Hawezi kukujibu. Ameongozwa na chuki tu kwa Samia as a Person. Mheshimiwa amefanya yote yaliyoachwa na mtangulizi wake..kuanzia miradi ya mkakati (SGR, Bwawa la Nyerere, Daraja la Busisi, barabara za Mwendo kasi, n.k, n.k). Pia ameanzisha yake miiingi tu kwenye elimu, afya na kilimo.
Kikubwa kafanya yote bila kuwabana watumishi, wamepandishwa madaraja na mishahara kinyume na mtangulizi wake ambaye hakupandisha madaraja wala kuajiri kwa muda wa miaka 6!.
Aangalie pia rekodi za mapato ya TRA kabla na baada, tena mapato yameongezeka bila watu kufungiwa akaunti zao wala kuporwa fedha zao kupitia Burea-de change.
Chuki za mtoa mada kwa Samia..ni chuki kwa Samia as a Person. Wananchi wanaona walipotoka na walipo. Kauli zake hizi za hovyo na chuki wala haziwezi kumkatisha tamaa Mh Raisi.