Mjadala: Kwanini wanaume wengi hufa mapema? Wanawake tuhurumieni please...
Wanaume tunafikiria sana ubongo unachoka wanawake unaweza kukuta kuanzia asubuhi hajawaza kitu cha kumoasua ndonga..kingine wanaume mihamala too much inatusubiri too much control number [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwa kawaida mwanamke anaumiza Sana kichwa wakati wa kutafuta mume. Akishampata na akaolewa anaingia ktk likizo ya maisha.

Kwa upande wa mwanaume, siku anayoingia kwenye ndoa ndiyo siku anaanza stress za maisha. Ndiyo maana tafuti zinaonesha wanaume ambao hawajawahi kuishi na wake (kuoa) huishi Sana.
 
Ndo ukute mzee enzi akiwa na nguvu alikuwa mnyanyasaji, show atakayopewa atafurahi na roho yake
Ukiwa mnoko kama sisi, lazima uhakikishe unawekeza ili ufaidi uzeeni. Ni ujinga kutowekeza maana unapostaafu sema at 60, ukipata pension yako haraka unaibwaaga BoT. Hutategemea vihela vya watoto
 
Kwanini wanaume wanakufa mapema
20230130_175634.jpg
 
Wanaume tunafikiria sana ubongo unachoka wanawake unaweza kukuta kuanzia asubuhi hajawaza kitu cha kumpasua ndonga..kingine wanaume mihamala too much inatusubiri too much control number [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji28][emoji28]
Hii nayo kweli unawaza kule nitume 30K huku natakiwa kutuma 100K hujakaa sawa hela ya school bus.. ile unageuka mjomba/shangazi kakupiga ngeu bado wana kitaaa.

Hapa nimekaa nawaza fundi ataniambia kifaa kinauzwa sh ngapi maana huko chini mguu wa kulia nimeusikia unagonga mbaya. Sasa yote haya unaachaje kupata stress ha ha potelea mbali yote maisha tu acha tufe waje wengine
 
Wenzetu jamii ya Asia, walitatua hiyo changamoto kwa kuishi na watoto wao boma moja, hii inasaidia sana kutoa hiyo changamoto.

Kwa sisi wanaume ambao labda tuna nguvu kwa sasa, ni kupambana na kuweka misingi kama ya hao wenzetu; kwangu haina maana niwagharamie watoto wangu, halafu mwisho wa siku wote watukimbie.

Kama utaoa mtoto wangu, kaa kwenye boma langu; na kama utaolewa na vijana wangu kaa kwenye boma pia. Hii itapunguza ile hali ya kupata msongo wa mawazo.

Bila hivyo, mtajikuta kwenye uzee unabaki na mkeo kama mlivyokuwa wawili wakati wa kuchumbiana.
 
Apandacho mtu ndicho avunacho. Tuchunguze baba anaepitia mateso haya enzi za ujana wake alimtreat vipi mke wake. Kuna mzee amestaafu mpaka leo anamtreat mke wake vibaya mno. Na watoto wameoa na kuolewa wanaona namna mama yao anateseka. Wanamjengea nyumba kimya kimya wamuondoe hapo. Na fedha zote anatumiwaga mama yao. Baadae huyu mzee atakuja alalamike watoto wanamtenga? Hakuna namna; Atapokea 50k huku mkewe akipata 200k. Lakin wako baba zetu waliotulea sisi na mama zetu vizuri. Leo Mungu atatuhukumu tukimshit baba yetu maana kiukweli tunamtukuza Mungu kwa ajili yake. So what you deposit is what you will withdraw.
 
Hizo zote ni useless, shida n moja tu mnatumika sana enzi za ujana wenu na wengine hadi uzee wao bado wanajikuta bado wapo, sasa lazima achoke sana na mwishowe kujifia mapema ukichanganya na magonjwa ya uzeeni ndio basi tena
 
Duh kweli bhana, wengine tumeanza kuexperiece tunajiliwaza mitandaoni akili isizimike.
Kikubwa ni kujikujipenda zaid ss wnyewe (wanaume) kwanza, kutoruhusu stress zisizo za lazima, kujipa wakat wa kuburudisha nafsi zetu.....bila kuathiri majukum yetu kwa familia.....hakika tutakufa wakat wa Mungu.
 
Wanaume kama umebahatika umeajiliwa na ukafikia kustaafu,usifanye kosa
kutumia mafao yako kujenga nyumba n.k
weka pesa yako kwenye mifuko ya akiba kama vile UTT na benki kuu
siku nguvu zikiisha hata kama mkeo hakupendi atapenda pesa,utatunzwa hadi umauti ukukute,
Tatizo kubwa linalowakumba wanaume,mshahara wote unatunza familia.
unasomesha watoto,unashindwa kujenga nyumba ya ndoto yako.
kununua gari ya ndoto yako,ukipata mafao ya uzeeni unajenga nyumba na kununua gari
na pesa yote inaisha,unaanza kulaani watoto kwa kutokukutunza.

Ni kweli watoto wana wajibu wa kuwatunza wazazi wao,ila
wanaume tujitahidi kuweka akiba,tusijisahau.
Kuna projects moja enzi hizo ndio nimetoka chuo kwenye team tulikuwa na wazee , mda fulani wa jioni baada kupiga masanga. Wale wazee wakaniambia dogo hakikisha una account yako ya kutunza hela zitakazo kulea uzeeni ambayo mke wako haijui na kuna mmoja akasema ana nyumba yake ya siri ambayo mke wake haijui nikasema duu haya mapya.
 
Ilikua jumapili Wakati Narudi toka mizunguko yangu ya kumsalimu rafiki angu anaeishi Malamba mawili. Kabla yakufika nyumbani nilipita kumsalimu rafiki yangu ambae tumefahamiana toka 2014 ofisin kwake pharmacy ni mtaalamu wa madawa. Nilifungua mlango nikamkuta kijana makamo 25-28 anajaribu kunusuru ndoa yake kwa kuomba ushauri kwa rafiki yangu muuza madawa ,kuwa afanye nini mke wake ana msaliti na amemuoa tayari akiwa na mtoto mmoja.

Kijana uyo ni mpambanaji sana anajihusisha na shughuli za uuzaji wa machungwa stendi kulingana na mujibu wa kazi yake huwa anatoka sa mbili asubuhi na kurudi sa tano ya usku. Amekua akijitahidi sana kumtimizia mkewe mahitaji yake yake muhimu napoongea ivo watu wazima wanakua wananielewa vizuri.

Siku za karibuni alikua akihisi mkewe ana mahusiano na mtu mwingine mana upendo aliouzoea umepotea hadi penzi kupoteza dira . Kijana alihisi ivo baada ya kuona dalili mbalimbali katika mahusiano yao ikiwemo kumnyima unyumba kwa siku tatu (3) , akamdanganya kuwa ana mimba yake lakini kila akimwambia twende tukapime anakataa ikumbukwe ni mke wake halali na pia mwanamke anakua yupo busy sana kuchat kipindi wapo pamoja badala yakumjali mumewe. Kila alipo ulizwa alisema yakua anawasiliana na rafiki zake waliosoma pamoja amna lolote baya.

Kadri siku zinavozidi kwenda kijana anakosa aman anakua mtu wa mawazo baada ya ndoa yake kuingia dosari. Siku ya Jumamosi alivorudi katika mizunguko yake alioga akala na akajipumzisha kitandani kutoka na hali ya msongo wa mawazo iliyokua inamkabili alishindwa kupata usningz vyema wakat huo bibie tayari alikua ashalala fofofo. Akasikia mlio wa meseji kuingia kwenye simu ya mkewe hakusita aliamua kuichukua ili ajue ni nini kinaendlea sio kawaida nyakati za usku mseji kuingia ilikua n mida ya saa 7 usku ,,meseji ilikua ikisomeka ivi "MKE WANGU NAOMBA TUKUTANE PALE TUNAPOKUTANA SIKU ZOTE" ,, Kijana alipigwa na Butwaa kubwa na mapigo ya moyo kuenda kasi Nakujiuliza kitu gani amekosa kama mahitaji yake ya msingi anampatia tena kwa wakati? Katika kuchunguza zaidi alikuja kugundua namba iliyotuma uo ujumbe ni namba ya mpenzi wake wa zamani ambae wamezaa nae huyo mtoto mmoja. Balaa linazidi kuwa zito

INAENDELEA ..............
 
1.Nyerere,Mama Nyerere anadunda.
2.Mkapa,Mama Mkapa anadunda
3.Karume,Mama Karume anadunda.
4.Magufuli,Mama Magufuli ana dunda.
5.Maalimu Seif,Mama Maalimu anadunda.

Hao ni watu ambao matibabu na fedha kwao sio issue.

Huku mtaani sasa ukitazama wanaume kibao wametangulua na kuacha wanawake,juzi tu nimetoka kumzika swahiba wangu aliekua hapo TRA Ilala,kaacha mke na kachanga,jamaa kazaliwa 86 tu!!
 
Ilikua jumapili Wakati Narudi toka mizunguko yangu ya kumsalimu rafiki angu anaeishi Malamba mawili. Kabla yakufika nyumbani nilipita kumsalimu rafiki yangu ambae tumefahamiana toka 2014 ofisin kwake pharmacy ni mtaalamu wa madawa. Nilifungua mlango nikamkuta kijana makamo 25-28 anajaribu kunusuru ndoa yake kwa kuomba ushauri kwa rafiki yangu muuza madawa ,kuwa afanye nini mke wake ana msaliti na amemuoa tayari akiwa na mtoto mmoja.

Kijana uyo ni mpambanaji sana anajihusisha na shughuli za uuzaji wa machungwa stendi kulingana na mujibu wa kazi yake huwa anatoka sa mbili asubuhi na kurudi sa tano ya usku. Amekua akijitahidi sana kumtimizia mkewe mahitaji yake yake muhimu napoongea ivo watu wazima wanakua wananielewa vizuri.

Siku za karibuni alikua akihisi mkewe ana mahusiano na mtu mwingine mana upendo aliouzoea umepotea hadi penzi kupoteza dira . Kijana alihisi ivo baada ya kuona dalili mbalimbali katika mahusiano yao ikiwemo kumnyima unyumba kwa siku tatu (3) , akamdanganya kuwa ana mimba yake lakini kila akimwambia twende tukapime anakataa ikumbukwe ni mke wake halali na pia mwanamke anakua yupo busy sana kuchat kipindi wapo pamoja badala yakumjali mumewe. Kila alipo ulizwa alisema yakua anawasiliana na rafiki zake waliosoma pamoja amna lolote baya.

Kadri siku zinavozidi kwenda kijana anakosa aman anakua mtu wa mawazo baada ya ndoa yake kuingia dosari. Siku ya Jumamosi alivorudi katika mizunguko yake alioga akala na akajipumzisha kitandani kutoka na hali ya msongo wa mawazo iliyokua inamkabili alishindwa kupata usningz vyema wakat huo bibie tayari alikua ashalala fofofo. Akasikia mlio wa meseji kuingia kwenye simu ya mkewe hakusita aliamua kuichukua ili ajue ni nini kinaendlea sio kawaida nyakati za usku mseji kuingia ilikua n mida ya saa 7 usku ,,meseji ilikua ikisomeka ivi "MKE WANGU NAOMBA TUKUTANE PALE TUNAPOKUTANA SIKU ZOTE" ,, Kijana alipigwa na Butwaa kubwa na mapigo ya moyo kuenda kasi Nakujiuliza kitu gani amekosa kama mahitaji yake ya msingi anampatia tena kwa wakati? Katika kuchunguza zaidi alikuja kugundua namba iliyotuma uo ujumbe ni namba ya mpenzi wake wa zamani ambae wamezaa nae huyo mtoto mmoja. Balaa linazidi kuwa zito

INAENDELEA ..............
Mayage yenga wa mpanda alioa watatu kwa mpigo sababu yake alisema alisha wahi kuoa mke moja alimtesa sanaa, shauri huyu rafiki yako pamoja na machungwa aongeze matunda mengine kama maembe na tikiti avute wa pili, hao wa dudu wa kianza hawatibiki
 
Back
Top Bottom