Mimi ni Mkristo mlokole, nimeanza kukosa Imani na ukristo nahisi Uislam ndiyo dini ya kweli

Nilimsikia nabii mkuu na mtume mkuu dr Geordavie kwamba yeye anafanya mambo makuu kuliko Yesu! Sababu yeye anatoa hela na misaada ya fedha na mitaji wakati Yesu hakutoa fedha wala mitaji. Waumini walishangilia na kuweka hela miguuni mwa mtume mkuu!
Yani ni maigizo kweli kweli mkuu.
Kuna muda mambo yanayoendelea kanisani ni bora walevi bar.
Kwaya zimejaa uzinzi, wachungaji na manabii nao pia, mavazi na uimbaji utadhani uko fiesta.
Mahubiri siku hizi 99% ni toa ndugu, na yanamfaidisha mchungaji anakula bata dubai na kuishi kama elon musk.
Ukiwauliza, majibu ni Mungu anaangalia moyo.
Wakati imeandikwa kilicho ndani mwako kitajidhihirisha nje.
Hao akina geodavie wanajiita manabii kila sku kuna nabii mpya.
Ukweli ni kwamba siku hizi watu hawaendi kanisani kuabudu bali wanataka kuwa part of a community tu.
 
Nimegundua we unachukulia dini Kama timu ya kushabikia. Unaona man u imeanza kufungwa unahamia man city...ukimaliza kuruka ruka hizi dini utafika conclusion kuwa zote ni man made zimeundwa na binadamu kwa ajili ya binadamu.
 
Sasa unatupa taarifa au unatupa habar
 
Kijibwa cha mudi kinaleta papara hapa na kujifanya kipo chachi.
 
Nikushukuru kwanza kwa kulitambua Hilo. Ila nikushauru kitu kimoja kabla hujaamua kuhamia kwa waislamu. Chunguza vizuri dhehebu la waadventista wasabato utagundua kitu
Yale yale ya kuabudu siku wewe muache aende akawe muislam then akaonje joto la jiwe,watu wanakimbilia favours za ajabu mimi nina experience na hili jambo.

Mke zaidi ya mmoja sijui kutoa talaka na vitu kama hivyo imani iliyojengwa rohoni haiachwi kizembe zembe hivi kuna cha ziada unafikiri anakotaka kuhamia hakuna wanaotaka kutoka?,wapo huko sababu wanajua wanafanya nini sasa kama mtu anafanya kwa ajili ya fulani huyo apewe nafasi
 
Yesu Hana kanisa ,kanisa linaongozwa na mchungaji Kila muumini ana mchungaji wake ,mchungaji akipotoka kanisa lote linapotoka !
Kichwa cha kanisa ni Kristo, kwahiyo kiongozi ni Yesu na siyo Mchungaji.

Wakolosai 1:17
Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

Wakolosai 1:18
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.

Wakolosai 1:19
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote
ukae;


Soma pia:

Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
Efe 5:23‭-‬24 SUV

 
Mkakati ni ule ule haujawahi badilika,

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Marko 16:15-16
Sawa mkuu
 
Sio kweli ila ukristo sio baba yangu Wala mama yangu
Kama kweli we ni mkristo Unajua ni wapi kwa kupata majibu!ila kama upoupo tu unataka mambo yaende unavofikilia hutoacha kuhamahama ibada za mwanadamu,hata huko uislam Kuna mambo ukikuta tofauti utahama,mwisho utapotea mazima
 
Umejibu vema sana mkuu...

Nakazia, Ukimjua Kristo hata dhambi haiwezi kukutenganisha nae:

Rum 8:35‭, ‬38‭-‬39 SUV
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Mleta mada anzia hapohapo ulipo kumtafuta Kristo Upya.
 
shida sana.Mungu atusaidie tu mambo ni mengi muda mchache,thtabaki wenye vifua vikubwa tunaweza kupambana na mawimbi.kwa mfano huna sadaka unaenda kukaa siti ya mbele kabisa kuonesha hauendi church kwa ajili ya kutoa bali kumwonba Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…