Mashariki ya Kati mfumo wa GPS haufanyi kazi

Mashariki ya Kati mfumo wa GPS haufanyi kazi

Tatizo la Marekani na washirika wake wanaidekeza mno Israel kiasi cha Israel kujiona ina haki ya kufanya chochote bila kuguswa.
Nafikiri kuanzia sasa Israel na washirika wake watakuwa na akili.

Vuta picha Israel ni taifa lenye nuclear lakini Iran Amepiga ndani ya Israel pamoja na onto kutoma kwa Marekani lakini kapiga.

Sasa nchi inayoamua kujilipua kama Iran ni hatari. Ina maana imeshajiandaa kupoteza. Na kwa tafsiri nyengine Iran ina nuclear tayari.

Swali linabaki; Israel, Amerika na washirika wake wapo tayari kupoteza? Kitakachotokea sidhani kama Amerika yupo tayari kukiruhusu. Kwa sababu middle East yote itachafuka ile. Iran na washirika wake hawatokubali kuanguka peke yao.

Kuanzia UAE, Saudi Arabia huko kote patachimbika. Yemen, Iraq, Lebanon, Jordan, Syria yaani eneo lote litaharibika. Marekani na washirika wao wapo tayari ku sacrifice hayo yote? Na historia ikubali imwandike yeye ndiye chanzo cha vita kwa kumlea vibaya Israel.

Na Jordan kwa kuruhusu anga yake itumike na mifano aliyoiana kilichowapata Israel sidhani kama atathubutu tena kwa Iran ilichokifanya.
 
Wataamua sasa Kusuka au Kunyoa..
Atajifikiria mara mbili kwa sababu alichokifanya yaani hapo Israel ilijipanga vya kutosha na kapata msaada wa marafiki zake wakubwa wa dunia ila bado athari za moja kwa moja kazipata.
Israel inabidi awe makini sana.

Ila mimi binafsi namlaumu Netanyahu. Huyu hafai kabisa na ndiye aliyewaletea matatizo yote haya raia wa Israel. Amani ya Israel kwa kipindi hiki cha sasa inabidi Netanyahu athlete madarakani.

Missile hii ikipita juu ya bunge lao Israel.
 

Attachments

  • Screenshot_20240414_033344_X.jpg
    Screenshot_20240414_033344_X.jpg
    277.3 KB · Views: 4
Mkuu vita sio kama mnavyofikiria huo sio mpira wa Man U
Nimeshuhudia vita ya Iraq na Iran na pia Iraq alipovamia Kuwait mpaka mwisho
Vita huwa haina mshindi hata kama tunauma upande mmoja kwa mapenzi lakini vita ina hasara kubwa sana
Unajua sasa hivi Israel wanarundika toilet paper na maji majumbani kuna uzi humu hebu fuatilia breaking news ndio nimesoma mda sio mrefu

Niliishi kwa tende na maji mwezi mzima na sio utani
I was in front bro
Pole Mkuu, hapa wachangiaji ni below 30 so Bado ujana unawasumbua
 
Bro vitu vimeingia ndani ya israel despite kujam GPS na maelecyromic warafare devices ya wazungu wala nini drones zinatembea kilometa 1500 na zinafika zinakotakiwa zifike mpersia mwamba aisee hii naona ni kutuma ujumbe kwa ulimwengu oneni ,je mmeona na kweli tumeona.
Mengi yameshushwa huko huko
Yaliyopita hayana athari,yameangukia kwenye open space
 
Kwani chanzo cha vita ya iran na Israel ni nini?
 
Anaweza maana asipofanya ataonekana hawezi katumia muda kufikiri na kujipanga offensive and defensive.
Israel ana disadvantage maana yeye anaweza shambuliwa na pande nyingi kwa mpigo ambapo atapigwa sehemu kadhaa maana akitumiwa drones 200 na ballistic 100 hawezi tungua zote ndo maana kajam GPS kwa msaada wa Marekani
Mnaleta hadithi za Saddam Hussein. Atakamatwa mtu anyongwe hadharani halafu muanze kulialia.
 
Back
Top Bottom