johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Haki ni ya Mungu wa Mbinguni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hukumu iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, ya mjane wa bilionea wa madini, Bilionea Msuya, Miriam Steven kusomwa leo.
Miriam pamoja na mshtakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, wanakabiriwa na shtaka la mauaji ya kukusudia, wanadaiwa kumuua kwa kumchinja, Aneth Elisaria, mdogo wa marehemu bilione Msuya.
Hukumu hiyo inatarajiwa kusomwa na Jaji Edwin Kakolako, ambayo ndiyo itaamua hatima yao kama wana hatia au lah. Kama watakutwa na hatia hukumu ni kunyongwa hadi kufa.
Watuhumiwa wamekuwa mahabusu kwa nane na leo ndio hatima yake, je, nini kitatokea leo Mambo yatakuwaje? Nini itakuwa hukumu ya kesi hii? Mke wa Msuya na mwenzake watakutwa na hatia au lah?
Mjane wa Bilionea Msuya alikuwa anatetewa na Wakili Peter Kibatala.
Hongera? Our legal system is very corrupt. Wenye jinai na hela ndio hu walk away with it. Ila the innocent are always getting shoved behind the bars.Hongera zake aisee ameteseka sana
Mahakama kuu kanda ya Dar-es-salaam imemuachia huru mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na revocatus Muyella baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
Ila leo imesaidiaLabda uwe na mafungamano na siasa.
Lakini pesa haisaidii chochote
Na huyo Revocatus Everist Muyella naye kachomoka!! Hatma ya kesi ya msingi ikoje? Kama hahusiki, muuaji halisi ni nani? Miaka 8 kwa nini serikali imekomaa na watuhumiwa ambao hawana ushahidi nao wa kutosha?Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemkuta hana hatia Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha...
Ajilinde na awe Makini kwani Uhai wake unaweza ukawa Mikononi mwa upande wa Marehemu Mumewe kama sehemu ya Kulipiza Kisasi.ACHA afaidi matunda ya mmewe
Hcho ni kifungo tosha, kibatala kama kibatala, watu walisema anamlia mjane hela tu, wakate rufaa basi.Miaka 7+ mahabusu si mchezo , mwenye fedha hafungwi.
Ni aibu kwa Jamhuri kuwashikilia watuhumiwa kwa miaka zaidi ya 8 huku wakiwa hawana ushahidi uliojitosheleza.Mahakama kuu kanda ya Dar-es-salaam imemuachia huru mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na revocatus Muyella baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
Kwa hiyo Aneth Msuya hakuuwawa?Ni aibu kwa Jamhuri kuwashikilia watuhumiwa kwa miaka zaidi ya 8 huku wakiwa hawana ushahidi uliojitosheleza.
Wafungue shauri upya sasa la mauaji ya marehemu ili wahusika halisi akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.
Naona utabiri umetimia. Watuhumiwa wameachiwa huru huku wananchi tukiachwa njia panda!Wataachiwa hawa, ukiwa na pesa Tanzania kufungwa ni ujinga wako tu
Alikufa ila walomuua sio waliofunguliwa kesi, jamuhuri imeshindwa kvthibitisha, jamuhuri iwasake wauaji, hiyo ndo hoja ya mwambaKwa hiyo Aneth Msuya hakuuwawa?
Kama sio walikuwa wameshitakiwa, ni akina nani walio muua Aneth Msuya?