Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Wataalamu wa vita wanasema" unapo panga kumshambulia adui kwa mbinu hizi nae adui anapanga mashambulizi makubwa kwa ajili yako kwa mbinu zake".

Asante kwa muda wako ulio nipatia mkuu.

Karibu mkuu
 
Something like that in reality. So wanadai katiba mpya, ili kipindi Cha mzozano wakuabliane kwanza kuwa na Tume huru na mambo Kama hayo wakati Katiba mpya inajadiliwa
Kwa hiyo basi, tuseme lengo la CHADEMA na matumaini yao makubwa ni kwenye matokeo ya "muda mrefu".
Wapiganie Tume Huru sasa hivi ipatikane, ili watakaposhiriki uchaguzi 2025 wawe na wawakilishi wengi Bungeni, ambako huko sasa watalianzisha la Katiba Mpya.

Sitakuwa na hoja dhidi ya hili.
 
Kwani kusudi kuu la haya maridhiano ni madhira ya utawala uliopita au mbinu za Chadema kui ondosha CCM toka kuanzishwa kwake kuonekana kugonga mwamba ?
Hivi Kuna mtawala anaweza fanya maridhiano na failure? JPM mwenyewe alielewa moto wa Chadema ikabidi anunue wabunge na madiwani wetu.

Ni hivi tumeridhiana Ili ukatili wa awamu ya 5 usiwahi jirudia Tena. Na maridhiano yatazaa katiba mpya
 
Hamna uhakika

Lini ?
Nani Hana uhakika? Kwani hauoni tofauti kati ya siasa za JPM na Sasa? Umesikia Leo kwamba hakuna mpinzani atakamatwa maana hayo mambo zamani hayakuwepo. Ilikua mkutano wa Chadema lazima uzuiwe na Polisi.

Kuhusu lini? Rais keshasema ataunda tume hivi karibuni Sasa si usubiri ikiundwa ndio uone kama katiba haitapatikana.

Ni either mjiunge na maridhiano au mtakufa kwa chuki tu maana there's no way tutarudi kwenye siasa za JPM. Nchi imeshakombolewa badilisheni mindset.
 
ANC walipigana wakachukua nchi, CHADEMA inaonekana kilichobaki ni kupigana kupewa fursa za kujiunga na hao wanaopambana nao. Sasa kama huoni tofauti hiyo, sina uwezo zaidi wa kuielezea tofautti hiyo.
Fursa gani? Kwani kipindi Cha JPM wapinzani hawakupewa uwaziri na ubunge? Mbona Mbowe au Mnyika hawakwenda if at all vyeo ndio vinawapa hamasa? Yaani why would Lissu risk kupigwa risasi 16 if at all akienda CCM angekua anakula Bata?

Kuna vitu huwa unaongea siku hizi nashangaa, yaani mtu akatae uwaziri aje kukubali cheo Gani Sasa wakati hata ubunge Hana?

Get serious.....
 
siasa zetu zilifika mahali pabaya sana ulikuwa ni uadui badala ya kuifikiria nchi. wenzetu sidhani kama wako hivyo, kwenye mambo ya msingi ya nchi wanaungana na kuwa kitu kimoja, wao wote wapinzani na watawala kiu ya ni maendeleo ya nchi na ustawi wa jamii, sisi tunalilenga sana kukomoana na kuoneana bila huruma, naamini kabisa ili kuondoa hali hiyo ni lazima tu tuanze kwa hatua kama hii ili tuamini kumbe siasa za vyama vingi si uadui baade tutakuwa kama wenzetu democrat vs Republican. badala ya kubeza hebu tuoneni kama ni mwanzo mzuri, tutoke huu, angalia picha hii
 
Kinachoendelea ni wanasiasa kuungana kuwakandamiza wananchi.

Tukatae huu usanii unaoendelea maana sisi ndio tunaopoteza zaidi.

Kwani hakuna wa kuzungumzia hali ngumu za wananchi katika mazingira haya ambayo wote ni kitu kimoja.

Dhalimu alijaza wanaccm kwenye mabaraza ya madiwani, watendaji ni Makada wa CCM, wabunge wa CCM nk, kwanini hao hawawatei wananchi maana walijifanya wazalendo?
 
Ni misingi ipi ya CHADEMA iliyowekwa pembeni katika hayo maridhiano? Huoni kwamba ni mapema sana ku-speculate hayo? Hatujasikia mabadiliko yoyote ya msimamo wa CHADEMA katika mambo makuu ya kisiasa, kiuchumi, kijamii ikiwemo utawala bora, katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, “Covid-19”, n.k.

Ni ushauri mzuri kujipa muda tujionee ukweli wa maridhiano hayo kama tunajali mustakabali wa taifa.

Kwa wanaopenda msimamo wa late JPM wa kuviangamiza vyama vya upinzani haishangazi wao kutamani CHADEMA wawe na direct and total confrontational approach itakayowezesha vyombo vya dola kuangamiza viongozi, makada, wafuasi na chama kizima - literally. Enzi za Hitler ilijulikana kama Final Solution.
 
Ni chaka gani waliloingizwa hawa CHADEMA?

Na ni kwamba unahisi wameingizwa chaka au una uhakika kuwa wameingizwa huko? Kama una uhakika eleza ni Kwa namna gani...

By the way, kwanini usiamini kuwa Rais Samia na CCM yake ndiyo haswaaa wameingizwa chaka na CHADEMA?

Ndugu Kalamu usiishi jana. Ishi Kwa kuingalia leo na sasa..

Nisome vizuri Kalamu, kwamba, mimi naamini na kujua kuwa CCM na Samia ndiyo haswaaa wameshanyoosha maneno...

Sababu ni hizi zifuatazo:

1. Kinana unayefikiri ni mwana mikakati hodari, alikuwa katibu wa CCM karibu kipindi chote Cha urais wa JK. Huyu huyu Kinana na JK wake alishindwa sawia kuiua CHADEMA na badala yake walipofanikiwa kumuingiza yule dhalimu mdarakani, moto ukawawakia na wao pia. Hawakuamini..!!

2. Kama CHADEMA ingekuwa ya kufa, ingeweza kuuwawa wakati wa miaka karibu saba (2015 - 2021) ya utawala wa CCM ya John P. Magufuli aliyedhamiria kufanya hivyo Kwa njia za mkono wa chuma na kuvunja sheria na katiba. CHADEMA chini ya Mbowe freeman, haikufa wala kuugua...!!
 
MANDELA ALIFANYA NA MAKABURU Wajinga wachache Tanzania wanashangaa
 
I am deadly serious. As a matter of fact I have never been serious than this.

Hayo maswali uliyouliza ya kupewa vyeo ndiyo maswali hasa ya kujiuliza wakati huu; lakini pia ni lazima ujue tofauti ya wakati ule na sasa.
Kwa hiyo usidhani kuuliza kwako maswali hayo kunaondoa uhalali wa hayo kuwa msukumo wakati huu kwa viongozi wa CHADEMA kuiona kuwa fursa.

Na kwa kweli, umeuliza maswali ya ajabu kidogo. Itakuwaje mtu kama Tundu Lissu aliyepitia katika hali ngumu vile, halafu leo hii asahau yote hayo na kuachana na misingi ya anayoyaamini na kuyapigania!

Hili ni swali atakaloulizwa hapo itakapobainika na yeye kaingia kwenye mtego.
Kwa ujumla, itasikitisha sana.
 
Mkuu 'Johnson Fundi', ninakubaliana kwa kiasi kikubwa kwa haya uliyoandika hapa, lakini usichukulie kuwa ni "kubeza" tunapohoji mwelekeo wa maridhiano kuonekana kama kuna chama kinajiondoa kwenye misingi wanayoiamini na kuonekana kama waliyohoji huko nyuma sasa yanakubalika au yanakuwa hayana uzito wa kuyakataa.

Hakuna anayetetea uhasama hapa kati ya vyama. Kwani huko siku za nyuma kabla ya awamu ya "uhasama" vyama vilikuwa havifanyi siasa zao vizuri tu?
Kwa nini sehemu ya huo mpito ya uhasama ndiyo kiwe kipimo cha kubadili yaliyokuwepo siku zote?
 
CUF na TLP walifanya hivyo mkawatukana kuwa wamenunuliwa
 
Lengo la chama chochote ni kupata nafasi ya kushika madaraka na kutekeleza wanayoyasimamia.

Sawa, CHADEMA hawajatangaza lolote kuhusu majadiliano yao na CCM, na hilo tatizo jingine linaanzia hapo; huo usiri mkubwa huku yanayoonekana yakiashiria uelekeo wa kutoka kwenye mstari, kama hiyo adhma ya kushika mamlaka kamili kama chama.

Huo usiri mkubwa ni wa kitu gani? Wapenzi na wanachama wao wastushwe tu dakika za mwisho kwamba chama chao kimekwishatekwa?

Hili la "...wanaopenda msimamo wa late Magufuli kuviangamiza vyama...", lisije likawa ndiyo fimbo ya kuwapigia na kuwanyamazisha watu wasihoji wanayoona yakiendelea, ambayo hawakutegemea kuyaona.

"Kujipa muda na kusubiri..." ni jambo zuri, lakini wakati huo huo ieleweke kwamba dalili zinapoonyeshwa kwa vitendo na maneno juu ya mambo kadhaa kuhusu maafikiano, ni lazima watu waanze ku'deduce' na kuuliza kulikoni juu ya hayo maridhiano ya siri kubwa.
 
Na kwa kweli, umeuliza maswali ya ajabu kidogo. Itakuwaje mtu kama Tundu Lissu aliyepitia katika hali ngumu vile, halafu leo hii asahau yote hayo na kuachana na misingi ya anayoyaamini na kuyapigania!
Lissu kaacha nini? Yaani Lissu aliyepigwa risasi Bado akarudi kupambana na JPM kwenye chaguzi ndio eti asalimu amri wakati wa Rais "mpole" kama Dr Samia?

Yaani asisalimu amri kipindi Cha kampeni then sahivi akiwa hana hofu ya kuuawa ndio aogope sijui alainike?

Mkuu you need to take a break from politics. Your analysis is below par or rather abysmal and biased.
 
La kuwa sehemu ya CCM iliyowakandamiza wakati wote huu. Badala ya kuwakandamiza kwa maumivu, sasa inawakandamiza kwa kuwaondoa kwenye lengo lao kuu la kushika madaraka ya nchi.

Nimekusoma vizuri kabisa na kukuelewa, nami nikueleza kwamba, inawezekana kabisa CHADEMA ilipata heshima kubwa wakati wa Magufuli kuliko wakati mwingine wowote. Hii turufu waliyokwishaipata, sasa inaonekana kama wanataka kuipoteza kimzahamzaha tu chini ya Samia.

Siwezi kamwe kum'underestimate' Kinana; na anakuwa hatari zaidi anapounganishwa na Samia. Hawa hawatumii njia za maumivu, wao wanatumia njia za laini tu kummaliza mpinzani wao.
 
Weird analysis!! Embu tuongee ukweli hivi kwa jinsi Samia alivyoji potray kuwa fair politically, je ukitokea uchaguzi Leo Mbowe hatorudi bungeni?? Yaani kwanini kipindi Cha Samia ambapo Mbowe yupo huru kufanya chochote ndio ategemee cheo CCM??

Kipindi Cha JPM Kuna mpinzani alikua na uhakika wa kushinda Jimbo au kata? So Ile ilikua ni motisha tosha kwa wapinzani kuhamia CCM Ili kusecure political future. Na ukweli wapinzani wengi mnoo walihamia CCM sio sababu ya kununuliwa Bali kuokoa political career.

Sasa kwa kuangalia hizo scenario mbili, je kwanini Lissu au Mbowe wasihamie CCM ya 2020 ambayo Kulikua hakuna hope ya upinzani kupata uongozi ILA wahamie CCM ya 2023 ambapo upinzani una matumaini ya kubeba sio tu majimbo zaidi ya 100 Bali Dola kabisa???
 
Nevermind, let it be abysmal, that is of the least worry to me.
But as we have agreed between us, let time speak for itself.
 
Siwezi kamwe kum'underestimate' Kinana; na anakuwa hatari zaidi anapounganishwa na Samia. Hawa hawatumii njia za maumivu, wao wanatumia njia za laini tu kummaliza mpinzani wao.
Kinana yupi? He's overrated, hivi si ndio huyu alikua Katibu mkuu kipindi CCM inapata heaviest losses tokea vyama vingi vianze 2014-15!!

Kama sio NEC, CCM ilikua imefia mikononi mwa kinana. Mawaziri mzigo walimshinda ndio sembuse Chadema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…