Mchungaji Msigwa hana sababu ya kusema lolote ambalo litaonekana kuwa baya kwa mtu yeyote.
Kwa hiyo wenye hofu waondoe hilo, na wenye tegemeo la kusikia shutuma msitegemee kuwa ndivyo itakavyokuwa.
Inatosha kutoa shukrani za dhati kwa ujumla kuwashukuru waTanzania, kwa niaba yake na wenzake kwa misaada mbalimbali, ikiwemo ya hali na mali.
Haitaongeza chochote kwake kushutumu au kuzungumzia mambo binafsi yeye na familia yake.
Hana sababu kabisa ya kuongeza chochote kitakachoonyesha utofauti wa vitendo vyake alivyoonyesha baada ya kutoka kifungoni na wengi waliomtangulia ndani ya chama chake waliotimkia upande wa pili.
Kila mwenye nia ya kutaka kujua amekwishatambua ubovu wa uongozi uliopo sasa unaofanya mambo ya aibu bila hifadhi ya staha mbele za watu.
Mchungaji Msigwa kaonyesha njia, kwamba kuna mambo mhimu zaidi katika maisha ya binaadam kuliko hadaa za kijinga ambazo wengine wanadiriki kuziita siasa.
Bila shaka wengi waliobaki huko CHADEMA sasa wataimarika zaidi kwa kujua kwamba sio kila aliyeko ndani ya chama hicho ananunulika kama bidhaa.
Haya yanayofanywa na CCM sasa sio siasa ni uharamia.