Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Tangu 1995 wimbo ni huu huu. Haipendwi, Haipendwi Ila wao ndo bado wanaongoza halafu 2020 dalili ni ndogo sana za kushindwa kuendelea kuongoza.
Unafikiri kungekua na tume huru na uchaguzi ungekuwa huru CCM wangeshinda miaka yote hii,CCM wanatumia wizi,ghilba,fitna na Nongwa kuweza kushinda
 
Tumepiga kura kwa wingi mno

Subiri jioni watu wajumlishe
Mkuu TBC walifanya kazi ya hamasa kwa makala nchi nzima siko zote, sijaona hata picha ya kituo cha uchaguzi leo.Sina hakika nao wamegoma bali wameepusha aibu.
 
Haahaahaa! nipo Arusha nyumbani mitaa yote ya kata ya sakina hakuna kabisa UCHAGUZI, yaani watu wa CCM wameenda kujichagua wanarudi hakuna kura zinazopigwa kabisa, yaani CCM wamefanya kampeni kitu walichoshinda Arusha ni kumchukua meya haaaaaa! kweli lazima mzee awe live TBC kukwepa aibu hii.
 
Unafikiri kungekua na tume huru na uchaguzi ungekuwa huru CCM wangeshinda miaka yote hii,CCM wanatumia wizi,ghilba,fitna na Nongwa kuweza kushinda
Sasa nani anataka kuongozwa na wa aina hii? Yaani imeshindikana kushawishi majeshi ya ulinzi na usalama watoe sapoti itawezekana kuendesha nchi? Mbona wananchi wanajaa kwenye mikutano na huwa mnasema hamuwaongi waje? Kama wananchi wanavyoshawishika kwenye mikutano bila hela, basi washawishini na majeshi na usalama wawalinde msiibiwe. Kama hamuwezi hilo tulieni muendelee kulalamika huku wengine wakiongoza hata kama mnaibiwa. Kazi kuimba Wizi wizi wizi tangu 95 hakufanyiki lolote.
 
Takwimu Zitakazo Tolewa Baada ya Huu uchaguziii Zitakuwa ni Za Uongooooooooo, Wananchi walio Jitokeza Kupiga Kura na waliofanikiwa Kupiga Kura Ni Wachache sanaaaaaa Kuliko Miaka Yote ya Uchaguziiiii, Either wamesusia Uchaguzi au Wameona Hainaaa hajaaa ya kupiga Kuraa! Ogopa Sanaaa Watu wanao kaa kimyaa kuja Kuwahamasisha hawa tenaaaa kujiandikishaaa Mtakeshaaa! Tena 2020 mtu asinifuate kuhusu kujiandikisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…