KITABU CHA YOSHUA BIN SIRA

- ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Mwandishi alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyetunga kitabu chake kwa Kiebrania mnamo miaka 196 KK - 175 KK huko Aleksandria (Misri).

Halafu mjukuu wake alikitafsiri kwa Kigiriki akitanguliza dibaji. Wakatoliki na Waorthodoksi wanakubali kama Neno la Mungu tafsiri hiyo, si maandiko asili.

Kitabu kinatoa hasa maadili yanayofanana na yale ya Kitabu cha Mithali.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.


Katika hicho kitabu kuna hii sehemu ambayo itatusaidia kuhusu wajibu wetu kwa wazazi wetu:




WAJIBU WA WATOTO KWA WAZAZI:

1
Wanangu sikilizeni mawaidha ya baba yenu.
Fanyeni ninayowaambia,
nanyi mtawekwa salama,

2
Maana Bwana amewapa kina baba mamlaka juu ya watoto wao,
na kuimarisha uwezo wa kina mama juu ya watoto wao.

3
Anayemheshimu baba yake anajipatia msamaha wa dhambi zake.

4
Anayemheshimu mama yake anajiwekea hazina kubwa.

5
Anayemheshimu baba yake atafurahishwa na watoto wake mwenyewe,
na atakapomwomba Bwana, atasikilizwa.

6
Anayemheshimu baba yake atapata maisha marefu,
anayempendeza mama yake anamtii Bwana.

7
Mtoto huyo, huwatumikia wazazi wake kama Bwana wake.

8
Mheshimu baba yako kwa maneno na matendo,
ili upate baraka kutoka kwake.

9
Maana baraka za baba huimarisha nyumba za watoto,
hali laana ya mama huingoa misingi ya nyumba zao.

10
Usijikuze mwenyewe kwa kumdharau baba yako.
Maana kumdharau baba yako hakutakuletea faida.

11
Maana fahari ya baba mtu ni fahari ya huyo mtoto,
na watoto wasiomheshimu mama yao ni balaa.

12
Mwanangu, mtunze baba yako alipo mzee
wala usimhuzunishe muda wote aishipo.

13
Hata akipungukiwa akili, umvumilie.
Usimdharau kwa vile wewe una afya na nguvu.

14
Bwana hatasahau wema wako kwa baba yako,
utakusaidia kukupatia msamaha wa dhambi zako.

15
Wakati wa taabu Bwana atakumbuka wema wako.
Kama umande kwenye jua, dhambi zako zitatoweka.

16
Anayemtupa baba yake anamkufuru Mungu;
anayemkasirisha mama yake analaaniwa na Bwana.
 
Hakika
 
Ndo ukute mzee enzi akiwa na nguvu alikuwa mnyanyasaji, show atakayopewa atafurahi na roho yake
Ndiyo. Kuna mzee alikuwa akimpiga sana mkewe kipindi akiwa na nguvu. Uzee akapalalaizi upwnde mmoja akawa hajiwezi.

Mkewe akaanza kumsulubu mpk ukiona mateso yale, unaona hata ukatili wa shetani una nafuu. Acha kabisa!
 
Wazee wengi wanajitakia mtoto akiwa mdogo mama anakuwa mkali ila mzee anakuwa kazini sio hajui utundu wa mtoto so akuwa fair...katika kipindi mtoto ni mdogo mama anakuwa mkali sana na sio rafiki kuliko baba.

Vice versal tuongee ule ukweli wazee wengi wakizeeka wanakuwa na hasira haswa wasio na pesa kapata mafao hata kushaurika hataki ,hasira hasira zisizo na kifani ..wakati huo mama kazeeka anakuwa kama mtoto na kupenda kukaa karibu na wanae hata anaweza hata kufokewa na watoto.

Wazee wengi hapa bongo sijui umaskini wakizeeka wanakuwa na gubu na hasira za ovyo ndo maana watu wanawakimbia..Hao wastaafu hawataki ushauri wanajiona wanajua sana kumbe kichwa chenga tupu.
 
Wanaume kama umebahatika umeajiliwa na ukafikia kustaafu,usifanye kosa
kutumia mafao yako kujenga nyumba n.k
weka pesa yako kwenye mifuko ya akiba kama vile UTT na benki kuu
siku nguvu zikiisha hata kama mkeo hakupendi atapenda pesa,utatunzwa hadi umauti ukukute,
Tatizo kubwa linalowakumba wanaume,mshahara wote unatunza familia.
unasomesha watoto,unashindwa kujenga nyumba ya ndoto yako.
kununua gari ya ndoto yako,ukipata mafao ya uzeeni unajenga nyumba na kununua gari
na pesa yote inaisha,unaanza kulaani watoto kwa kutokukutunza.

Ni kweli watoto wana wajibu wa kuwatunza wazazi wao,ila
wanaume tujitahidi kuweka akiba,tusijisahau.
 
Hakika
 
Kuna jambo la kuangalia pia,wakati wa utoto mara nyingi watoto Huwa na ukaribu na mama hivyo hutengeneza bond,baba wengi Huwa ni watu wakali Kwa watoto,ni mara chance kukuta watoto Wana ukaribu na baba zao.
Ni mfumo wa malez ila ukikuw jiongez
 
Maisha yako ya sasa hivi na mke wako na watoto wako ndo yata-determine maisha yako ya uzeeni. Sasa hivi unawachukulia poa halafu ikifika uzeeni unataka uheshimiwe.

Hakuna kitu kama hicho na mtaendelea kufa mapema. Tunzeni familia zenu vizuri acheni ubabe usiokuwa na maana.

Hapa jirani kuna mama kafiwa na mume wake kama miezi miwili hivi imepita, ukimuona sasa hivi alivyorudi kuwa binti huwezi amini, anang'aa balaa...hana pesa ila kapendeza bwana. Ni kama mume alikuwa anampa stress.
 
Ndiyo. Kuna mzee alikuwa akimpiga sana mkewe kipindi akiwa na nguvu. Uzee akapalalaizi upwnde mmoja akawa hajiwezi.

Mkewe akaanza kumsulubu mpk ukiona mateso yale, unaona hata ukatili wa shetani una nafuu. Acha kabisa!
Na mara nyingi inakuwa hivyo. Ukimnyanyasa mke na akakuvumilia usitegemee uzeeni atakupenda. Lazima upigike
 
Wanaume tunafikiria sana ubongo unachoka wanawake unaweza kukuta kuanzia asubuhi hajawaza kitu cha kumpasua ndonga..kingine wanaume mihamala too much inatusubiri too much control number [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…