babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 14,478
- 18,341
Iko matakoni kwako huifeel?Umesahau kutia tangawizi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Iko matakoni kwako huifeel?Umesahau kutia tangawizi
Dawa yao ni kuwapa wale vyuma tu....Halafu katika zama hizi bado watu wanashindwa kutumia technology kufanya manunuzi? Haina haja ya kwenda bank kuchukua mzigo mkubwa ,wa nini? Kama unaenda kununua kiwanja,gari or malipo yeyote si unafanya bank transfer? Kama vimilioni viwili au vitatu si unatransfer tu kwenda kwenye mobile? Usiangalie gharama jali uhai.
Milioni 8 ama 10?
Jambo la pili, kuhamisha pesa kiasi chochote kutoka bank moja hadi nyingine ni elfu kumi tu.
Usitembee na pesa zote hizo unahatarisha maisha yako kwa gharama ndogo sana ya elfu 10 tu.
Sasa jamaa anachukua 8M bank moja anaenda nayo bank nyingine badala ahamishw kwa only 10k tu.
Unafikiri huo uliisha. Tatizo ilikuwa nani atathubutu kuripoti?
'Kiroba limefungwa kama furushi' !!!kuanza 2016,ujambazi wa silaha ulikoma kabisa.mpaka watu wakaanza kuona hakuna sababu ya askari kuzurula na silaha mtaani.
sababu ni moja,ulikuwa ukikamatwa na silaha haijasajiliwa bro,siku mbili mbele tutakuta likiroba limefungwa kama furushi.
SadPolisi Dar es salaam imetangaza msako mkali wa Majambazi waliosababisha kifo cha Kijana Jimson Kibiki baada ya kumpiga risasi wakiwa kwenye purukushani za kumpora pesa maeneo ya Mbezi Beach.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM Camilius Wambura amesema "tukio lilitokea jana saa saba na nusu mchana alikua ametoka Benki Mikocheni alikochukua kama milioni 8 akaelekea kwenye Benki nyingine Afrikana nafikiri kulikua na matatizo ya kibenki pale kwahiyo akatoka kuelekea nyumbani maeneo ya Juliana"
"Alikua ana milioni nne kwenye mifuko yake ya suruali na milioni nne nyingine kwenye bahasha ndipo alipokutana na hilo tatizo, Watu hao wadhaniwao kuwa Majambazi walimpiga risasi tumboni, akapelekwa Hospitali Mbezi beach kwa huduma ya kwanza baadae Muhimbili ndiko alikofariki"
"Wale ni Watu ambao wameua, lile ni tukio la mauaji.. taarifa ya Polisi ni kwamba tuko mbioni kuwatafuta na kuhakikisha tumewapata na kuchukua hatua za kisheria dhidi yao, kwenye tukio hilo walichukua milioni 4 na kuondoka nazo"
Lazima alaumiwe mana hachukui hatua stahiki amfukuze IGP kama mfano ... mbona Magu aliweza na palituliaKwa nini Mama alaumiwe?
Je, ni kweli kwamba Mama ameagiza Polisi waache kushughulika na UHALIFU na WAHALIFU?
Au, Kamanda Siro na timu yake wameamua kuachia UHALIFU NA WAHALIFU ili Mama Mh. Samia Suluhu Hasan "ALAUMIWE"
LAWAMA ZIELEKEZWE KWA KAMANDA SIRO NA TIMU YAKE.
WA KUWAJIBIKA NA AU KUWAJIBISHWA NI KAMANDA SIRO NA TIMU YAKE.
tukifikiri hivyo tunaondoa tatizo kwa kujifunika shuka usoni tusilione.'Kiroba limefungwa kama furushi' !!!
Ilikuwa moja ya staili za wasiojulikana ambao pia walitumika kuwasulubu wapinzani, wakiwa orchestrated na utawala.
Kwa nini tusifikiri kuwa haya ya ujambazi unaotokea sasa yanakuwa oragnised na watu wale wale ambao kwa sasa wako kwenye inner cycle ya mama , wakiwa na lengo la kumhujumu?
Hapana, Ukweli ni kwamba viongozi wa Jeshi la Polisi wengi wanamdharau mama, Mama anaenda kuwaomba ushauri hao Mapolisi wakati JPM yeye alikuwa mtoa Order kuwa sitaki jambo flani kama ujambazi, uuaji n.k na linafanyiwa kaziKidogo inaanza kutia wasiwasi.
Ni kama mama hakuwemo kwenye serikali iliyokuwa imeyadhibiti haya mambo, na sasa ni kama anatafuta njia zake mpya kabisa kwa kila kitu, jambo ambalo inaonekana inamchukua muda mrefu na kutoa mwanya kwa watu kujifanyia yao.
Hivi polisi nao wamebadili utendaji kazi wao uliokuwa umedhibiti uhalifu wa aina
Samia atalinganishwa na mtangulizi wake katika baadhi ya mambo, na ataonekana hatoshi kabisa!
Umejuaje kuwa alipangiwa kufa hivyo??Killed for his own money. Ila Alipangiwa atakufa hivyo.
JWTZ ni malaika?.Polisi ndio majambazi wenyewe. Huyu mama acha acheke na nyani atavuna mabua soon. Inatakiwa hii nchi sasa hivi miji mikuu yote ilindwe na JWTZ. Udokozi ujambazi na ujinga ujinga unarudi kwa speed ya mabomu ya Israel.
Magufuli nilikuwa simkubali kwa mambo mengi sana ila yule dume halikuwa hataki ujinga wa kisengesenge kama huu. Jiwe alikuwa kiboko wasomi na elimu aliwageuza chekechea jiulize kuna mtu na elimu ya mwisho kbs alikunywa dawa ya Madagascar bila kupenda halafu leo anagomea chanjo ya covid 19.
Magu mungu akuweke unapostahili, ila ulijua kuchezea na ndeze wabongo.
Naona mmezinduka usingizini sasa, wenye akili tuliwatahadharishaMama akija kushituka, itakuwa teyari too late wacha aendelee kuwakumbatia.
Kwa hali ya sasa mtaani inawezekana kabisaMajambazi wanawezavizia 2m?
UKWELI MTUPUmkuu, JPM kauli zake tu majukwaani zilikuwa zinatisha. samia anapoongea na wananchi zile kauli hana. mfano kuhusu hili la ujambazi JPM aliongea live kuwaambia askari kwanini jambazi anapora na silaha alafu anafanikiwa kukimbia, kwanini msiwanyang'anye hizo silaha ' haraka haraka' tena neno haraka haraka akalirudia kama mara 3 hivi. alimaamisha jambaz lazima afe. sasa kama ww ni jambazi ukisikia hii kauli rais anaiongea live lazima uogope. kama tunahitaji kusikia maneno matamu kila siku haya ndio madhara. kauli za JPM ndio zilikuwa zinatulinda
Haya mambo ya kuishi kwa kuvizia vizia na bila amani hayafai kabisa kuchukuliwa kirahisi, Polisi wahakikishe wahalaifu hawa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Poleni sana wafiwa nq Vodacom maana nimesikia redioni wanasema jamaa alikuwa ni Meneja wa Mauzo na Masoko wa Vodacom Tanzania.Afande sina cha kueleza, taarifa zinajitosheeza hapa chini!
View attachment 1792209
Tukio la kusikitisha limetokea leo mchana maeneo ya Juliana Mbezi beach ambapo Jimson Kibiki amefariki baada ya kupigwa risasi.
Kutokana na vyanzo vya mashuhuda Jimson alivamiwa alipokuwa ametoka bank na kuporwa na majambazi kiasi cha fedha ambacho mpaka sasa hakijajulikana.
Baada ya kupigwa risasi alipatiwa huduma ya kwanza na kusaidiwa kufika kituo cha afya lakini baada ya kufika hospital akapoteza maisha.
Jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi na tutaendelea kukujuza kila kinachoendelea.
Kumbe unaleta ushabiki wa vyama.Bali yupo Samia .Rais wetu good gooo mama .Enzi za mwendazake zimepita lazima maisha yaendelee.Siku nyingine CCM mpate akili ya kuweka makamu wa rais.Mlijua ni ceremonial position.Sasa kawa rais bila kura.Wamama oyeeeeeeeeeeeeeeeeee.Safari hii wanaume mtaenda labor msipotafuta hela.Kazi kulilia mwanaume mwenzenu.Kaza msuli
Waanze na teller aliyemuhudumia wakifatilia call watapata jibuKuna banker kauza ramani.
Waanze na teller aliyemuhudumia wakifatilia call watapata jibuKuna banker kauza ramani.