Pre GE2025 Mbowe yupo kimya anatafuta kura, Lissu yupo bize mitandaoni kukilaumu chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii siku zote ilikuwa hoja.

Ila, ilikuwa hoja ambayo ilikuwa haijapata endorsement ya mwanachama wa CHADEMA kugombea Uenyekiti,
Mwaka 2019 Cecil Mwambe aligombea uenyekiti hakuwa mwanachama au hadi agombee kiongozi.
 
Mwaka 2019 Cecil Mwambe aligombea uenyekiti hakuwa mwanachama au hadi agombee kiongozi.
Point yako nini hapa?

Mimi nasimamia kanuni kwamba uongozi wa CHADEMA upangwe na wanachama wa CHADEMA, usipangwe na wanaharakati wasio hata wanachama wa CHADEMA.

Nilikuwa naona tatizo wakati wanaharakati wasio wanachama wanasema "Mbowe Must Go" wakati hakuna hata mwanachama mmoja aliyechukua fomu kumuondoa Mbowe.

Sasa wamejitokeza wanachama watatu zaidi ya Mbowe. Tundu Lissu (ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti) Odero Charles Odero na Mapunda. Wote wanagombea uenyekiti.

Hoja ya "wanaotaka kumuondoa Mbowe ni wanaharakati tu" imekufa. Tumeona kuna wanachama watatu wanataka kumuondoa Mbowe. Wapo. Mpaka watatu wamechukua fomu.

Usichoelewa ni kipi hapo?

Sasa kama mwaka 2019 Cecil Mwambe aligombea uenyekiti kama mwanachama wa CHADEMA hapo tatizo liko wapi?

That is a logical non sequitur fallacy.

What is the point you are trying to make here, if you even know it yourself.

Huna point au unashindwa kuieleza vizuri tu?
 
Mkt wa kudumu ana sera ipi mpya ya kuuza Kwa wapiga kura?
 
Nadhani kelele za Lissu zina faida kuliko kimya cha mwamba
 
Nadhani kelele za Lissu zina faida kuliko kimya cha mwamba
Lissu anafanya kampeni inayosaidia Watanzania kuelewa matatizo mengi yaliyo katika siasa za Tanzania.

Anafanya kitu kikubwa kuliko kampeni ya Uenyekiti wa CHADEMA.

Kwangu mimi Lissu hata akishindwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, atakuwa ameshinda kitu kikubwa zaidi ya uenyekiti wa CHADEMA, kuwaelimisha Watanzania kuhusu matatizo ya demokrasia nchini mwao kuanzia chama tawala mpaka vyama vya upinzani.

Tatizo watu wengi wako stuck kwenye kampeni ya uenyekiti wa CHADEMA, hawaoni kampeni kubwa zaidi ya hiyo ya uwazi, demokrasia, kupinga rushwa popote Tanzania.
 

Ingekua ni Lissu isingekuwa tatizo, lakini ACT hawawezi kulikubali kundi la kina Maria Sarungi kabisa
 
Lisu anashinda kwenye media tu na kuropoka na kulalamika
 
Swaga za kiccm hizi, halafu ikifika siku ya kura tunaona kura fake, vitisho, rushwa nk.
 
Aelezwe Maria Sarungi sio mpiga kura.
Safari hii Mbowe atajua watu wamemchoka, hata akishinda kwenye hizo kura kwa kuhonga, bado hatakuwa na uwezo wa kupandisha hamasa ya wafuasinwa cdm. Ukweli ni kuwa wakati ukuta.
 
Kama ni hivyo kwa nini wanaharakati wanalia mitandaoni kuwa Mbowe aachie kwa busara na si kwa box la kura?
TAL aachane na wanaharakati bali awashawishi wajumbe wampigie kura.
Shida ya chama chao kila mmoja mjuaji na kujifanya kuwa yeye ndio chama. Hii ya kujifanya kuwa mtu ndio chama imeshapitwa na wakati, na kama chama chao kitakuwa kimejijenga kwa sababu ya mtu basi CCM itatawala hadi mwisho wa dunia.
Taasisi inatakiwa kuwa na nguvu kuliko mtu. Watu wanakuja na kuondoka ila taasisi itabakia milele.
Kama chadema inasimama kwa sababu ya TAL basi kuna tatizo. Au unafikiri CCM/Serikali inaogopa maneno ya mtu? Ili taasisi isimame lazime ijijengee ideology ambayo ndio itakuwa inaendesha taasisi na sio mtu. We need strong institution and not a strong person.
Ndio maana Malema wa Afrika Kusini amebakia kupiga domo tu wakati wenzie wanachukua majimbo na kujenga taasisi zao. Zuma kasajili chama kipya na kilipata uwakilishi mkubwa kuliko Malema wa siku nyingi na chama chao.
 
Tumeona kuna wanachama watatu wanataka kumuondoa Mbowe. Wapo. Mpaka watatu wamechukua fomu.
Kwa hiyo hoja ni kumuondoa na si kushindana kidemokrasia! Kama wamejitokeza wanaohitaji hiyo nafasi mimi naona ni jambo la heri kwa chama chao ili tuone demokrasia kweli ipo au limebaki jina tu.
 
Wanaharakati huwa wanajiona wao wako sahihi muda wote, kwao demoktasia ni Mbowe aondoke hawana option nyingine.
Hiki chama chao wakikubali kuendeshwa na wanaharakati ndio utakuwa mwisho wa anguko lao.
Wanaharakati wanapata vipesa vya wafadhili ndio maana wanakuwa na mdomo mrefu sana. Mimi natamani Mbowe ashinde tuone hiyo hoja yao kuwa chama kitakufa kama CUF.
Ubaya wa kujenga taasisi kwa kutegemea mtu tunauona kwa CUF na Maalim Seif. Meisho wa siku kimazaliwa chama kipya (ACT + CUF) ambacho hakieleweki kinafanya nini maana kinategemea kauli ya kipngozi na sio maamuzi ya kamati kuu ya chama ambayo ndiyo inayoendesha chama.
Wacha CCM iendelee kutamba kwa ujinga huu wa kupangiwa na wanaharakati.
Ukiangalia siasa za Kenya, wanaharakati ni wanaharakati na chama cha siasa ni chama cha siasa. Kila upande unapita njia yake wakutane mbele huko.
 
Na huwa unasali mbele ya Muumba wako!!!
 
Yaani Mbowe sasa kawa rafiki wa maccm. Hata maneno ya maccm ya kusema vyama vya upizani vinashindwa kwasababu havikujipanga. Naye anasema Lissu hakujipanga huku akiwa anagawa hela kwa wajumbe. Ccm wanamtumia mbowe kuuwa chadema wakifikiri chadema ndio adui yao . Ila ccm wasicho juwa chadema imewasaidia kuendelea kuwa madarakani kama chadema asinge kuwepo ccm ingekuwa imeisha ondolewa . Hivi sasa ngoja chadema ichukuliwa na Mbowe imfia mikononi mwake. Halafu uone moto wake . Kama hakuna upizani unao aminika basi atatokea mtu anaye aminika na ataongoza wote walikata tamaa na utawala mbovu wa ccm na wataiangusha serikali.
 
Ukihitajika kutoa ushahidi unao?au stori za kusimuliwa kijiweni na wewe unaziandika andika humu bila kua na uhakika.

Utaingizwa mkenge na wanaharakati wakuache badae usimame peke yako ujute
 
Kila mmoja wao anazo sera zake….weka mezani tuchambue….acha longolongo miiiingiiiiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…