Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wahenga walisema "Ulimi umeponza kichwa"Ila watu bhana maneno yako mwenyew yanakufunga mwenyew
Kamasi zimeingiaje hapo..content kwa kuharibu reputation ya chuo kwa cheating?
hiyo DR mangungo au.?kichwani umejaza kamasi.
Mkuu chuo kina wanafunzi 10k, kila mwaka wanafanya UE mara 2.. wana storage gani ya kutunza hizo karatasi za miaka yote hii. Hapo kuna mafile ya wanafunzi na ya staff ya chuo..Ulidhani wanachoma?
Aah basi hii nilikua sifahamu.Examination office nyingi huwa zimakaa na booklets kwa miaka mitano nadhani sheria ndio inasema hivo
Ardhi ni miaka minne mpaka mitano mkuu, kutegemea na kozi husika.Mwana kulitaka, mwana kulipata. Kiranga komo. Dakika mbili za umaarufu zinaenda kugharimu miaka 3 ya elimu zao. Pumbavu.
Unajua maana ya ‘Confession’?Chuo kitawezaje kuthibitisha hili?
Hapo kwenye sahihi, handwriting kwenye booklets zinaweza kusaidia kutoa hukumu ya haki.Wanahukumiwa na chuo sio mahakama.
Kuna hizo booklet pia kuna sahihi
Wataanzia na Miandiko handwriting siyo lazima ifanane hadi kwa mapacha,Hapo ndio ngoma. watathibitishaje huo uchunguzi wao?
Udaktari wangu wewe haukuhusu..
Kwa sababu vile vile hata ulofa wako wewe mimi haunihusu..
Unachotakiwa ni Kujibu hoja Iliyo mezani..
Siendi,huo muda sina .Mimi nimesikiliza kipande kilichowekwa hapa.Nenda YouTube.
Any way miandiko yao inafanana basi.Mitihani yako yote toka mwaka wa kwanza mpaka mwaka wa nne ipo......
Ni mtihani mmoja tu ndio ulibadilisha mwandiko ukafanana na dada ako?
Afu baada ya hapo ukarudia mwandiko wako wa zamani?
Ni masista duu wakisasa hawajavaaKama kwenye hiyo video wamevaa hijabu basi samia lazima hatafanya hivyo ....mimi hiyo video sijatazama
Uchunguzi utafanyika na itathibitika sio kweli na wahusika wataomba radhi kulinda image ya chuoHivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!
Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.
Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.
Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo
Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024
View attachment 2927199
Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
Forensic experts wapo na wamefuzu kwa uchunguzi... Anyway huwezi kuishi na dhambi ya uongo miaka yote. Lazima useme tu. Issue ni kuwa kaisemea kwenye vyombo vya habariAny way miandiko yao inafanana basi.
It was a minimal estimate.Ardhi ni miaka minne mpaka mitano mkuu, kutegemea na kozi husika.