Maoni yangu kuhusu Vita ya Urusi Kama Magharibi Au NATO watalazimika kuhusika moja Kwa moja

Ikitokea kupigana NATOAMERICA vs Russia si ajabu tukatumia saa moja tu vita vikaisha.

Sababu:
1. Mmoja akiwahiwa kuhackiwa satelaiti zake michezo unaisha.
2. Mmoja akiwahiwa kupigwa sehemu nyeti, hataweza kujibu..

Intelligences za nchi zote ziko lakini.

Naomba isitokee
 
Hivi Bakressa akikuattack atakushinda kwa sababu uchumi wako ni mdogo?


Nauliza tu usichukie.
 
Naona kama Uzi haujashiba!Kwa Tambo ulizoanza nazo basi nikajua Uzi utakuwa na content ila nimekuwa disappointed!
Unasema uzi haujashiba wakati unaona kabisa bado kuna mwendelezo unakuja,kweli bado tuna safari ndefu sana kama Taifa
 
Lakini, pamoja na vikwazo hivi, wewe unadhani wao pia hawatatetereka. Unadhani dunia haitaanza kujiuliza kwa nini mfumo wa biashara uhodhiwe na nchi moja au kundi la nchi? Unadhani huu hautakuwa mwanzo wa kuuliza maswali juu ya mfumo huu?
Hapa umeonesha unazi wako na mahaba kwa Urusi bila kuukubali ukweli uliopo.

Kwani unadhani Dunia haijawahi kujiuliza kuhusu mfumo wa uchumi uliopo mpaka baada ya hivi Vita?...

Marekani Kama kubwa la Ubeberu, ndiyr kinara wa uchumi kwa Sasa, ana ushawishi mkubwa kwenye taasisi/mifuko yote ya kifedha achilia mbali wa kidiplomasia, na Dunia inatambua hilo hivyo hakuna wa kujiuliza kuhusu hilo.
 
Heshima mkuu 'Proved'.

Hapana, usinielewe hivyo. Binafsi sina kabisa unazi wowote na Urusi; kwani Urusi yenyewe ilishatumbukia kwenye mfumo huo huo wa uchumi wa dunia, kwa hiyo hakuna tofauti yoyote kwenye mfumo kati ya huo unaotawaliwa na Marekani, akiwa kinara na washirika wake wengine, ambao sasa silaha yao kuu katika vita, hasa na hivi viinchi vidogo vidogo kama Korea Kaskazini, Zimbabwe, Venezuela ni kuwapiga kwa kuwawekea vikwazo vya uchumi. Hii sasa ndiyo silaha ya hawa wakubwa, kuwanyoosha hawa wengine.

Nadhani hujaelewa vizuri hoja ninayojaribu kuiwasilisha hapa kuhusu hii silaha ya vikwazo vya kiuchumi ambayo sasa ndiyo inayotumika sana.
Maana yangu ni kwamba, nchi za dunia lazima zitaanza kujiuliza juu ya swali hili. Kwa nini ziwe tegemezi katika haya maswala kwa nchi moja na washirika wake wachache katika kuendesha mfumo mzima wa uchumi wa dunia?

Ni sawa kabisa kulinganisha hili swala na watu kuanza kujiuliza na kukataa kutawaliwa (ukoloni). Baada ya maswala hayo kuwepo, ukoloni ukapigwa vita, waliokuwa na makoloni bila kupenda wakayaachia.

Sasa wewe unadhani watu wataacha kujiuliza kwa nini sarafu ya nchi moja ndiyo iwe msingi wa uhai wa uchumi wao?

Unadhani watu wataacha kujiuliza kwa nini mabenki ya nchi za upande mmoja ndiyo yawe na uamzi wa wapi pesa zielekezwe?

Huu ni mwanzo tu, mambo hayawezi kubadilika kwa siku au wiki moja. Hayo unayoyasema kuwa kinara wa uchumi duniani, hilo ni swala la mpito tu, leo ni huyo, kesho atakuwepo mwingine.

Nisome vizuri unielewe mkuu wangu 'Proved'.
 
IRAQ labda ilikua inaogopewa na IRAN na SYRIA labda
Kwamba US akiingia vitani na RUSSIA yale majengo marefu pale DC nakwengineko yatabakia kama yalivyo!!?
US ndio anatapatapa hv kuelekea mwisho wake
Wewe nakubaliana na mleta Mada Iran ilikuwa tishio
 
Kwanza Shikamoo Join the chain ya CHADEMA inaendeleaje!

Naona CHADEMA mmeshika msimamo kwamba mnasimama na Urusi nauliza Mbona mkitoa mifano ya democracy mnatolea ya USA, na mnaposhambuliwa mnaenda USA si Urusi?
huo msimamo wa Cdm na Urusi ni wa Yeriko peke yake
halafu hii inaingiaje?
 
Kwanza Shikamoo Join the chain ya CHADEMA inaendeleaje!

Naona CHADEMA mmeshika msimamo kwamba mnasimama na Urusi nauliza Mbona mkitoa mifano ya democracy mnatolea ya USA, na mnaposhambuliwa mnaenda USA si Urusi?
Mkuu, sidhani kama huo msimamo ni wa chama.. Itakuwa ni maoni binafsi ya watu wachache.
Kuunga mkono udikteta kwa sababu yoyote ile lzm uwe kiazi!
 
Mkuu ulichokisema ndo uhalisia wa vita vya kisasa tatizo huyu lwaitama1 amechambua haya mambo ya vita vya karne hii kwa kuangalia technology na facts za kizamani za kutumia mapanga, visu, gobole, farasi, bunduki na mabomu ya kutifua ardhi , ambapo hiyo technology ndo ilikuwa inaweza kutumia muda mrefu mkipagana kwenye battle field face to face.

Au kama siyo hivo basi amechambua kwa kuangalia uwezo wa majeshi yetu ya Africa yanayojivunia kumiliki AkA47 na mizinga, hapo ndo vita inaweza ikaenda miezi hiyo aliyoitaja au hata miaka.

Ila sasa tukirudi kwenye full scale war inayohusisha miongoni mwa nchi hizi nazo enda kuzitaja.
Russia
USA
CHINA
UK
GERMANY
N.KOREA
IRANI
ISRAEL
FRENCH
INDIA na n.k
basi usitegemee kama kuna vita ya miezi hapo.
Mfano ikitokea battle ya USA Vs Russia, halafu wote wakatumia full scale war, kama vita wakianza leo jumatatu basi kufikia Jumatano vita itakuwa imeisha kabisa na hizo nchi zinakuwa zimebaki either magofu au historia katika ulimwengu huu.

Haya mapigano waliyo/wanayopigana Urusi, NATO na Marekani kwenye nchi mbalimbali duniani kama iraq, libya, syria,chenchen, Afghanistan na sasa Ukraine siyo full scale war bali ni special military operation tu.

Na ndo maana ukiondoa ujinga wetu wa ki afrika kama wa huyo mleta mada, mataifa mengi ya ulaya kwa kutambua uhalisia wa Vita vya kisasa yanaogopa na hayataki kabisa kuingia vitani na nchi inayomiliki nukes na hata hao wenye nukes nao wanaombea isitokee migogoro itakayo walazimu wao kutumia hizo nuclear weapons.

Mwisho; naomba nimalize kwa kuuliza maswali mawili kwa mleta mada lwaitama1

Swali namba moja: Just imagine, kama bomu la nukes la 1945 lililopigwa japan liliweza kuteketeza mikoa mikubwa miwili (Hiroshima na Nagasaki) na kuua watu zaidi ya elfu20 kwa mpigo na bado likaacha athari zinazo athiri hadi leo hii vipi leo currently advanced nuclear bombs zikianza kutua kwenye uso wa ardhi unadhani kipi kitatokea na itachukua muda gani kuona hayo matokeo?

Swali namba mbili; unadhani nikwanini mpaka leo japan, south korea na USA hawathubutu hata kuikoromea north korea kijeshi zaidi ya kulia lia tu licha ya north korea kutest mambovu hatari yanayo angukia hadi sehemu ya bahari ya japan ambaye ni mwanachama wa G7 na rafiki wa USA?

Unadhani kwanini Rais(D. TRUMP) wa taifa kubwa kama USA alikubali kutoka white house mpaka kwenda Singapore kwaajili tu yakufanya mazungumzo na bwana mdogo kabisa wa taifa linalosemakana ni masikini Mr Kim jung Un(kiduku)?

Nawasilisha.
 
Mimi kwakweli sikubaliani na hiyo hoja..kama Marekani wangekuwa vizuri kama unavyosema, waliwahi kuingia vitani na Vietnam, nini kilitokea? Walichemsha vibaya sana. Na tena walikuwa wanasaidiwa na ufaransa na nchi zingine za ulaya. Juzi tu alikuwa huko Afghanistan, amefanya nini? Baada ya miaka kama 20 hakuna lolote la maana Ali achieve. Kama alishindwa huko ndo ataiweza urusi? Marekani ameishia kuwanyanyasa waarabu tu. Urusi sio level yake. Kwa kuthibitisha Hilo, hakuna mahali marekani yupo anapigana, urusi akaingia akaendelea kubaki. Wiki 2 tu zilimtosha kumfurusha mmarekani hapo Syria.
 
Urusi kusaidia wengine haihalalish kuvamia sovereign nation , hata mm nlikuwa shabiki mkubwa wa Putin ila nimemuona kenge kwa huu uvamiz
 
Hapo kwanza nicheke , kwan tunazungumzia mataifa ya ukanda gan ? mara hii ushaanza uliza kama hamna mataifa sehemu nyingine ? Naamini umeelewa hoja yangu ila ndo utimu unakutoa ufahamu , mataifa ya mashariki ya Ulya sio wajinga kumwaga damu kujiunga na WEST , Urusi anafanya maovu mengi kwenye uchumi na siasa za majirani zake , ova
 
mjomba tuliza akili hoja zinakuelemea tyr , huelewek unaandika nn , ebu kumbuka mada ni ulaya ya mashariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…