Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Sawa mkuu! Ila Aneth Msuya angekuwa ni dada yako wa kuzaliwa leo BP yako ingekuwa 200 baada ya kupokea hii hukumu.
Nimekuambia kuwa tatizo lako unatumia hisia zaidi badala ya sheria. Sasa huoni huyo aliyeachiwa naye angefungwa kama alikuwa hajatenda ingekuwa siyo vizuri? Kuna kukata rufaa na kama vipi wanatakiwa wakate. Kimsingi mimi silalamiki kwa sababu siyo nakubali kuwa hakuua, bali sina ushahidi wa kuwa aliua na wala sijui kesi iliendaje, na ni ushahidi gani ulitolewa.
 
Let's assume wewe ni kaka wa Aneth Msuya, baada ya hii hukumu ya leo. Ungefanyaje?
 
Sasa muuaji ni nani? Serikali itaendelea kufanya utafiti wa kumpata muuaji au kesi ndiyo itakuwa imeishia hapo?
Hawa wahusika walioachiwa huru wana haki ya kudai fidia ya usumbufu miaka nane,na muda walioupoteza huko ili hali hawakuwa na hatia.
 

Familia ya hovyo sana hii
 
Your browser is not able to display this video.

Wakili Peter Kibatala akielezea kesi ya mjane wa Bilionea Msuya baada ya Mahakama Kuu kumwachia huru Miriam Mrita.

"Watu wa Arusha nawatania kidogo, nimewaletea dada yenu, wifi yenu na shemeji yenu, hatudaiani tena" - Peter Kibatala Wakili wa Mjane wa Bilionea Msuya.

Pia soma:
- Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haikumkuta na hatia
 
Hiii ndo inatumika sana kwetu, watu wanapigwa tego anahaha nalo huko.
 
Ile kesi ilihitaji majaji mahiri kama akina Lugakingira, sio hawa UPE! Kakolaki hawezi ku handle kesi kama hiyo..... tuwekee hapa tuipite tuone reasoning ya Judge!
Shida sio kakolaki.

Kakolaki ni mzoefu kwenye kesi za jinai kafanya miaka mingi tangia akiwa wakili aa serikali , kapitia pia tume ya kupambana na madawa ya kulevya, huko ndiko anakopajua.

Tatizo lipo kwenye upepelezi, haufanyiki vizuri, niliwahi kushauri hapa na pia tume ya haki iliyoundwa na kumpa ripoti Rais Samia ilikuja na maoni kama hayo kuwa iundwe taasisi maalum ya upelelezi wa makosa ya jinai.

Bila kufanya hivyo tutarudi hapa kulaumiana kila siku.
 
Hakuna watu wa hovyo kama polisi! Wanaharibu sana kesi za mauaji kwa tamaa zao! Ifike mahali wananchi wamalize hizi changamoto kienyeji! Sumbawanga/Katavi/Kigoma siyo mbali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…