Mboga nisizopenda katika maisha yangu

Mboga nisizopenda katika maisha yangu

😂😂😂😂😂 Unajua hizo NYANYA CHUNGU sio kama inapikwa kwa kuwa uliacha pesa ndogo... Laaah ila unakuta kuna wadada wanapenda tuu sasa mi huwa na pdf yangu kabisa mlangoni...

Katika kanuni zangu sitaki hizo NYANYA CHUNGU akipika ni kesi kubwa mno
Hata zikichanganywa na nyama au samaki na hivyo huwezi kula?
 
Hizi mboga sizielewi sijui kwa nini watu wanazipenda
Sababu hujapata mtaalam, mpishi sahihi, wa kukupikia.
2.Mlenda.
Pata mpishi toka Tabora, Mrenda wa karanga, Acha kabisa
Tazama hapa pishi la Mlenda
Code:
https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=amEKNoxCT6Y
1730385851134.png

Picha: Mlenda mkavu (Mzubo, Nswalu, Mkunungu, Ndalu, Ighonda, Msele, Lilende, Mshigino) wa karanga.
Pata mapishi ya Pwani, Kwa tui la nazi. Utauliza mara mbili hivi mboga ipo au imesha?
 
Mabiringanya sijui yalitokeaga wapi .Yaani kama una unatafuna maboksi au godoro.Ukitaka kunilaza njaa pika mandizi hata uyarembe vipi hayana ladha kabisaa.Mwisho Tambi au maminyoo.
😂Biringanya ❌ bomoa
😂Ndizi napenda mzuzu tu zingine ❌
😂Cabbage ❌
😂Dagaa inategemea na upishi, mpishi akiwa na CPA nakula zote kasoro kigoma zile kama vijiti vya ngubiti hapana.
😂Mboga za majani kwangu ni tembele, majani maboga, spinach OG, mnavu.✅
😂Nyanya chungu ❌
😂Maharage ila usiunge na chochote zaidi ya kitunguu maji✅
😂Macaroni au noodles ❌
😂Dengu❌
😂Kuna maharage flani ya gololi yakipikwa yanakuwa kama mahindi ya kande nimesahau jina lake.❌
😂Mlenda❌ naona kama nakula denda la ng'ombe
 
Wakati nalelewa nilikua sili kabeji,nyanya chungu,dagaa na vingine yani nilikua nachagua vyakula ila sasa hivi nakula mpaka mahindi ya kukaanga kwa hyo usijali life ndio linakuchagulia ulaje
Hata mimi nilikuwa hivyo nilikuwa sili biringanya,mchicha,dagaa na kachumbari ila nilipopitia magumu nikaamua kwenda mgodini motipwez nilijikuta navipenda mno hivyo vyakula
 
Wapeni watoto wenu wa kiume tu kisha mje kushangaa jinsi wanavyohaha kutungisha mimba😂...

Sahizi kupata watoto wa kiume tu ishakuwa ishu yani. Unashangaa wewe na wadogo zako wote kila uzazi anazaliwa demu tu. Ipo siku watu wataongea kuhusu hili nahisi ipo shida mahala.
Hao watoto wakiume wenyewe siku iz tunaogopa kuwazaa maana wanabadilika kama vinyonga
 
😂😂😂😂😂 Unajua hizo NYANYA CHUNGU sio kama inapikwa kwa kuwa uliacha pesa ndogo... Laaah ila unakuta kuna wadada wanapenda tuu sasa mi huwa na pdf yangu kabisa mlangoni...

Katika kanuni zangu sitaki hizo NYANYA CHUNGU akipika ni kesi kubwa mno
Ajipikie mwenyewe tu au na hio pia kesi?
We ule wali wako na chukuchuku 😅
 
We utakuwa unaongelea yale mabilinganya (mabilingani) yale makubwaaa hayana ladha. Zanzibar kuna mabiilingani madogo madogo yana kokwa nyingi. Hayo pishi lolote yanakubali. Lkn zaidi ya kukaanga tena yapikwe na maganda yake. Mmhh, yummy 😋😋😋
Mabiringanya sijui yalitokeaga wapi .Yaani kama una unatafuna maboksi au godoro.Ukitaka kunilaza njaa pika mandizi hata uyarembe vipi hayana ladha kabisaa.Mwisho Tambi au maminyoo.
 
Back
Top Bottom