Yeah, playok hakuna kibonde, kule usimchukulie poa yeyote, unaweza fungwa na mchezaji uliyemzidi point kibao. Ukitaka ujue drafti fululiza kucheza playok, au waangalie wengine wanavyocheza.
Wanaoweka dakika 1, 2 au 3 wanapima uwezo wao kuzizoea copy walizozizifanyia mazoezi na kufikiri kwa haraka. Wengine wanaocheza kwa dakika 1 ni kweli wezi/wajanja wajanja, shida yao ni ushindi tu hata game ni sare, wanafosi kucheza ili uwahi kumaliza muda ashinde. Game za muda mfupi kama dakika 1-3 inatakiwa network yako iwe faster na strong 4G, siyo network za kuungaunga au slow.
Kabla ya kuanza kucheza na mchezaji anayesubiri kucheza na mtu, angalia kwanza table yake ni ya dakika ngapi?, kama ni ya dakika 1 achana naye kama hutaki kwa dakika moja.
Kule kuna watu wanaolala, yaani kete ya mwanzo tu anafikiria weeee!!, wanaboa sana.