Labda anawaambia magaidi, maana huko jimboni kwake kuna shida huko.
Wakati magaidi wametamalaki kwenye Jimbo lake alikua wapi asiwashughulikie . ?
Kenya huwezi kuwatisha Watu Kwenye siasa.
Siasa zijibiwe kisiasa na Sio kuuana . Kuua Watu Kwa sababu ya siasa ni ugaidi .
Asiltuletee hulka za magaidi.
Hii ni Nchi huru na ya Kidemokrasia Kama Hana moyo Wa kuvumilia kukosolewa basi aachane na siasa.
Ni Wazi KUWA Afrika watawala ni Wezi na wabadhirifu Wa Mali za UMMA. Wanajificha Nyuma ya vyombo Vya Dola.
Nchi zinapopinduliwa Watawala ndio wanakua Wakwanza kukimbilia ugenini Kwa sababu hawana Uzalendo na Nchi zao. Kazi za watawala wengi Afrika ni kujiona miungu Watu na kuweka Sheria za kutoshtakiwa .
Tatizo tuna Upinzani uliojaa Wala rushwa na vibaraka Wa CCM. Lakini Kwa Hali ilivyo wapinzani mpaka Sasa walitakiwa wawe wameshaajipanga Barabarani kumpinga huyo waziri Mpaka atolewe madarakani vinginevyo ni maandamano yasiyo na kikomo. Kauli Kama hizi wakati Wa Magufuli zilianza kutolewa kidogo kidogo Huku wapinzani wakiwa wanakenua meno na kulaani Kwenye mitandao Kwa maandishi. Matokeo yake waovu wakajipenyeza na kuanza kuua Watu na Kupiga Watu risasi.
Huu ni ujuha . Wanaolengwa ni Chadema lakini wamekaa kimya . Chama chenye vijana wengi kuliko Vyama vyote kinakua ni chama kondoo . Kwenye siasa za kutafuta madaraka woga ni Nguvu kubwa ya waovu ndani ya mifumo ya wezi . Wezi walijipanga muda Mrefu Tangu azimio la Arusha mbinu za mabeberu kuchukua Tena hii Nchi zilipangwa Kwa muda Mrefu na Sasa wamefanikiwa . Walianza na Azimio la Zanzibar . Wachache wakamiliki uchumi Wa Nchi wakishirikiana na mabeberu kutoka nje . Wakafanikiwa . Wakafanikiwa kushika Chama ,wakafanikiwa kushika Dola . Sasa wanataka kurejesha himaya ya kibeberu Tanganyika Kwa Kasi ya ajabu. Wanajua Watu wengi wanapenda Fedha hivyo rushwa ni mtaji wao Mkubwa . Wataingia mpaka Kwenye vyombo Vya Dola . Watapenyeza fedha ,wataingiza ,Sílaha ,wataanzisha mafunzo ya kigaidi Kwa Kasi ya ajabu . Nchi itajikuta Haina Nguvu Tena . Dola itakua Haina uelekeo wataiba Mali za umma Huku wakiemeza propaganda za kidini na kikanda.
Chama legelege huzaa Serikali lege lege.
CCM Imekua legelege .
Nchi Haina mbeba maono.
Wapinzani wamegawanywa Kwa sababu Wanapoona udhaifu Wa CCM wanadhani kuchukua madaraka ni rahisi matokeo yake Kila mmoja anawaza Urais Badala na kupingana wenyewe Kwa wenyewe.
Wanasingizia Katiba . Hakuna Nchi iliyoshunda mapambano ya Kupinga uhuni Wa watawala Kwa kusaidiwa na Katiba . Wahuni wanaondolewa Kwa mikakati na wanakuja kuadhibiwa Kwa katiba yao na kuonddoshwa kabisa Kwenye ulimwengu Wa siasa. Siasa inahitaji Imani za kimungu au miungu. Siasa inahitaji mpaka uchawi na kuwasomea Albadiri waovu Mpaka wawe kama vichaa waanze kuvhanganyikiwa na KUWA kama vichaa. Siasa inahitaji mipango na fedha . Siasa inahitaji kujitoa Kwa hali na mali.
MTU anapokwenda kuwapigania wamasai ni Lazima aomyeshe moyo Wa uaminifu, ukweli , Huruma , Imani kubwa na ujasiri. Wamasai waweze kuuza Hata n'gombe na kutoa michango Kwa Wingi Ili kujenga Nguvu ya kiuchumi. Wanasiasa maskini WASIOJUA kesho yao ni rahisi sana kununuliwa kama aalivyonunuliwa Zito Kabwe .
Kabwe alikua mpinzani Mzuri sana Lakini akawa na tamaa ya KUWA Tajiri kama Mbowe bila kuangalia historia ya Mbowe. Matokeo yake Zito akawa mfanya biashara Wa kisiasa na mamluki Wa Watawala nafisadi. Kweli ndoto ya tamaa yake imetimia .
Wapinzani Wa kweli ni Lazima wapinge kauli hizi za walevi Wa fedha na madaraka ya umma wanaotoa maneno ya kuwatisha Watu na kutishia uhai Wa Watu Kwa sababu hii Nchi SIO Mali Yao . Kama Wanapigania Maslahi ya umma wangelunda rasilimali zetu na kuwawajiibisha Wezi kule Bandarini ,TRA na Benki kuu na Huko Halmashauri. Mchnengelwa amepewa wizara iliyojaa ufisadi Kwenye Halmashauri Badala ya kupambana wezi anataka kuondosha uhai Wa wanaowakosoa wahuni.
Wahuni Sio Watu wazuri.Tuwakatae wahuni. Wahuni walimtisha Ndugai,wahuni walimtisha Bashiru Ali Wahuni walimtisha Dr. Slaa. Wahuni walimtisha Komredi na mzalendo Polepole.
Ni Lazima tuangalie hii Vita Kati ya wema na ubaya Kama inapigania maslahi ya umma au maslahi ya mabeberu na mawakala wao.
Je,wanaounga mkono wanaunga mkono Kwa sababu ya Nia njema Kwa Taifa au Kwa maslahi Yao Huku wakineemeka Kwa ufisadi Wa Mali za umma. ?
Bila shaka Waovu watashindwa Kwa Nguvu za Mwenyezi Mungu Muumba Wa vyote mana wanacheza na Mali za umma Kwa mgongo Wa chama kilichoasisiwa Kwa ajili ya Kupinga Unyonyaji na Sasa wamekigeuza KUWA Chama Cha mabeberu.
Ni Lazima mabwanyenye ama waondoke ndani ya CCM au waondoshwe na CCM waliyoiteka .
Freedom is coming 2024 - 2025.