Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Kwanza alivunjiwa nyumba,, ikabidi ajenge ingine
Pili hela ikatumika kwenye kampeni na ubunge hakupata,
Tatu ameugua kila wiki cost milioni 4,,
Lazima atepete tu
Ruge alipigwa 6M kila siku clouds media na kiburi chao chote ilifikia mahali walinyoosha mikono juu wakaomba wa TAG ubavu kwa wananchi!
 
Mie sitoi hata mia
 
Acha uchawi, na we ukiumwa sema watu wakuchangie, wasipokuchangia basi wakikuchangia ni vema.
kuchangia ni hiari tuu alafu pia ni ile tuu kuonyesha ile love kwamba mko pamoja naye katika kipindi hiki cha matatizo nadhan hamna alolazimishwa hata familia yake haikutaka achangiwe
Kama watu wanavyokuleteaga matunda ukiumwa its the same to this
 
Kutoboa bongo ni ngumu sana kwa sababu bado tunaishi kijamaa. Huwezi kuwa unacho ndugu wasilete shida zao na lazma uwatatulie kiungwana tu.

Watu wanahisi ukiwa Mbunge ndio tajiri hawajui deepdown mambo yakoje! Jamaa pia hakukaa vizuri kwenye ubunge kama ambavyo wengine wamepiga term zaidi ya 3 mtu ana hela ndefu kweli kweli! Kama kujiwekeza kawekeza sana tayari.

Naimani angepata nafasi ya kuhudumu walau term 2 angekuwa pazuri zaidi
 
Watu wanajisahau sana, kuna magonjwa hata uwe na hela kama Diamond Platinumz lazma utembeze bakuli tu! Utapambana wee ila hela inayotoka ni kubwa kuliko inayoingia yani!

Imagine upigwe invoice ya 6M kila siku kwa week tu uweze kulipa 42M hata kama una billion 1 bank utaweza kukimbizana na hizo charges kwa muda gani?

Kila mwezi ulipe 168M utakaa muda gani ukikaza sana miezi mitatu tu lazma uombe poo!😂

Maana ikunbukwe ukiwa hospitali kuna wengine nao wanategemea mfuko wako huo huo waishi magari yaendeshwe uje kutazamwa hospitali.
 
Bima ya afya imekaa kitapeli sana hasa hii ya NHIF!

Magonjwa yote critical na yanayohitaji care kama za Dialysis wameyaondoa sababu yana gharama kubwa ila wameacha malaria ambayo kila mtu ana mudu!

Kawaida ya bima inatakiwa kundi la watoto na vijana libebe watu wazima wenye matatizo Mengi ila hali ni tofauti! Watoto wana options nyingi kuliko watu wazima ambao ndio wako Prone to sickness!
 
Kiongozi sawasawa kabisa NHIF ipo kiwiziwizi mie mwenyewe muhanga nilichangia miaka mitano baada ya kutumbuliwa na KAYAFA bima ikakoma wana utaratibu mbovu sana eti mpaka uchangie miezi 120 yani miaka 10 mfurulizo ndio unakidhi kigezo cha kutibiwa maisha yote.

Ndugu yetu prof' J baada ya ubunge kukoma na bima ikakoma labda km angetumikia vipindi viwili vya ubunge angekidhi kigezo na masharti ya bima kutibiwa maisha yote. Kutoa ni moyo sio utajiri tumchangie prof' J amefanya kazi kubwa sana ya kutuburudisha na kukuza muziki wa kizazi kipya.
 
Kuna mwanasiasa na mwanasiasa! Binafsi ningezisikia ni yule mbunge chotara wa kuitwa Azan Zungu ningefungua nyuzi hata 50 kuhamasisha apambane na hali yake sababu ni mtu wa hovyo asiejali utu!

Ila kwa Prof. Jay huo utakuwa ni ukosefu wa utu maana jamaa hana baya kabisa! Hajawahi kuropoka utumbo na ni mtu asie na noma na wananchi!
 
Huyo Dogo mxenge kweli aisee figo iacheni ikiamua kuleta kirambasi ujue kama huna hela watu wapange taratibu za mazishi tu
 
Mzigo unafika 4M kwa week mzee! Unahitaji kuwa na serious investment kukabiliana na hilo Gap!

Angekuwa kwenye Ubunge isingekuwa shida sana. Maana wabunge wenzie wangemchangia sana na hata Serikali ingegharamia matibabu yake.
 
Mleta mada unazifahamu gharama za dialysis kweli?Tumuombee tu mwenzetu...Na acha watu wenye Moyo wa kutoa wamchangie....achana na hii kampeni
 
Ngoja siku figo ifeli ndy akili ikukae sawa

Unamkumbuka Ruge mtahaba? Bakuli zilivyo pitishwa?
Ruge alikuwa anapigwa 6M daily jamaa wakawa wamepiga kimya ilipofika mzigo umegonga 650M ilibidi wafunguke tu kuwa mziki mnene jamani tunaomba mlioguswa tusaidiane😂!

Hao ni Clouds Media Group pamoja na viburi vyao vyote.
 
Dah kumbe hata haya ma broilers na maziwa and all that yana chemical za ajabu?
 
Acha kabisa hio moment ya kusomewa mkeka wanaitwa wazee kwenda kuchukua taarifa za deni! Lazma warudi mwengine mkono kiunoni mwengine anaongea na simu 😂huku akipuputa jasho!


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…