Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Hakuna muendesha taxi mwenye mshahara mmoja/anayetegemea taxi tu ambaye bado yuko sokoni.

Ndiyo maana yake wanaolalamika kuwa kipato chao ni kidogo ktk shughuli wafanyazo mjini wasililie mkulima au sekta ya kilimo ibanwe na serikali.

Bali wafanye shughuli zingine za ziada. Tanzania ni tajiri wa rasilimali za asili ikiwemo ardhi. Nchi zingine ardhi yote inamilikiwa watu wenye hati miliki za ardhi, hivyo hawana fursa ya kurudi kijijini au mkoani wakalime au kufuga na kuvua samaki. Tanzania mapori na ardhi ya rutuba zipo na hazimilikiwi wala kuhodhiwa na watu.

Bado kuna shughuli za uvuvi, mifugo n.k ni wakati wa kuachana na umachinga, bodaboda na bajaji turudi mikoani tukafanye shughuli zingine.
 
Uko sahihi 100% kwa sababu tukitegemea tu aina moja ya uzalishaji tunajiwekea mazingira magumu,tufanye kazi halali ili baadaye zitusaidie sisi na jamii inayotuzunguka.
 

KATIBU MKUU KILIMO ARIDHISHWA NA SKIMU YA UMWAGILIAJI MVUMI KILOSA​


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa skimu ya umwagiliaji kijiji cha Mvumi wilaya ya Kilosa ambayo imefikia asilimia 94 ya ujenzi na tayari wakulima wameanza kunufaika.
Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya mradi huo uliopo wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro chini ya mradi wa Kuongeza Tija na uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP).Katibu Mkuu huyo alisema mradi wa umwagiliaji kijiji cha Mvumi umegharimu shilingi Bilioni 1.97 na utanufaisha wakulima wengi wa zao la mpunga katika wilaya ya Kilosa kuongeza uzalishaji na tija.
Source : KATIBU MKUU KILIMO ARIDHISHWA NA SKIMU YA UMWAGILIAJI MVUMI KILOSA – Tanzania Agricultural Development Bank
 
Serikali yetu ingefanya juhudi ili Diesel isipande, wangeacha Petroli hata ipande vipi haina athari sana kwenye mfumuko wa bei,
Diesel iondolewe makodi kodi mengi.
Gari za petroli ni nyingi kuliko za Diesel na kuna gari za petrol ambazo zinafanyiwa biashara. Sasa usichukulie poa kisa unaendesha Civilian ya hesabu.
 

Serikali inayojielewa hutoa ruzuku inayoeleweka kwa wakulima.
 
Morogoro, Tanzania

Mkulima mwanamke aliyepata mafanikio makubwa kupitia kilimo


Source : Kilimo TV
 
Tulipokuwa tunasema Magu ni genius na mzalendo watu walikuwa hawaelewi. Wakaruhusu kudanganywa na propaganda za upinzani na wanaharakati wanaotekeleza ajenda za wazungu.

Sasa wengine ndiyo wataelewa!
Mpumbavu yule....sisi wakulima tulishindwa hata kununua uniform za shule kisa bei za mazao kuwa chini....
tunashukuru sasa ingalao
 
Huwa mnakera sana mnapomtaja huyo marehemu
 
Serikali inayojielewa hutoa ruzuku inayoeleweka kwa wakulima.

Upo sahihi lakini ndiyo hivyo tena mkulima hapati ruzuku ambayo itahakikisha bei za mazao yake kama zikiporomoka bei ktk soko huria, basi mkulima alindwe kwa kupatiwa ruzuku aweze kurudisha gharama za uzalishaji ili msimu unaofuta aendelee kulima tena.

Ruzuku kwa Tanzania zipo kwa wakubwa wanaopatiwa maVX-8 ya shilingi milioni 500,000,000, marupurupu kugharamia fenicha za nyumbani na ofisini za bei ghali kabisa, safari za 'kikazi' na ziara kibao zinazoambatana na posho kubwa n.k
 
Hali mbaya unaambiwa vita ya Ukraine kila kitu nivita tu..
 
Mimi mwenyewe ni muhanga nakula asubuhi na jioni saa 12 jioni tuu, siku imeisha
 
Wameuza sana nje mazao wakati ndani chakula hakitoshi eti wapate kupendwa na wafanyabiashara..
 
Mimi mwenyewe ni muhanga nakula asubuhi na jioni saa 12 jioni tuu, siku imeisha


Mkuu maeneo ya kulima hayajaisha na vibarua wa kuwaweka wakufanyie kazi ukiwalipa wapo wamejaa vijijini kwanini tusiwe tunalima kuepuka adha hizi
 
Wapo mkuu na kuna mkulima maarufu wa mchele mbeya juzi tu kapata tenda ya kuuza maelfu ya tani za mchele kila mwezi kwenda Kenya au nae huyo sio mtanzania?
Kwa Tz, hakuna mkulima anayeweza kuwa na uwezo wa kufanya hiyo biashara eti maefu ya tani za mchele kwa mwezi?
Mkuu dunia imebadilika na kama unadhani mazingira yanaruhusu utajirikie kupitia bei za shamba ingia uone moto wake watu wanasafirisha mahindi anafika na mzigo anakula loss
Hujanielewa, mimi nilikuwa namkatalia jamaa, aliyesema kuwa wakulima msimu huu wamefaidika kutokana na nafaka kuwa juu, nikasema sio kweli, kwani wakulima wetu wengi wakaishavuna wao ni kuuza tu, ila wanao kuja kufaidika ni wafanya biashara ambao wao hununua mazao mengi kipindi cha mavuno na kuyaweka kwenye maghara hadi bei zipande, ndipo wauze, sikatai nao kuna wakati wanapata hasara kutokana na bei, kuwa chini, kwa muda mrefu, hii biashara ya mazao nimeifanya sana hada mpunga ninajua nini nasema.Mfano kipindi cha mavuno una nunua gunia la mpunga kwa tsh.25, 000 ukiuhifadhi baada ya muda hasa kuanzia miezi ya 12-1, hilo gunia unaweza kuliuza kwa 80, 000-100, 000!!
 
Wameuza sana nje mazao wakati ndani chakula hakitoshi eti wapate kupendwa na wafanyabiashara..

Usijali mkuu serikali inayo maghala ya chakula hivyo kikipingua itafungulia maghala isitoshe zipo njia nyingine nyingi tu ilimradi bei zisishuke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…