Pre GE2025 Mgombea Urais wa CCM 2030 lazima awe kijana with zero corruption status. Je, ni nani kati ya hawa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna rais hakuwahi kuwa mwizi!?
Huyo Trump mwenyewe former president wa USA aliiba serikalini.
Ila unaiba je maendeleo yanaonekana!?
Kuhusu kina Dewji na hao wengine kauatilie masakata yao ya kodi na mishahara midogo wanayolipa wafanyakazi wao.
Mfanyabiashara ambaye yuko perfect bwana ni Said Salim Bakhresa tu,wengine wanafuata.
Nina swali moja tu mkuu,Samia kwa rekodi yake ndani ya miaka mitatu amekopa pesa zaidi ya rais yeyote wa Tanzania kuanzia Nyerere mpaka Magufuli,unaweza ukaeleza hizo fedha zilizokopwa zimefanyiwa nini mpaka sasa cha maana!?
 
Umechambua vizuri sana mkuu
 
Moja na kubwa zaidi ameqjiri mamia ya vijana kitu ambacho jpm alishindwa akatelekeza vijana for five years bila ajira. Ameajiti takukiru, polisi, jeshi, walimu nk na kuongesa mishahara pia. Huu ndo ustawi tunaoutaka. Ndoa zilizovunjika zimerudi including me sasa niko pccp
 
Kwahiyo pesa zinakopwa badala ya kuwekeza kwenye jambo productive unatumia kulipa watu mishahara!?
Na huo mkopo unajirudishaje mkuu!?
Una uhakika hakuna waliopoteza kazi kipindi cha Samia?
Kuna miradi ilosimama wafanyakazi wakarudishwa,TRC kuna mabadiliko ya kipumbavu kayafanya yamepunguza watu vyeo na wengine kuwaacha jobless.
Alichokua akifanya Magufuli ni kulifanya hili taifa economic independent,na kama hili lingekamilika tungekua mbali sana.
Furahieni hiyo mishahara kuongezwa ilhali watu wanakopa nje IMF huko na mashirika ya fedha ya kimataifa ili ninyi mpate mshahara,mwishowe ni pesa yenu kupungua thamani na gharama za maisha kupanda.
Sasa sijui hiyo mishahara mikubwa itakua na thamani gani!!??
 
Mtu mzuri bila mfumo imara na katiba ya kueleweka ni kama kuvaa suruali safi njee ,ndani boxa chafu na imetoboka.
 
Yaani kwako ajira siyo productive? Sasa hiyo purchasing power itatoka wapi kama watu hawana ajira?
 
hiyo listi hakuna raisi
 
Yaani kwako ajira siyo productive? Sasa hiyo purchasing power itatoka wapi kama watu hawana ajira?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Aiseee,mkuu hata mahesabu rahisi ya biashara umewahi kufanya!?
Tunatarajia shirika ambalo limeajiri watu ndio lilipe watu mishahara.
Mathalan TRC mapato yake ndio yalipe watu mishahara.
Kukopa ili ulipe watumishi ni sawa na kukopa ili uanzishe biashara ambayo haijapitia transition period na wala haujui mapato yake na wala haijakomaa.
Mapato ya Tanzania yako chini,hayo mapato hukusanywa katika mashirika mbali mbali ya serikali na ya watu binafsi.
Kama mapato tu HAYAJATOSHELEZA KULIPA WATUMISHI MISHAHARA MINONO NA KUAJIRI WENGINE,je kwa kukopa ili muajiri na kuongezea watumishi mishahara,je mtawezaje kulipa hiyo mikopo mliokopa!?
Ilhali mapato yenu tu hayakutosheleza kulipa mishahara minono!?
Sasa toeni mchanganuo mikopo itakua ni asilimia ngapi ya pato la taifa halafu uone namna kitavyowalamba pakubwa.
 
Tuna Rais mpya na UPYA wake 2025.

Msijitoe ufahamu.
 
Hakuna hapo mbona.

Naweza kuwa mimi.
 
Hawa karibu wote 2030 watakuwa na miaka 55 na zaidi je ndio vijana hao. Au ni vijana wa kwenye siasa ?
 
Hayo unayajua wewe ila mi naenjoy maisha kwa sasa mana nina ajira. Jpm alikuwa shetani kwangu mana kidogo nijinyonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…