Mkuu dunia hailingani.
Usipotumia AKILI dunia hi, utajikuta unatumika mpaka mwisho wa Maisha yako.
Hivi hujawahi kusikia msemo kuwa, wewe ukiwa huna gari unaombewa upate ila Kiongozi wako wa kidini akitaka gari ANACHANGIWA😀
Imagine,
Mwanasiasa anahitaji Support yako:
Utatunga nyimbo utamwimbia sana, na kumsindikiza akachukue fomu ya kugombea.
Utaondoka nyumbani kwako, utaenda kwenye mikutano yake ya kampeni kumpa support.
Siku ya KURA utasimama JUANI siku nzima kumpigia kura.
Ukishampigia kura inabidi usubirie kituoni kulinda kura ili asiibiwe.
Akiibiwa inabidi uandamane upigwe mpaka atangazwe kuwa yet ndio mshindi.
Pamoja na kulipwa mabilioni, akiugua Ni lazima achangiwe.
Watanzania Ni WAKARIMU sana, na Kuna watu weshajua hili na wananufauka nalo kill siku.
Hasa Wanasiasa na Wasanii.