Unakumbuka nini, tukio gani kila ukilikumbuka unaishia kucheka?
Vipi JF imekuletea michongo gani na connection ipi!
Umewahi kubahatika kuonana na member yoyote nje JF?
Unahisi miaka ya sahivi na miaka ile kuna utofauti gani hapa jukwaani.
Ulikuwa wapi kipindi kile ofisi za JF zinapigwa msako mkali? Au kipindi kile Makonda na Zitto wako active huku.
Unahisi saivi makali ya nyuzi ndani ya JF yamepoa au ndio yameongezeka.
Any story unaeza share.
Matukio ni mengi sana hasa la kukutana na Members wa humu.
Kuna Member nilikua namkejeli sana kuna siku akajitambulisha yeye ni nani na yupo nchi za Gulf ni Mkurugenzi wa fedha na utawala. Akasema anakuja Tanzania kama kuna member anataka kuonana naye namba ya Simu ni hii.
Kama utani nikachukua ile namba na kweli siku aliosema anakuja niliiacha sikumpigia baada ya siku 2 jioni nikampigia, akapokea mpambe wake na akasema Dr yupo VIP chamber ilikuwa hotelini ni Selena Hotel. Nikaingia reception kusubiri lakini baadae nikaona Wapambe wameshiba kama wale waliokuwa wanamlinda JPM (RIP). Nilitetemeka mnoo ukizingatia nilikuwa below 25 yrs mbona niliamua kutoroka na kukimbia.
Kuna member mwingine humu alikuwa anapenda sana kutukana na alikuwa anapigwa BAN mara kwa mara na akawa kama Mshikaji wangu. Akaniomba namba ya Simu nashangaa baada ya siku tat namba ya UK inanioigia akajitambulisha.
Aliporudi Bongo akanipigia tukakutana JB Bellmonte NSSF Posta mpya, sikuamini anachoandika mtandaoni na alivyo, akajitambulisha ni Dr UK na anachukua PhD ya udaktari huko UK. Tukapiga sana vyombo pale. Na akanipa namba yake ya Tanzania.
Kuna siku tukiwa na baadhi ya Members wa humu Malijendary (Sasa wamekuwa adimu humu) uso kwa uso tulikutana na Nape Nnauye enzi hizo Publicity & Ideology wa Kijani, alitukata jicho baya sana 😅
Currently nimekuwa nikikutana na Member mmoja ambaye ni muhimu sana, tunapiga story na kupeana miongozo mbalimbali ya mambo. Long life Legend
Mshana Jr
Yapo mengi sana na Mimi nikiwa na muda nitaandika uzi. Nina miaka 16 ndani ya JamiiForums