Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Unafikiri huo uliisha. Tatizo ilikuwa nani atathubutu kuripoti?
Eti Ee!? Hata wapita njia na Kigogo pia hawakuripoti matukio yaraia wema wakiporwa pesa na kuuawa mchana kweupe kwa miaka 5+ ya JPM? Au ni "sukima gang" wanamhujumu mama?
 
Huyo mwehu anajifanya kumtaja Magu sahizi! Atulie aache mapepe si walidai mama atatuvusha! Kama disko ndio kwanza saa 4 usiku sahizi
Watu wasilalamike awamu hii ni kubembelezana. Polisi wabembelezeni hao majambazi. Msiwakaripie tumieni demokrasia. Awamu hii ni yamaelewano na mshikamano.
Tuko pamoja mama utatuvusha. Kesi ambazo hazina ushahidi achia wote hata kama ni majambazi yaliiba, yakaua, achia wote waende mtaani.
Harafu nanyi majambazi muwe mnabembeleza mnapo pora. Tumesema awamu hii ni kubembelezana.
Hongera Rais wetu kipenzi Samia Suluhu Hassan. Tunaimani na wewe. Tunakupenda. Tuvushe!
 
mkuu kwa kifupi sasa hivi hii nchi haitishi. kila mtu haiogopi, majambazi, matapeli, mabeberu, wafanyakazi wa umma. wote poa tu
time will tell
Enzi za JPM kuna mtumishi wa umma alikuwa anapita hapa kwangu saa 12 kamili Sharp na baiskeli yake ya Avon akienda kazini, siku hizi anapita saa mbili kwenda na saa saba mchana tunakutana machimboni, hahahaha! Natamani kurudi kwenye ajira mimi!
 
Sawa, suppose mtoa hela aliwaambia washikaji atakwenda kutoa bilioni moja benki, je aliwaambia ni benki gani? Huu mchongo ni wa wafanyakazi wa benki wenyewe, unaitwa inside job na usikute hata bunduki waliazima toka jeshini au polisi.
Miaka mitano iliyopita kiliwazuia nini hao uliowahita inside job? Kwann mara hii wamekuja kwa kasi?
 
Kima tunajua hayo, tuache tupigwe tu risasi
 
Sio.kweli matukio yalikiwepo hata wakati.wa.JPM tumepoteza ndugu zetu nyamaza kabisa.Hakuna mtu wala.chombo cha habari walikuwa wanatangaza .Ni kama Corona tu tuliaminishwa hakuna ila watu wanakufa tu
 
Wewe kufa ukaungane na Magufuli tu,his time is gone na hakuna namna isipokua ukubali tu Tanzania ina raisi mwingine.
 
Hilo tukio usikie tu
Siku moja Masaki kule,kijana mdogo tu wa kihindi aliuliwa mbele ya baba yake. Wote tunaangalia.
Walikua na Bureau de Change pale Sea Cliff Village.
Yule kijana alikua sio mchovu pia anapigana kick boxing na kila kitu,
pale alikua likizo tu maskini anamsindikiza babaake majambazi wakamuuwa mbele yake wakapora fuko la pesa wakaondoka nalo.
Ni kwamba dogo alitoka na gun awathibiti majambazi akatulizwa.
Yule baba yake alilia akapiga magoti kwenye damu ile kama anaswali, Akaondoka hakurudi tena pale Sea Cliff Village miaka hiyo.
Sasa balaa kuna kakaake na huyo dogo alieuwawa Mafia vilevile.
Alianza nao hao nyumba kwa nyumba, ni moto tu,sijui aliua wangapi ninamkumbuka JB aliuliwa Sinza pale kijiweni, ila hapo walikua washaondoka wengi tu.
Yule muhindi alilipiza kisasi mbaya kabisa,
Nilikua mteja wao na nnafanya kazi mitaa hiyo,
So alikua ananionyesha picha kabisa,
"Jana tumelala mbele na huyu, kesho huyu tunammaliza"
Waliuliwa majambazi wote wa5 jumla
 
Miaka Gani?
 
Ooooh amekuja Farao asiyemjua Yusufu. Kwa sauti ya mzee wa upako
 
Mods huyu kilaza threads zake zote ni za kumshambulia na kumdhalilisha Rais Samia jee mna ubia naye
 
Umesahau kutia tangawizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…