Mawakili wa Mbowe waache maswali yasiyo na msingi, ulizeni maswali ya maana mteja wenu aachiwe haraka

Kama kweli kesi ya Mbowe ni kutunga ,na walaaniwe wote waliohusika na wasipotubu eee Mwenyezi Mungu hatukupangii chakufanya utajua mwenyewe.
 
Ni swali technical sana kwa wanaojua sheria.unakuta swali moja kama Hilo linakuwa na majibu zaidi ya moja kutoka Kwa wakamataji waliokuwa pamoja.
inamsaidia nini angalia mahakama kuu wametupilia mbal;i na kesi ya mbowe
 
Kama maswali yao hayana msingi si ndipo pa kuwashindia hapo, woga wa nini?
 
Soma vitabu vya Permason&Francis Drake .Drake akiwa investigator na Mason akiwa wakili.sikumbuki mwandish ila Mason na Drake ndo main characters katika hizo novels. Kama umevisoma basi Kibatala na Mallya uhakika wamevisoma.Mungu bariki Tanzania.
 
Haya ndio yale mambo ya kukariri kitabu cha mapenzi kisha unaenda kutongoza kwa mtiririko wa hiyo hadithi uliyosoma, matokeo yake unafika mtiririko wa Kutongozana hauwi kama ulivyokariri.
 
Mbowe atatiwa hatiani sio kwa ushahidi, bali ni kwa maagizo ya rais na genge lake. Hapo hamna kesi bali ni utoto unaofanywa na wazee.
 
Unaleta ushabiki wa Simba na Yanga kwa mambo ya maana.
Amejibu maswali yako matatu kwa weledi na heshima kubwa! Polisi wako na mawakili wa serikali wangekupa majibu rahisi zaidi! Kimsingi mkuu, maswali yako ni meepesi sana, labda yana tosha kwenye ‘chekechea’ ya sheria, siyo mahakamani wala Hapa jukwaani!
 
Sina uhakika kama mleta uzi wewe ni mwanasheria. Kama wewe ni mwanasheria basi huko law school ulienda kucheza na kama wewe sio mwanasheria basi endelea kufuatilia hii kesi ili upate shule.
 
Ni ushahidi kwamba ni kesi ya kutunga, kama hawana msimamo wa pamoja wa walivyo kamata watuhumiwa!
Nadhani baadhi mmenisoma vibaya pamoja na kwamba nimeeleza mtazamo wangu kuhusu kesi hii ukoje. Angalia hata title ya uzi, nimetoa ushauri ili kesi iende haraka, Mbowe aachiwe huru mapema. Nikasema kwa uzito wa kesi, haiwezi kufutwa kwa sababu ndogo ndogo kama hizo za technicalities za ukamataji. Hii siyo kesi ya kuiba mayai.
 

Hii huruma kwa kuku, mwewe alianza lini kuwa nayo?
 
Na nyie hamjaelewa msingi ya maswali yangu. Ni mazito kuliko unavyodhani na majibu yake yana athari kubwa hata baada ya kesi baada ya mtuhumiwa kuachiwa huru.
 
Hii huruma kwa kuku, mwewe alianza lini kuwa nayo?
Tatizo wapinzani mnaamini wasiotakiwa kuaminiwa halafu wengine wenye nia thabiti ya kuwasaidia mnaona hawana maana. Angalia track record yangu kama nimewahi kuwa upande wa Serikali.
 
Natumaini haupo katika jopo la Mawakili wa Mbowe. Kama ni kesi ya kisiasa, inabidi mjue malengo ya kisiasa ya waliobambikiza kesi ni nini na nini lengo lao hasa la kesi, hilo ndiyo litawasaidia kujua mbinu sahihi za kutumia.

Mnampotezea muda mteja wenu kwa kukariri mbinu na taratibu za kushinda kesi bila kuangalia 'context'.
 
Mawakili hawajakosea. Hawaachi kitu. Lengo lao ni kuudhalilisha ushahidi. Ni tactic nzuri
 
Mawakili hawajakosea. Hawaachi kitu. Lengo lao ni kuudhalilisha ushahidi. Ni tactic nzuri
Lengo namba moja la Wakili wa upande wa utetezi linatakiwa kuwa kumtetea mteja wao ashinde kesi na aachiwe huru haraka iwezekanavyo. Siyo showoffs na kuonyesha umahiri wao wa vitu ambavyo sana sana vinachelewesha tu kesi ya msingi kuanza kusikilizwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…