Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya


Hukumu tayari imeshatolewa jioni hii. Tega sikio kwenye taarifa ya habari saa 2 usiku.
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemkuta hana hatia Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha...
Na huyo Revocatus Everist Muyella naye kachomoka!! Hatma ya kesi ya msingi ikoje? Kama hahusiki, muuaji halisi ni nani? Miaka 8 kwa nini serikali imekomaa na watuhumiwa ambao hawana ushahidi nao wa kutosha?

Nadhani kuna uzembe kwa wapelelezi wetu! Ila pia Wakili Msomi Peter Kibatala na jopo lakr watakuwa wametisha sana. Maana wameigaragaza Jamhuri kwa mara nyingine tena.
 
Mahakama kuu kanda ya Dar-es-salaam imemuachia huru mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na revocatus Muyella baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
Ni aibu kwa Jamhuri kuwashikilia watuhumiwa kwa miaka zaidi ya 8 huku wakiwa hawana ushahidi uliojitosheleza.

Wafungue shauri upya sasa la mauaji ya marehemu ili wahusika halisi akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.
 
Ni aibu kwa Jamhuri kuwashikilia watuhumiwa kwa miaka zaidi ya 8 huku wakiwa hawana ushahidi uliojitosheleza.

Wafungue shauri upya sasa la mauaji ya marehemu ili wahusika halisi akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.
Kwa hiyo Aneth Msuya hakuuwawa?

Kama sio walikuwa wameshitakiwa, ni akina nani walio muua Aneth Msuya?
 
Wataachiwa hawa, ukiwa na pesa Tanzania kufungwa ni ujinga wako tu
Naona utabiri umetimia. Watuhumiwa wameachiwa huru huku wananchi tukiachwa njia panda!

Maana haileti mantiki kwa Jamhuri kuwashikilia watuhumiwa kwa miaka chungu nzima huku ikiwa haina ushahidi uliojitosheleza kuhusu uhusika wao katika hayo mauaji.

Na baada ya hii hukumu, wawatafute wauaji halisi sasa wa huyo marehemu kama kweli hawa watuhumiwa wawili walioachiwa leo, hawahusiki na hayo mauaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…