Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Daah polen sana Auntuja polen sana dada zangu, na wazee wangu. Rafiki yangu Erasto Mungu azid kukupa pumziko la Aman tuonane ile asubuh iliyo njema. that's how life it's. Jambo la muhimu kukumbuka daima ni hili.
Kabla hujaoa piga magoti funga hata mwez tu muombe Mungu akupe mke wa kuwa nae maishan. Mungu sio dhalimu utapata. Unaweza kuoa mtu mmoja akasambaratisha familia nzima. Hiz sura na makalio yasikupofushe hakuna jipya aisee. Mtwisheni Mungu fadhaa zenu mbona liko wazi. Watu wengi wanateseka coz ya kwenye maamuz ya kuoa. Kumbuka wanawake wameamka na wanaume itabid tuwe macho. Kuna maisha baada ya hela ambayo ni mateso matupu.
'Hiz sura na makalio yasikupofushe hakuna jipya'uko sahihi sana,wengi wameumia hapo.Angalia mfano wakina Diamond,Ali Kiba,Harmonize n.k,wanajitahidi kwa pesa zao kuchukua wanawake walio wazuri ajabu,lakini baada ya muda mfupi unashangaa mahusiano yamevunjika...
 
Mambo ya Mahakamani mtu kufungwa ni mpaka iwe proven beyond reasonable doubts (kwahio kama ushahidi ulikuwa na mashaka hata kidogo basi mtu atakuwa hana Hatia)

It is better that ten guilty persons escape than one innocent suffer. - Ingawa na huyu kwa kukaa ndani muda wote huu hata kama alikuwa innocent inaonesha walakini katika kushughulikia haya mambo kwa haraka....

Anyway Andhaa Kanoon - Na hii sio Bongo tu bali dunia kwa Ujumla
 
Mambo ya Mahakamani mtu kufungwa ni mpaka iwe proven beyond reasonable doubts (kwahio kama ushahidi ulikuwa na mashaka hata kidogo basi mtu atakuwa hana Hatia)

It is better that ten guilty persons escape than that one innocent suffer. - Ingawa na huyu kwa kukaa ndani muda wote huu hata kama alikuwa innocent inaonesha walakini katika kushughulikia haya mambo kwa haraka....

Anyway Andhaa Kanoon - Na hii sio Bongo tu bali dunia kwa Ujumla
Kama ulimsikiliza kwa makini na kwa kutafakar alichosema siku zile Rostam Aziz wala hutashangaa kilichotokea. Kuna kitu kinaitwa siasa za mahakaman mzee hata uwe na ushahid live kesi itapigwa dana dana ili upatikane upenyo tu wapite na wewe kama wamedhamiria. That's why kila cku nasema hii life kwa Africa ni kudance according the tune. Tofauti na hapo umeumia.
 
Narudia tena Hii sio Africa tu.....; Exhibit A: O. J. Simpson Case
1708770518883.png
 
Shida sio kakolaki.

Kakolaki ni mzoefu kwenye kesi za jinai kafanya miaka mingi tangia akiwa wakili aa serikali , kapitia pia tume ya kupambana na madawa ya kulevya, huko ndiko anakopajua.

Tatizo lipo kwenye upepelezi, haufanyiki vizuri, niliwahi kushauri hapa na pia tume ya haki iliyoundwa na kumpa ripoti Rais Samia ilikuja na maoni kama hayo kuwa iundwe taasisi maalum ya upelelezi wa makosa ya jinai.

Bila kufanya hivyo tutarudi hapa kulaumiana kila siku.
Rais anaruka ruka tu na ndege kila siku.
Nchi hii inapaswa iwe na National Bureau of Investigation, iwe inajitegemea kabisa. Polisi wetu hawana issue. Tena hiyo taasisi iajiri watu vichwa tupu, watu watakaofanya reasoning wakiwa trained vizuri. Wanasayansi kwa ajili ya bio-investigations (forensic), wachumi na business na wanasheria. Vijana wa kazi, wapewe task na target kama business vile. Wawe na power ya kukamata pia na ikibidi matumizi ya silaha.
Halafu waziachie mahakama zifanye kazi.

Kabla mtu hajakamatwa, basi upelelezi uendelee kimya kimya. Haina maama kumuweka mtu kizuizini wakati upelelezi haujakamilika.
Polisi wabaki kutuliza ghasia, barabarani na ulinzi wa maofisi basi.
 
Wakili anaingiaje hapo wakati hapo swala ni upelelezi na vidhibiti hafifu?
Walaumiwe Polisi
Nani kakudanganya ushahidi ndio kila kitu? Ni lazima uwe na mawakili mazuri hasa kwenye mahojiano na Cross examination ya ushahidi, utetezi, exhibits kama hauwezi tetea hoja vizuri hata kama una ushahidi utaanguka. Mfano Sabaya ushahidi ulikuwepo cha ajabu kosa lilikua kwenye aina ya mahakamai iliyosikiliza kesi! Mambo ya hovyo kabisa mawakili wa serikali.

Ifike kipindi ofisi ya DPP na DCI labda wapewe Dp world iendeshwe kiufanisi zaidi maana hawa mawakili wa mishahara hawana cha kupoteza
 
Vijana wa kazi, wapewe task na target kama business vile. Wawe na power ya kukamata pia na ikibidi matumizi ya silaha.
Halafu waziachie mahakama zifanye kazi.
Unless tender iwe ya mtu binafsi ila as long as ni serikali na check number inasoma mshahara kila mwezi ufanisi utakua chini sana. Maybe wasiwe na salary ila walipwe based on the tasks they successfully execute wawe tu kama private investigators
 
Yes, itangazwe tender kama kampuni ya ulinzi. Na wasiingiliwe mambo yao. Kila baada ya miaka 5 mkataba mpya kwa kutangaza tender. Check number zinaharibu sana, kama unavyoona mawakili wa serikali.
 
Mimi nadhani ofisi ya mwendesha mashtaka na wapelelezi wao wanafanyaga makusudi. Kwa kesi kama ya Sabaya, unakoseaje majina ya mtuhumiwa? Na kwanini hakimu wa mwanzo anahukumu, in favor of prosecutor baadae kwenye rufaa anashinda mrufani? Huu si mpango kabisa watu wanakuwa wamepanga?

Kuna ile kesi ya aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha, somebody Pima na wenzake. Unaambiwa mahakama iliyomhukumu haikuwa na jurisdiction ya kusikiliza hiyo kesi. Why hakimu alikaa akasikiliza na kufanya hukumu? Hajui? Mwendesha mashtaka hajui?
Kwanini mahakama haikutupilia mbali tangia mwanzo?
 
Wakili anaingiaje hapo wakati hapo swala ni upelelezi na vidhibiti hafifu?
Walaumiwe Polisi
Tatizo watu wanachanganya haki na taaluma. Mbele ya sheria kila mtu ana haki (hata muuaji) ya kupewa Wakili wa Kumtetea. Tena Wakili anakwambia useme ukweli wa kilichotokea then baada ya hapo anatafuta weak points ili Mteja wake ashinde kesi. Kwenye kesi hii Wakili aliyekuwa anamtetea Mtuhumiwa hana shida. Tatizo lipo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashtaka wetu. Yawezekana hawajajengewa uwezo wa kutosha wa kupambana kisheria na Mawakili Binafsi ambao ni Wabobevu.
 
Back
Top Bottom