Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

Tunataka twende sawa. Sijahongwa na wala sitahongwa.
Hoja zako 3 ni nyepesi sana kwa tukio hili na hazina lolote
MOJA,
Hoja yako ya mwanzo, naijibu kama ifuatavyo. Mtakubaliana na mimi kuwa mifumo mingi ya kiutendaji hapa nchini chini ya katiba hii ni "one man show" yaani utendaji wa kile anachotaka boss. Na boss hapa ni rais ambaye katiba inamfanya awe mfalme. Ile tume ilihoji wana ccm wengi ambao ndio walikuwa na nafasi ya kufika mbele ya tume na kuongea. Ni kama kampeni flani hivi iliendelea ili kulinda mfumo uliopo usianguke. Nyerere aliliona hilo na kutumia busara yake akashauri vingine. Pamoja na hayo wakaficha nyenzo muhimu ambazo zinaendeleza mfumo wao wa kama chama kimoja vile japo wamezema sasa tunaruhusu vyama vingi. TEC hawakuongeza neno kwa kuwa mabadiliko ni mchakato. Pia hakukua na umafia kwa kiwango hiki tunachokishuhudia sasa. Mimi sio mkatoriki ila nawatetea kwa kuwa jamaa wapo smart.

MBILI,
Kuhusu mihimili, ukiisoma vizuri ile hukumu kwa jicho la tatu utagundua inajikanganya. Sasa hapa itategemea kama uwezo huo unao. Kukusaidia hint, kunapahala hukumu inasema, japokuwa mashart ya mkataba yanakinzana na vifungu vya katiba, havizuii mkataba huu kuwa haufai/kutekelezeka. pia hukumu ikasema kwa kuficha inaheshimu maamuzi ya bunge, shit.
Hapo baada tu ya kutolewa hukumu ile kwa tyming ya kumchinja kobe. nguvu kubwa ikatumika kuwadhibiti wahusika wasiendelee na jitihada za kuupinga. Nani mwengine asaidie, walio madarakani wanaitumia dola kufinya umma ili mambo yao yaende. Nani wa kutetea. TEC wakaona wasaidie bila kutumbukiza hoja za udini. Mbona wangetaka kutumia hoja hizo zipo ila kuepuka kuchanganya siasa na dini wakazikwepa.

TATU
Mbona vyombo hivi vya dini huwa vinajichanganya kuombea serikali na kufungua matukio kama sherehe za serikali za kitaifa ila hamsemi vinachanganya siasa na dini. pale vikikemea maovu ya serikali ndio mnakuja kukinga eti vyombo hivi vya dini visichanganye siasa na dini. BAKWATA wanaweza wakatoa hoja zao kisomi kama wenzao bila kuchanganya siasa na dini. Upo hapo! Wakasema na kuingerea vipengere vya mkataba kama jinsi vilivyo. Hakuna shida kama wataonyesha mazuri yaliopo na wakatetea. Sasa wakishindwa kutetea hoja wakatumia UDINI itajulikana. Wewe embu niambie kipengere cha udini kilichopo kwenye hoja za TEC. Sasa vyombo vingine vijikite kwenye hoja za mkataba kama wenzao TEC sio hoja za kidini.

HITIMISHO.
Mfano wa hoja za kidini ambazo TEC wangekosea ni pale ambapo wangesema katika maadhimio yao kuwa mfano; kiongozi muislamu amechagua kampuni kutoka nchi ya kiislamu. Hiyo ni point moja ya udini niliiitolea mfano, zipo nyingi naweza kuorodhesha zikafika 10. Ila huko hakufai mana haileta afya katika undugu wetu Tanzania kama sio Tanganyika. Mleta mada hoja zako nyepesi na hazina mashiko. Nawasilisha nukta.
( kuna wale wakosoaji wakikosa hoja wanaanza kuvamia spelling na herufi, angalizo sikijui vizuri kiswahili, kosoa hoja sio herufi
. Mimi ni Mtanzania ninaejitahidi kukijua vizuri Kiingereza mana Ccm imeshindwa kunyanyua uchumi kiasi kwamba kiswahili sio lugha ya wawekezaji waajili wanayoitumia maofisini na ku-interview waajiliwa wapya)
 
Watamke maaskofu, mashehe, wapagani au dini nyingine yoyote.
Mkataba ni wakilaghai na haufai unaondoa utu wetu.
Mambo ya udini yanaletwa na wanaofaidika na mkataba ili kutuvuruga mkataba upite.
 
Wewe mdini mkubwa ndio hujielewi.
Ngoja Bakwata watoe tamko la kuunga mkono uwekezaji kwenye Bandari halafu tuone Serikali itamsikiliza nani.

Wakati wa Magufuli Kanisa lilikuwa wapi?

Si kulikuwa na mambo mengi ya hivyo ,kwakuwa kanisa lilinufaika na utawala wa magufuli halikutoa tamko hata moja.

Kwanini kanisa huwa linafufuka mtawala akiwa Mwislaam.

Pale Bandarini kuna Maslahi gani ya kanisa?

Mnamtaja taja magufuli wa nini kwenye hili la bandari???? Mzee ashakufa yule!!!! Kwaiyo kwa sababu hakutajwa basi serikali ikikosea tusiseme?

Ulitaka tuseme nini kwenye utawala wa magufuli? Na kwann wewe haukusema kwenye utawala wa magufuli kama uliona mapungufu?
 
Mapadree waendelee na jukumu lao la kuchunga kondoo waliopotea haya mengine wayaache.
 
Ndo hapo.

Yaaani kuna watu wanajiona kama wao ndo wanaongoza nchi.

Sasa naelewa kwa nini China walipiga marufuku upuuzi huu wa dini
Kwanini mmeheuka kutokana na tamko la maaskofu?mbona masheikh naowameongea tena walikuwa wa kwanza au wao hawana athari kwa kauli zao?acheni kuwadharau masheikh bhanaa.
 
punguza jazba ....umeshaambiwa bandari haiuzwi tena kwa upole na upendo.

kunywa maji
Hakuna anayeuza bandari ni uwekezaji unaokwenda kufanyika ili iweze kulingana na hadhi ya kuhudumia nchi nane zinazotuzunguka.

Huwezi kuuza lango la nchi, bandari na viwanja vya ndege huwezi kuuza hizo ni njia za kuingia na kutoka kwenye nchi husika.
 
Ndo hapo.

Yaaani kuna watu wanajiona kama wao ndo wanaongoza nchi.

Sasa naelewa kwa nini China walipiga marufuku upuuzi huu wa dini
Halafu hivi ulivyo unasema we ni mkristo na unampenda Yesu. We ni mjukuu wa mudi bila shaka, hakuna mkristo wa namna yako
 
Mkristo gani unauponda ukristo kila siku? Nini kinakuzuia kuhamia ambapo unapaona pako sahihi kwa upande wako?
Tofauti yangu na wewe mimi sipo kidini. Mimi nipo kwenye kweli na imeandikwa kweli itatuweka huru!
 
1. Wanadai Serikali iachane na Mkataba wa Bandari kwa sababu wananchi wamegawanyika kuhusu mkataba huo!

Swali langu kwao, Ni jambo lipi nchi hii limewai kukubaliwa na asilimia 100 ya wananchi wote? Kwenye Mfumo wa vyama vingi, Mbona asilimia kubwa ya Wananchi walikataa mfumo huo ila Serikali wakauunga mkono! Je kwa nini hawakutoa tamko kipindi icho kutaka nchi iendelee kuwa ya Chama kimoja? Kwa tamko lao walilosema maamuzi ya wananchi yaheshimiwe basi wanaunga mkono Serikali i reverse maamuzi yake ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi na turudi kwenye mfumo wa Chama kimoja?

2. Kwenye tamko lao wanadai Mihimili ya dola iheshimiwe. Swali langu kwao! Juzi Mahakama Kuu wametoa maamuzi ya kutupilia mbali maombi ya watu walioshtaki mkataba wa Bandari.

Sasa kwa nini wanataka mihimili ya dola iheshimiwe na wao hawataki kuheshimu maamuzi ya Mahakama? Kama Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 hasa ibara ya 107A inasema Mahakama ndio Mhimili wa mwisho katika kutoa haki sasa kwa nini hawaheshimu maamuzi ya Mahakama alafu wanatoa tamko kusema Mihimili ya dola iheshimiwe?

3. Wao wanavyotoa tamko kutaka Serikali iachane na mkataba wa bandari kesho BAKWATA wakitoa tamko Serikali iendelee na mkataba wa Bandari wanataka Serikali imsikilize nani? Kesho kutwa mabudha wakitoa tamko pia wanataka Serikali imsikilize nani kati yao?

Kwa hali hii sasa nimejua kwa nini mapadre wa kanisa katoliki walishtakiwa kwa kuhamasisha mauaji ya kimbari Rwanda!

Pia soma
- News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
Kuna maswali na mimi nataka nikuulize. Kwa hiyo, kama wewe umeweza kusema hivyo ulivyosema, unadhani TEC ndio hawawezi kusema hivyo hivyo walivyosema?

Hapa sina majibu ya TEC maana mimi si msemaji wao, lakini kutokana na maswali yako na mimi nataka niseme haya yafuatayo na nikuulize pia.
1. Conclusion, ya andiko lako ni "erroneous" - maana halitokani na premises ulizozitoa hapo juu. Kwa hili, nikuulize hivi: je, kwa vile baadhi ya wanaume huwa wanakamatwa matukio ya ujambazi na mauaji na kama na wewe ni mwanaume, je na wewe tunaweza kusema ni jambazi au muuaji? Nauliza hivi kwa sababu umeleta mambo ya mauji ya Rwandwa kwa kusema Mapadre Wakatoliki Rwanda walishiriki kwenye mauaji au una ushahidi kwamba Mapadri Wakatoliki Tanzania ndio waliofanya mauaji Rwanda? Nataka ujenge hoja kuonyesha maoni ya TEC kuhusu bandari yanaishiaje kwenye mauaji kama ya Rwanda?

2. Kama wewe ulivyoona una haki ya kuandika hayo uliyoandika - ambayo ni maoni yako - je, unadhani Maaskofu wa TEC si Watanzania wanaoweza kutoa maoni yao kuhusu mambo yanayowahusu kama Watanzania? Ni sheria gani imewakataza wasitoe maoni wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema:
"Article 18: Every person -
(a) has a freedom of opinion and expression of his ideas;
(b) has a right to seek, receive and, or disseminate information regardless of national boundaries;
(c) has the freedom to communicate and a freedom with protection from interference from his communication; and
(d) has a right to be informed at all times of various important events of life and activities of the people and also of issues of importance to society."

Article 27(1): "Every person has the duty to protect the natural resources of the United Republic, the property of the state authority, all property collectively owned by the people, and also to respect another person’s property.
(2) All persons shall be required by law to safeguard the property of the state authority and all property collectively owned by the people, to combat all forms of waste and squander, and to manage the national economy assiduously with the attitude of people who are masters of the destiny of their nation."

3. Je, unadhani hizi Ibara mbili au kama kuna Ibara zingine kwenye Katiba kama hizi haziwahusu TEC au viongozi wa dini Tanzania? Kama ndiyo unaweza kuleta 'justification' yake?

4. Je, mahakama ikishatoa uamuzi, hakuna mtu anayeweza kuwa na opinion tofauti na huo uamuzi wa mahakama? Is it illegal? Kama hivyo ndivyo, kwa nini huwa kuna rufaa na hata kama rufaa zikigonga mwamba hapa nchini, kwa nini watu wengine huwa wanaenda the Eastern Court of Justice (EACJ) au ile ya Afrika? Au je hata kama huko watashindwa, hawawezi kubaki na opinion yao hiyo na kufanya hivyo huwa ni kosa?

Mwaka 2010 Chief Justice (rtd) Barnabas Albert Samatta alitoa public lecture kuhusu "Judicial Protection of Democratic Values: The Judgement of the Court of Appeal on Independent Candidates". Hapa naweka extracts 2 za aliyosema kuhusu hiyo hukumu ya Court of Appeal: "Our Court of Appeal's function is to interpret the provisions of the Constitution and arrive at a correct and just decision and not to 'half-interpret those provisions and thereafter surrender the noble function to an organ un-authorised by law and ill-equipped to perform it...The Court of Appeal expressed the opinion, among others, that courts in this country do not have power to amend the Constitution, that function being that of Parliament. With respect, that observation is perfectly correct, but it was not necessary in the resolution of the issues before the Court. Rev Mtikila did not ask the High Court (or the Court of Appeal itself) to amend the paramount law of the land. What he asked to do was to declare that the constitutional amendments in question were unconstitutional on the ground that they were violative of Article 21 of the Constitution. That is not a prayer to usurp parliamentary powers. The petitioner's contention was in essence that the purported amendments could not in law become part of the Constitution as they were void ab initio or, to use a modern expression, void from their inceptions (p. 21).

"Unyielding courage of judges is a priceless asset of any country. There is no substitute for it. Judges must not hesitate to make decisions they consider just however unpopular those decisions are likely to be to Parliament, the Executive or political parties, including the ruling party and regardless of their impact on the relations between the Judiciary and the other pillars of State..." (p. 32). Je, kwa haya maoni ya Judge (rtd) Samatta kuhusu hiyo hukumu anayoiongelea, unasemaje?

5. Tukitaka tunufaike na mijadala tuwe tunajikita kwenye hoja kuliko kuwashambulia watoa hoja. Watanzania wote wana haki ya kutoa maoni kwa serikali yao na kama wana hiyo haki, wewe usiye msemaji wa serikali huwezi kuwa msemaji wake. Mara nyingi viongozi wa serikali wamekuwa wakisema "serikali yenu ni sikivu" which means inajua kama kuna issue wananchi watakiongea na serikali itatolea ufafanuzi jambo hilo. Au hata kama serikali imetolea ufafanuzi wananchi wanaweza bado wakawa na dukuduku kuuliza maswali mengine na serikali inayowajibika kwa wananchi inawajibu wa 'to take care of it'. Sasa wewe mheshimiwa sijui hapa ndiyo unatoa kauli ya serikali au na wewe unatoa tu maoni, lakini hutaki wengine watoe maoni, je hiyo exlusive right unatoa wapi? I hope utaweza kujibu bila kunishambulia na mimi kama ambavyo hata mimi sijakushambulia. Asante.
 
Ushauri wao tumeusikia na tumeuchukua lakini hatuutaki.
Kwani shida iko wapi? Ni mangapi wewe uliyokwishataka yafanyike na hayajafanyika hadi leo? Kwani ikitokea hivyo ina maana unakuwa umepoteza na kama ni kupoteza wewe hujawahi kupoteza na unadhani TEC ndio watakuwa wa kwanza kupoteza katika hili? Hata Yohane Mbatizaji na Yesu walipoteza. Walitaka watu wabadilike, laki wakageuziwa kibao. Hivyo, rejection of advice or an opinion is a social phenomenon!
 
BARUA YA WAZI KWA RAISI WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA LA KATOLIKI TANZANIA DR GERVAS NYAISONGA; KUFUATIA SAKATA LA UWEKEZAJI WA BANDARI KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA SERIKALI YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

Imeandikwa na;
BY LUGETE MUSSA LUGETE
Na. Comred Mbwana Allyamtu-CMCA

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga amani ya Mungu iwe nawe,rehema na baraka zake zikujaze upendo,amani ,utulivu na busara.

Naitwa Lugete Mussa Lugete, mchambuzi wa siasa za Kimataifa, Mwanamajumui wa Afrika na Mwanahistoria, kwa pamoja na Comred Mbwana Allyamtu-CMCA tumeamua kuandika barua hii ya wazi kwako kufuatia waraka kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania kupinga uwekezaji wa Bandari, ambapo wewe ndio Raisi wa TEC.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga, naanza nukuu mbalimbali kutoka kwa Mwalimu mkongwe na mwenye heshima kubwa ndani ya Kanisa la katoliki St Augustine kutoka Algeria.

"Upendo wa Mungu hauna mipaka ya dini, bali unawakumbatia watu wote bila ubaguzi." - Mtakatifu Augustine

"Kuabudu ni kujitolea kwa Mungu, siyo kujitenga na watu wengine." - Mtakatifu Augustine

"Uhuru wa kuabudu ni haki ya kila mtu, na hakuna dini inayopaswa kupewa upendeleo." - Mtakatifu Augustine.

Tarehe 20/8/2023 Baraza la Maaskofu Tanzania lilitoa waraka kupinga uwekezaji wa Bandari kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaani U.A.E. Hoja za TEC ni kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,hivyo serikali haipaswi kupuuza sauti ya umma juu ya mapungufu ya mkataba wa Bandari.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga, naomba unisamehe Kwa kuandika barua hii Kwa sababu miezi miwili iliyopita viongozi mbalimbali wa dini waliitwa ikulu na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Dr Samia Suluhu Hassan ili watoe maoni yao kuhusu sakata la Bandari, Miongoni mwa waliozungumza ni Baba Askofu Dr Kalikawe Bagonza, Raisi aliwaambia kwamba maoni yao yatafanyiwa kazi Kwa sababu bado kuna nafasi za kujadiliana na kuzungumza kati ya wawekezaji na serikali ya Tanzania.

Kiufupi ni kwamba serikali haijachelewa, nimesikitishwa na usaliti uliofanywa na TEC Kwa serikali Kwa sababu maoni yenu yanafanyiwa kazi na mazungumzo ya utekelezaji wa mkataba bado hayajaanza.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga; naomba nianze kueleza sintofahamu kati ya viongozi wa kanisa la katoliki na makundi kadhaa ya wapigania Uhuru wa Tanganyika tangu mwaka 1920.

Baada ya vita ya kwanza ya dunia mwaka 1918 kundi la Wahafidhina yaani Triple Alliance lilipoteza pambano ambapo wanachama wake kama Ujerumani, Muungano wa Austria na Hungary, Italia na Dola ya Kiislamu ya Ottoman walipoteza na kuadhibiwa kikanuni na mkutano wa Versailles Paris wa mwaka 1919.

Hapa nchini Tanganyika Kleist Mbuwane Sykes mtoto wa shujaa wa Kizulu Mbuwane Sykes, alianza harakati za ukombozi wa Kifikra kutaka Watanganyika wapate kutambua haki zao, baadae akakutana na Dr James Emman Aggrey akiwa mmisheni Dar es Salaam na kumuomba ushauri kuhusu kuanzisha chama Cha Wafanyakazi,kwakuwa Dr James Emman Aggrey alikuwa analinda maslahi ya kanisa la katoliki Afrika Mashariki,akaandika waraka kwenda Vatican kuhusu hofu yake kwamba huenda miaka ijayo Tanganyika ikatumbukia Kwa waislamu,

Wakristo wa kanisa la katoliki wanapaswa kuwa macho Kwa sababu kanisa lina mali nyingi, Kuanzia hapo chama Cha TAA kikaanzishwa tayali vuguvugu za udini kati ya waislamu na Wakatoliki zilianza, mwaka 1949 Kleist Mbuwane Sykes aliaga dunia na kuwaachia chama wanae wa kiume wanne ambao ni Abdulrahd Sykes, Ali Sykes, Ayoub Sykes na Abbas Sykes, Mwaka 1952 Joseph Kasela Bantu alimpeleka Mwalimu Nyerere kariakoo kuonana na familia ya Sykes na mipango ya Nyerere kushika dola ilikuwa chini ya Dr Vedastus Kyaruz.

Uchaguzi wa mwaka 1954 ulikumbwa na sintofahamu nyingi na bila shaka mkono wa kanisa la katoliki ulihusika mpaka Mwalimu Nyerere akamshinda Abdulrahd Sykes.

Mara baada ya Uhuru wa Tanganyika ukazuka mgogoro kati ya kanisa la katoliki na waislamu hasa 1962_1970 ambapo Mwalimu Nyerere alimtumia Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa kuwadhibiti familia ya Sykes.

Historia ya kanisa katoliki Tanzania imeanza toka mwaka 1880, imekuwa hadi kufikia mwaka wa 1960 Kanisa katoliki likawa taasisi kubwa inayomiliki mamilioni ya dola ya misaada inayopokelewa kutoka wahisani na wafadhili walioko katika ulimwengu wa Kikristo.

Kanisa katoliki sasa hivi linahodhi mahospitali, misururu ya ndege binafsi, viwanja vya ndege, makampuni ya uchapaji na mitambo ya kupiga chapa, stesheni za radio na magazeti.

Kanisa katoliki pia limekuwa na nguvu na udhibiti wa mambo kiasi kwamba wakati mwingine watendaji, hasa Wakristo katika serikali na ndani ya chama tawala CCM hawajui utii wao upo kwa nani, serikalini au katika Kanisa?.

Ni katika kuchanganyikiwa huku kwa watendaji wa serikali kuhusu uhusiano wao na Kanisa na serikali ndiko kulikoamsha kutoaminiana kati ya Waislam na serikali mara tu baada ya uhuru kupatikana.

Serikali ikaonekana kama moja ya taasisi za Kanisa katoliki na Waislam wakiwa ni watazamaji tu, Mara baada ya uhuru Kanisa katoliki likaangalia nafasi yake na serikali mpya iliyokuwa madarakani, Wakati wa kudai uhuru Kanisa lilijiweka mbali na siasa na ikaonekana kuwa Kanisa lilikuwa likiheshim ule mpaka kati ya dini na siasa.

Wakati ule mgongano kati ya Kanisa na serikali haukupata kusikika hata kidogo.

Baada ya uhuru kupatikana tu na serikali ikawa mikononi mwa wananchi, Kanisa katoliki likaanza kusikika likisema kuwa lina haki na wajibu kuwa na ushawishi ndani ya serikali, kuikosoa serikali na kuingooza pale inapoona serikali haifanyi mambo sawa kwa matarajio yake, Katika msimamo huu mpya, Kanisa likajipa fursa ya kuwa msemaji wa watu.

Huu ulikuwa ni mwelekeo mpya katika mambo ya siasa na utawala.

Hapa ndio kanisa katoliki likatengeza mfumo wa kanisa ndani ya serikali, mfano wa hayo ni pamoja na..

Endapo waislam watakuwa na hoja nzito kwa serikali lakini Wakatoliki wakaipinga basi hakuna litalokuwa,
Lakini wakristo wakitaka kwa serikali hata waislam wasipewe habari jambo litakuwa, Kwa mfano mahakama ya kadhi vs Mou.

Pili, kama jambo halijapata ridhaa ya maaskofu wa Katoliki haliwezi kuwa kama ambavyo haikuweza Zanzibar kujiunga na OIC na hivi sasa Tanzania haiwezi kujiunga na jumuiya hiyo kwa sababu maaskofu hawataki, mfumo katoliki hautaki.

Tatu, kanisa katoliki limejiimarisha na kujipa uhalali ambao kiasi cha kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika hadi kuomba radhi, na kuvitisha na hata kuvikemea vyombo vya dola na kusalimu amri.

Nne, kubanwa kwa waislam kupitia Sheria ya Ugaidi, Mkataba baina ya Serikarli na Kanisa (MoU), Mauaji ya Mwembe Chai, Maandamano ya Dibagula, mauaji ya Waislam Zanzibar, Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwaomba radhi maaskofu Sumbawanga, Samuell Malecela kumtaka aliyewaambia maaskofu wa Arusha wavue majoho ya dini na wavae ya siasa awaombe radhi.

Haya yote yamekuwa ni matokeo ya kanisa katoliki kujiona kuwa ndilo lina mamlaka pekee ya kuhodhi mambo yote ndani ya Tanzania.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga, naomba unisamehe Kwa kuandika barua hii ya wazi Kwa sababu tangu zamani kanisa limejipa nguvu ya kuamua hatma ya wengi kuliko uhalisia, nadhani hofu ya kanisa ni juu ya mizigo yao inayopita bandarini Kwa unafuuu wa Kodi wa karibu asilimia 100, ikumbukwe kwamba kanisa la katoliki ndio taasisi yenye mashirika mengi hapa nchini kuliko taasisi yeyote ya kidini hivyo mnamizigo mingi kutoka Ulaya na Amerika.

Hilo jambo linazungumzika kuliko waraka ambao lengo lake ni kuwagawa wananchi ili wasiwe na imani na serikali,huo ni uasi dhidi ya serikali na athari zake ni mbaya na taifa linaweza kuingia kwenye migogoro isiyoisha.Hivyo tunaomba tuitunze tunu yetu ya amani Kwa sababu nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki zinaitegemea Tanzania kama sehemu yenye ustawi wa haki,usawa na amani,ndio maana nchi hizo kila zikikumbwa na machafuko Tanzania ndio kimbilio lao .

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga; naomba unisamehe Kwa kuandika barua hii Kwa sababu nataka kueleza Ajenda za Club Bilderberg dhidi ya mataifa ya Kiislamu. Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga.

Kundi la Bilderberg ni shirika rasmi la watu mashuhuri na viongozi wa kisiasa, biashara, na vyombo vya habari kutoka nchi mbalimbali duniani. Kundi hili lilianzishwa mwaka 1954 na Prince Bernhard wa Uholanzi, ambaye alikuwa mwanachama wa familia ya kifalme ya Uholanzi na alikuwa na uhusiano wa karibu na wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa duniani.

Lengo la kundi hili ni kulinda maslahi ya mabeberu dunia, kuthibiti mataifa ya kijamaa Kwa kivuli na vuguvugu za demokrasia, kulinda uhusiano kati ya Marekani na mataifa ya Ulaya,kutetea taifa la Israel dunia nzima na kupambana na mataifa ya Kiislamu ambayo ni kikwazo kwenye Ajenda yao ya NEW WORLD ORDER.

Lengo lingine la Kundi la Bilderberg ni kujadili masuala muhimu ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii duniani, na kutoa mapendekezo kwa viongozi wa serikali na biashara juu ya jinsi ya kukabiliana na masuala hayo.

Mkutano wa kwanza wa Kundi la Bilderberg ulifanyika katika Hoteli ya Bilderberg huko Oosterbeek, Uholanzi, ambayo ndiyo iliyotoa jina la kundi hilo.

Mkutano wa Kundi la Bilderberg ni siri na wajumbe hualikwa kwa njia ya faragha. Kila mwaka, mkutano hufanyika katika eneo tofauti duniani, na wajumbe huwa ni pamoja na watu mashuhuri kama vile wanasiasa, wafanyabiashara wakubwa, wanahabari, na wataalamu wa masuala mbalimbali.

Kundi la Bilderberg limekuwa likikosolewa kwa kuwa siri na kutokuwa na uwazi, na wengine wanadai kuwa kundi hilo linawakilisha maslahi ya watu wenye nguvu duniani na linaweza kuathiri maamuzi ya kisiasa na kiuchumi duniani. Hata hivyo, wajumbe wa Kundi la Bilderberg wanasema kuwa mkutano huo ni wa kujadili masuala muhimu ya dunia .

Katika mkutano wa Bilderberg kiongozi wa Shirika la Ujasusi la Kanisa la katoliki duniani Black Pope ambaye ni mshauri namba Moja wa Papa , Black Pope au Generali wa kundi la Jesuit Society huingia katika mkutano wa Bilderberg ili kulinda heshima na maslahi ya kanisa duniani.

Mkutano wa Bilderberg na kundi lote haliungi mkono uislamu, mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kujitanua kiuchumi na kisiasa nje ya mashariki ya kati, ndio maana kanisa la katoliki hapa nchini kupitia Baraza la Maaskofu limepinga uwekezaji wa Bandari kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu yaani U.A.E. Kiongozi mkuu wa Shirika la Ujasusi la Kanisa la katoliki Generali Fr Arturo Sosa aliingia kwenye mkutano wa Bilderberg wa mwaka huu.

Miongoni mwa Ajenda zilizojadiliwa ni pamoja na kuthibiti mataifa ya Kiislamu na Kiarabu yanayojitanua Afrika, Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga kuna athari mbaya sana Kwa dini Moja kujipa nguvu na mamlaka ya kuishawishi serikali au umma kufuata matakwa yao huku dini zingine zikiwa kimya.Hapo waumini wa dini zingine hujiona wanyonge katika taifa lenye Uhuru wa Kuabudu.Kwa matamko na waraka mbalimbali za kanisa,hii inathibitisha kwamba mmejipa nguvu wenyewe,

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga; katika waraka wa TEC unasisitiza kuzingatiwa Kwa sauti ya wengi kwani ni sauti ya Mungu ambapo Kwa kilatini ni Vox Populi Vox dei.

Kuna matukio kadhaa yamewahi kutokea hapa nchini na kanisa au baraza la Maaskofu hawakutoa waraka au kukemea.

Naomba kuuliza maswali yafuatayo.

1. TEC inafahamu kwamba mwaka 1992 wakati Serikali inapitisha mfumo wa vyama vingi ulikuwa umekataliwa na asilimia 77 ya Watanzania? Hata hivyo serikali ikaamua uruhusiwe. Hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni sauti ya Mungu, na Sauti ya Kanisa la katoliki lilikaa kimya Kwa sababu ajenda ya vyama vingi ulikuwa ni mpango wa mabeberu hivyo kanisa lilipuuza sauti ya umma kukataa mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

2. TEC inafahamu kwamba mwaka 2001 baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar na mauaji ya wafuasi wa CUF mwezi Januari, asilimia 98 ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla walitaka kuwepo na mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na SMZ na SMT chini ya Mkapa haikutaka? Hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu.

3. TEC inafahamu kwamba mwaka 2014 maaskofu wote wa Katoliki Tanzania akiwemo Kardinali Pengo na wasaidizi wake walipokea mamilioni ya shilingi pesa taslimu na nyingine kwenye akaunti zao kama Askofu Nzigilwa (milioni 80 benki) na Kilaini (milioni 40 benki). Inajua fedha hizo zilitoka katika kampuni yenye makando kando ya rushwa ya kihistoria Tanzania. Wananchi wengi walipiga kelele lakini fedha hizo hazikurudi wala hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu.Kwa maana hiyo TEC iliunga mkono rushwa na kupuuza sauti ya umma.

4. Padri Kitima anasema kwa zaidi ya miaka 60 ama toka tupate uhuru bandari yetu haijawahi kuendeshwa na wageni. Hii ni kauli yake au ya maaskofu wa TEC? Ni kweli TEC haifahamu kwamba kwa zaidi ya miaka 22 Bandari yetu ya Dar imekuwa chini ya kampuni ya TICTS ikiendeshwa kwa ubia na kampuni toka Hong Kong (Hutchsons?). Kama wanafahamu, wanakumbuka wabia wazawa wa kampuni hiyo wanahusika kwenye kuwapa hela maaskofu kama Rugemalira na IPTL yake walivyofanya? Hili wamewahi kuwaambia waumini wao katika mimbari za ibada?

5. TEC wanafahamu kwamba mwaka 1998 kwenye mauaji pale Mwembechai walikufa wasio na hatia na ilikuwa rai ya mamilioni ya Watanzania kutaka kuwepo na suluhu ya kisiasa? Hakuna kumbukumbu za kanisa katoliki kupinga na kusema Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu.

6. Padri Kitima anasema wananchi wamelikataa Bunge? Ametumia kipimo gani cha Kikatiba? Maana wananchi wanalikataa Bunge kwa kutowachagua Wabunge kwenye Uchaguzi. Hii “Vox Populi Vox Dei” ya TEC imetumia kigezo gani? Wananchi wakikataa Bunge pia si wameikataa Serikali? TEC inaomba vipi busara ya Mheshimiwa Rais ambaye wakati huo huo inasema serikali yake imekataliwa? Kuna kuchanganyikiwa na haraka kubwa kwenye tamko la TEC hata namna lilivyochapwa na kupangiliwa. Inanipa mashaka kwamba chombo hiki muhimu cha Kanisa kimekubali kutumika kwa maslahi binafsi bila tafakari ya kutosha.

Je hii “Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu” ni wengi wapi hasa? Na mungu anayetajwa hapa ni nani? Usikute mungu anayetajwa na kusemwa asikilizwe ni mungu au miungu watu waliokuwa wanaingiza miamala kwenye akaunti za baadhi ya maaskofu wetu na viongozi wengine wa dini nenda rudi. Tujihadhari. Tusiigawa nchi kupitia madhabahu.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga hayo ni baadhi ya maswali kadhaa nimeyabuni ili kujenga hoja kwamba TEC inalinda maslahi yake kupitia kivuli cha sauti ya umma. Kama taifa tunapaswa kufikiri Kwa kina kama Kobe na kuona mbali kama tai.

Mwaka 2009 kulikuwa na vuguvugu la Tanzania kutaka kujiunga na OIC yaani Organization of Islamic Countries, kanisa lilipinga na Raisi Wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete alisemwa na kutukanwa ,nakumbuka kwenye Msiba wa Dr Baba Askofu Anthony Mayala Mwanza, Kadinali Pengo alitoa vijembe na kejeli Kwa serikali na hakuna kumbukumbu ya waraka wa kanisa au TEC kukemea Kwa sababu kwenye Biblia Kuna mstari wa "Heshimuni Mamraka" pia kuhusu waislamu kudai mahakama ya kadhi kwao wenyewe kanisa lilipinga na kupuuza sauti ya umma ambapo ni sauti ya Mungu Kwa mujibu wa Dr Charles Kitima.

Suala la TEC kutumia wino na maarifa yao kulinda maslahi yao bila kujali mpasuko katika taifa letu ni mbaya sana na linapaswa kuzungumzwa na kukemewa kabla ya taifa kuingia kwenye mazonge na songombingo ambazo zinaweza kuliingiza taifa vitani.

Dunia imeshuhudia migogoro mingi kutokana na dini moja kujipa nguvu, mamlaka na propaganda katika kulinda maslahi yao. Mfano nchini Rwanda viongozi wa kanisa la katoliki kama Askofu Ntihinyurwa, Augustine Misago ,Athanase Seromba na wengine zaidi ya therathini walihusika kumpa nguvu dikteka Generali Juvenile Habyalimana na kuanzisha Sheria na kanuni za kudumisha ukabila yaani AKAZU.

AKAZU ni kanuni na Sheria za kibaguzi zilizotungwa mwaka 1973 mara baada ya Meja Generali Juvenile Habyalimana kumpindua Raisi wa kwanza wa Rwanda Gregory Kayibanda.Akazu ililenga kuwapa nguvu na ushawishi Wahutu na kuwakandamiza Watutsi.Baada ya mauaji ya Kimbali Rwanda mwaka 1994 viongozi wa kanisa la katoliki baadhi walikamatwa na kufungwa jela baada ya mahakama kuwakuta na hatia.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga, nchini Burundi Generali Michel Micombero aliwatumia viongozi wa kanisa la katoliki kujiimarisha kidola na akapata uhalali wa kuua na kudhibiti wapinzani Kwa sababu kanisa la katoliki lilimtangaza kama chaguo la Mungu na mkombozi wa wanyonge.

Nchini Nigeria, viongozi wa kanisa la katoliki katika majimbo ya Kusini hasa kabila la Igbo waliunga mkono kuanzishwa Kwa taifa la Biafra,matokeo yake wakafanikiwa kuwashawishi wanajeshi wakristo kuasi na kumuaminisha Emeka Ojukwu kwamba anaweza kuwa mkuu wa taifa la Biafra. Matokeo yake zaidi ya watu 500,000 waliuawa na taifa la Biafra likawa kama ndoto ya mwendawazimu,ashukuriwe Mungu na Generali Yakub Gowon. Hapa nchini Tanzania kuanzia mwaka 1967_1970 viongozi wa kanisa la katoliki walimshawishi Mwalimu Nyerere kuandika barua na msimamo wa serikali ya Tanzania kulitambua taifa la Biafra.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga; Operesheni Condor ilianzishwa na Marekani miaka 1950 Kwa lengo la kupambana na mataifa ya kijamaa Amerika Kusini na visiwa vya Karibeani, Vatican ilitoa tamko la kupinga ujamaa hivyo Kwakuwa Latini Amerika Kuna Wakatoliki wengi ikabidi waraka utumwe makanisani ili wananchi wawakatae viongozi wa kijamaa Kwa kivuli cha kukuza demokrasia.Hivyo kupelekea mapinduzi ya kijeshi nchini Chile, Brazil na mataifa kadhaa ambayo yalikuwa chini ya ujamaa.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga, serikali yetu ni sikivu na itayafanyia kazi mapungufu yaliyopo kwenye mkataba Kwa sababu hata mazungumzo na viongozi wa Bandari na wizara ya ujenzi bado,yale mliyopendeza ikulu yatafanyiwa kazi kuliko kuzua taharuki na kuligawa taifa letu.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga naomba kuhitimisha barua hii Kwa kuchambua walau falsafa na itikadi ya Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kuhusu R nne ili kujenga maridhiano na demokrasia nchini.(Reconciliation maridhiano, Resilience ustahimilivu,Reforms mageuzi na Rebuilding of the New State na ujenzi wa taifa jipya.).

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ana nia njema na taifa letu na ameonyesha uongozi wa kimkakati katika kutoa huduma za kisiasa, kiuchumi na kijamii Kwa Watanzania wote bila kujali dini zao,mila,kabila na tofauti zingine katika taifa letu.

Uongozi wa kimkakati ni mchakato wa kufanya maamuzi muhimu kuhusu malengo na mikakati ya shirika,taifa au taasisi kwa kuzingatia mazingira ya ndani na nje ya shirika hilo. Uongozi huu unahusisha kuchambua changamoto na fursa zinazojitokeza, kuweka malengo ya muda mrefu, kufanya mipango ya utekelezaji na kuchukua hatua za kutekeleza malengo hayo.

Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga uusomapo ujumbe huu naomba uwe na uvumilivu na ustahimilivu kwani kuna mambo yatakuudhi na kukukera . Ahsante sana Ndugu Mheshimiwa Baba Askofu Dr Gervas Nyaisonga.

Tanzania inataka kulazimishwa kuwa mawazo ya kanisa katoliki ni mawazo sahihi ya kutakiwa kufuatwa na serikali na ya Watanzania wote, iwe kwa kutaka au kutokutaka.

SIGNED BY LUGETE MUSSA LUGETE.
THE GRAND MAESTER.
GURU OF PHILOSOPHY.
MASTER OF HISTORY.
Kayonka Kikenke Kamasa Mwamgongo Kigoma.
22/8/2023.
0755988284.
 
Andiko refu lakini hakuna sehemu hata moja uliyojibu au kugusia hoja za waraka wa TEC!

Jipangeni tena.
 
Back
Top Bottom