulizi mazito yanazidi fanywa na Urusi na sasa hesabu zimegoma hata propaganda ya kwamba Urusi watu wanalala njaa haziwezekani tena kila nchi muda si mrefu itaanza kutetea maisha ya watu wake badala ya porojo za US.

Kuna watu wanaikosoa Russian kwakuwa ni undemocratic kitu ambacho ni kweli lakini wakumbuke kuwa nchi zote duniani zilizoingia mapigano na NATO pona yao ni kusaidiwa na urusi kama si hivyo hiyo nchi lazima eteketee hivyo ni nchi nyingi sana zilikuwa ni makoloni zilipata uhuru kwa msaada wa AK47 hata Julius Malema aliwahi sema hili.

Kikubwa ktk vita ni mipango na siyo kukariri uchumi kwani ilikuwaje Israel akazishinda nchi zaidi ya 5 kwenye vita?
NATOA ONYO BILA KUJALI UNA UCHUMI MKUBWA KIASI GANI USIJE VAMIA URUSI UKIAMINI UCHUMI UTAKUOKOA UTAKUFA KATIKATI YA MANOTI YAKO NA YASIKUSAIDIE CHOCHOTE.
 
Naona kama Uzi haujashiba!Kwa Tambo ulizoanza nazo basi nikajua Uzi utakuwa na content ila nimekuwa disappointed!
 
Ninakusikitikia sana mkuu 4by94, kwa kukosa ufahamu wa mambo ya dunia kama haya.

Sitapoteza wakati wangu zaidi hapa kufafanua chochote nilichokwishakiandika humu kwa maana naona huna uwezo wa kuelewa kilichoandikwa.
Unauliza kama NATO alishavamia nchi yoyote (ya ulaya), kwani ni ulaya pekee ndiko kuna nchi? Hii inaonyesha wazi huna ufahamu wa kutosha juu ya mambo haya.
 
Dr.

Shukurani sana kwa mada na asante kwa kunitaja.

Mimi jana nilikuwa nafuatilia mjadala mmoja wa vita hivi (inawezekana tulikuwa tunafuatilia pamoja mjadala huu huu), nikamwambia rafiki yangu mmoja maneno kama hayo uliyoyaandika, kabla hata sijasoma maandiko yako haya. Mpaka mfano nilitumia huo huo wa ushabiki wa Simba na Yanga.

Niliandika kwamba kuna Watanzania wanajadili vita ya Urusi na Ukraine ambayo inaweza kwenda kwenye vita vya dunia ya nyuklia, lakini kwa ushabiki ambao utafikiri wanajadili Simba na Yanga.

Na mara nyingine, watu wanaotaka mijadala ya tija, ya data, ya kuelimishana, wanaweza kuepuka mijadala ya hivi.

I think there is a Mark Twain quote "Never argue with stupid people. They will drag you down to their level and beat you with experience".

I am not interested in that.
 
Nitaendelea kwanini tunapaswa Kukataa vita! Maana nilivyoandika hapa kuna watakaosema natetea maovu Au vamizi za US kwingine Hapana nakemea sana kama nilivyokemea Afghanistan, LIBYA na sasa Nakemea..
Upo sahihi kabisa Dr.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…