Mdude Nyagali, shikilia hapo hapo na usipoe

Vipi akishtakiwa kwa kosa la kumkashifu raisi aliyeko madrakani, lakini pia kumtishia maisha akaona haitoshi kumdhalilisha aliyekuwa raisi wa awamu ya tano (Ambae sasa ni marehemu) huoni nimakosa matatu yaliyoshiba yanayomtosha kurudi alikotoka kupigwa mvua za kutosha.

Nafikiri hawa ndio wapinzania wachache wanaofanya upinzania uonekane ni watu wa hovyo, wanashindwa kuelewa misingi ya harakati ni kuwa na hoja madhubuti kwa lengo la kuikosoa serikali pasipo kuvuruga amani ya nchi, wala kuleta udharirishaji na migogoro isiyo na lazima.

Chadema wawe makini na hawa watu watapoteza dira na malengo waliyojiwekea kuelekea kuiongoza nchi.
 
Walilima lami kwa meno. Yeye sasa hivi anaoza. Hii dunia bwana. Kibao kinageuka muda wowote
 
wapuuzi nyie mlimponza jiwe hivi hivi mpaka akadanja.
 
Mdude ni mfano halisi wa wana chadema walivyo!

Angalau Mbowe anaweza kuwa na siasa za kistaarabu! Lakini mtu kama Lisu akili yake ni kama hiyo ya Mdude!
Jiwe the killer ni mfano halisi wa wanaccm. Unaongelea maneno tu? watu wamezika watu wao.
 
Naona unamtia ndimu na alivyo mwehu ataona yeye ni hero, atafurahi tu. Jela ataenda pekee wakati wenzie wanakula makvant kwenye mikutano ya matusi.
 
Wasakwe wote waliofanya UNYAMA huu chini ua Mwendakuzimu...
 

Wembe ni ule ule
 
Mdude angekua CCM haya maneno angeyatumia dhidi ya viongozi wa Chadema ingekua ni vyema na haki.
 
Reactions: Qwy
Mjazeni ujinga akirudi korokoroni itayoteseka ni familia yake na yeye mwenyewe nyie mtaishia kumuweka hashtag tu on social media.
 
Poor MATAGA, bado tu mnamuota Mwendazake? He is gone for good.
 
Kwa kauli yako hii simply umeshakubali kuwa mtumwa ndani ya nchi yako, ndio maana tunataka kumuondoa mkoloni mweusi tuliyenaye.
Huwezi kupambana na dola ukiwa peke yako. Achana na hizi oya oya ukafikiri mko wengi.

Siku yakikukuta ndio utajua uko peke yako tu na wazazi wako.
 
Kumshitaki mtu mahakamani si kazi ngumu. Ugumu upo katika kuthibitisha mashitaka ya mtuhumiwa kama kweli nchi husika ina utawala wa sheria.

Je, kuna ushahidi upi kwamba mtuhumiwa amevunja sheria kwa kumkashifu rais aliyeko madarakani?

Ama kuna uhusiano gani unaoweza kuthibitika mahakamani kuwa maneno yaliyozungumzwa na mtuhumiwa yalimlenga rais aliyeko madarakani?
 
Yaani unamteka mtu mara 2, unamtesa, haitoshi, unampa na makosa ya uongo ya madawa ya kulevya (wapo wanaamini Mdude ni drug dealer), ametunzwa gerezani siku 414, baadae mahakama imemuachia huru, anatoa hisia zake, wapambe mnakuja na story za "staha".
wanashangaza
 
Wahenga walisema kua uyaone.

Sasa tunayaona ya CCM.

Miaka mingi CCM wakikutana Dodoma kwenye mkutano mkuu wimbo pendwa ni ule wa CCM nambari one ambao una kibwagizo cha wembe ni uleule.

Basi watafurahi, wataruka na kuonesha ishara ya kuwanyoa wapinzani wao.

Sasa leo hii Mdude Nyagali akitaka kuendelea kuwanyoa mnasema anawatukana.

Katika speech ya Mdude ya dk zaidi ya 3 nyie wanaCCM hamjaona la maana bali moja tu la kumtukana Rais?

Kwanini msiende mahakamani badala yake mnashinikiza jambo ambalo halipo?

Mnataka Samia atumie authority yake vibaya kumfunga au kumuua Mdude bila kuwa na hatia?

Onyo: Msithubutu kumlazimisha Rais Samia Suluhu awe dikteta, mtamponza.

Mlifanya kwa Magufuli leo hayupo.

Mbingu hazilali kama mnavyolala nyie waganga njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…