Mkakati wa kumchosha na kumpotezea Muda Tundu Lisu utafanya kazi?

haha harusi ya Mfanyabiashara tu hapo Kariakoo

Michango week 2 Milion 700.

Chadomo

Chama pendwa bado mnakusanya michango kama ushuru wa choo cha stendi?

Chadema wana viongozi 3000 nchi nzima na bado milion 300 inawatesa😂
Ndio nakuambia watanzania 70m wanapewa msaada na Sweden ya watu chini ya 10m na isiyo na raslimali kama sisi, ww huogopi?
 
Watanganyika hao wanaochanga 400M wiki nzima ndio wataweza kuwa wadhamini wa Lissu?
Yaonekana unaandika ukiwa huna reference. Issue ya kuwalipia kina Mbowe na Msigwa faini ya milioni 400 zilichangwa na watu gani kama sio hawa watanganyika wasio na kipato unaowadogosha?
Unastahili kudharaulika kuanzia sasa kwa kujitambulisha kuwa chawa mwandamizi!
 
Wengi, Siku za nyuma ilikuwa inaonekana hakuna mbadala wa Slaa. Lakini Lisu ameonekana ni zaidi ya Slaa pamoja na kukitumikia cheo chake kipya kwa kipindi cha chini ya miezi mitatu tu.

Kweli kabisaa ndani ya miezi iyo mitatu wafuasi wa Chadema zaidi ya mia 300 wameuwawa kwa sera zake za kukinukisha AKA Savimbi wa Bongo👈

Leo michango haipatikani ❗️ wachangiaji ndio wale wameondoka na sera zake za kukinukisha🦘 ✍️
 
Yaonekana unaandika ukiwa huna reference. Issue ya kuwalipia kina Mbowe na Msigwa faini ya milioni 400 zilichangwa na watu gani kama sio hawa watanganyika wasio na kipato unaowadogosha?
Unastahili kudharaulika kuanzia sasa kwa kujitambulisha kuwa chawa mwandamizi!

Sasa wale wenye moyo wa kuchangia manake ni Wafuasi kweli kweli 👈

wenyewe wameitikia wito wa mwenyekiti wenu mpya TUNDU Savimbi kuwataka wakakinukishe

leo Michango imegoma wachangiaji hakuna yumkin wamesepa na Mo29 🦘🦘

kiongozi bora au bora
kiongozi❗️
 
Alikuwa ameshika bunduki siku hao watu wakiuwawa? Au waliuwawa ili kulinda kura 31m za kupika?
 
Yaonekana unaandika ukiwa huna reference. Issue ya kuwalipia kina Mbowe na Msigwa faini ya milioni 400 zilichangwa na watu gani kama sio hawa watanganyika wasio na kipato unaowadogosha?
Unastahili kudharaulika kuanzia sasa kwa kujitambulisha kuwa chawa mwandamizi!

Tujadili kwa hoja. Ingawaje sitakuzuia kutoa maoni yako ya kiwango cha chini na wala sina tatizo na labeling utakayoamua kuifanya.

Watanzania ni jamii Maskini. Kusema wao ndio watamdhamini Lisu ikitokea anapelekwa nginja nginja kama hivi leo. Hawatakuwa na msaada wowote.

CCM kupitia serikali, wanauwezo wa kumfunga Lisu miaka nenda rudi mpaka mwisho wa uhai wake. Na Watanzania wasiweze kufanya jambo lolote kumnusuru. Sasa huo udhamini wa Watanzania unaouzungumzia ni upi?

Watanzania ambao maandamano tuu ya kushinikiza jambo fulani lifanyike wanashindwa kuandamana walau siku Tatu mfululizo. Njaa zitaanza kuwabana.

Tujitahidi tuwe realistic
 
Sasa wale wenye moyo wa kuchangia manake ni Wafuasi kweli kweli 👈

wenyewe wameitikia wito wa mwenyekiti wenu mpya TUNDU Savimbi kuwataka wakakinukishe

leo Michango imegoma wachangiaji hakuna yumkin wamesepa na Mo29 🦘🦘

kiongozi bora au bora
kiongozi❗️
Hakuna michango iliyogoma bali ccm wameitishia nmb na kuzuia watanganyika wasiweze kuchangia. Huo ni uoga wa mbwakoko ambaye hukalia mkia au kuufyata!
Lisu ni shujaa wa watanganyika na usavimbi upo huko unakolamba makalio! Mtaanguka tu saa yenu ikitimia.
 
Kina shabiby wa Gairo kila siku wanayasema bungeni. Tena zaidi ya Polepole.
Kwa kiwango na undani wa alivyo kuwa anaongea Polepole?
Umejiuliza kwanini hao akina Bashe na Shabiby hawajapotezwa?!
Kwanini hao hawana wafuasi au shabiki wengi kama Lissu na Polepole?
BTW, hoja yako ulisema Polepole hakuongea kabla hajawekwa pembeni, hicho ni nini na ilikuwa lini?
 
Tujadili kwa hoja. Ingawaje sitakuzuia kutoa maoni yako ya kiwango cha chini na wala sina tatizo na labeling utakayoamua kuifanya.

Watanzania ni jamii Maskini. Kusema wao ndio watamdhamini Lisu ikitokea anapelekwa nginja nginja kama hivi leo. Hawatakuwa na msaada wowote.

CCM kupitia serikali, wanauwezo wa kumfunga Lisu miaka nenda rudi mpaka mwisho wa uhai wake. Na Watanzania wasiweze kufanya jambo lolote kumnusuru. Sasa huo udhamini wa Watanzania unaouzungumzia ni upi?

Watanzania ambao maandamano tuu ya kushinikiza jambo fulani lifanyike wanashindwa kuandamana walau siku Tatu mfululizo. Njaa zitaanza kuwabana.

Tujitahidi tuwe realistic
Kwanza ndugu mbwabwajaji, maandamano siyo culture ya watanzania elewa. Hata hivyo wewe na ccm mnatumia dola kuikanyaga katiba kwa kuzuia maandamano ya amani yaliyoruhusiwa kikatiba!
Pili mmetumia dola kuizuia nmb isiendelee kupokea michango ya wazalendo wa kweli wenye mapenzi yaliyopitiliza kwa cdm pamoja na kuwaagiza mapandikizi yenu (chaumwa) kuiga tonetone ili kuipunguzia cdm wigo. Tunajua na unajua kuwa huo ni utoto!
Kuhusu kumfunga hamna ushahidi wa kutosha juu ya tuhuma mlizombambikia na mnajisumbua na kujiaibisha tu!
Wewe umejitanabaisha humu kama mshauri, washauri hao ccm wako jinsi ya kuliponya taifa na kulileta pamoja ni kutafuta vichwa vipya vyenye akili timamu viishauri ccm namna bora ya kulimaliza swala hili la kijinga la uhaini wa mtu mmoja.
Najua unatafuta majibu ya wadau ili ukaishauri ccm iendelee au ijitoe kwenye aibu ya kuangukia pua kwani siku zao zahesabika ni bado kitambo kidogo tu. Lisu ni shujaa wetu, mtamwachia tu hamna namna.
 
Sijasema Mimi ni Mungu.
Hapa tunajadili. Alafu kutoa maoni sio kazi ya Mungu
Hukutoa maoni bali ulikuwa unatupa assurance kwamba Lissu hawezi kuwa Raisi,ngoja nikupe story kidogo,mimi nilikuwa na kiongozi wangu fulani hivi Msenegali,miaka kama minne iliyopita tukiwa naye ofisini nikaona anashangilia sana,nikamuuliza nini akaanza kunionyesha picha iloyokuwa kwenye simu yake kwamba kiongozi wa chama cha siasa nchini kwao kafungwa jela,akanitamkia jina lake akiitwa Fae,yule kiongozi wangu alikuwa anajipiga kifua kweli kweli kwamba wamemkomesha na Fae hatakuja kuinuka tena,lakini Fae baadaye alikuja kuwa Waziri mkuu tena miaka michache tu tokea ule mwaka.
Kwa hiyi hapa chini ya jua wewe binadamu usijifanye Mungu
 
Kwanza ndugu mbwabwajaji, maandamano siyo culture ya watanzania elewa. Hata hivyo wewe na ccm mnatumia dola kuikanyaga katiba kwa kuzuia maandamano ya amani yaliyoruhusiwa kikatiba!
Pili mmetumia dola kuizuia nmb isiendelee kupokea michango ya wazalendo wa kweli wenye mapenzi yaliyopitiliza kwa cdm pamoja na kuwaagiza mapandikizi yenu (chaumwa) kuiga tonetone ili kuipunguzia cdm wigo. Tunajua na unajua kuwa huo ni utoto!
Kuhusu kumfunga hamna ushahidi wa kutosha juu ya tuhuma mlizombambikia na mnajisumbua na kujiaibisha tu!
Wewe umejitanabaisha humu kama mshauri, washauri hao ccm wako jinsi ya kuliponya taifa na kulileta pamoja ni kutafuta vichwa vipya vyenye akili timamu viishauri ccm namna bora ya kulimaliza swala hili la kijinga la uhaini wa mtu mmoja.
Najua unatafuta majibu ya wadau ili ukaishauri ccm iendelee au ijitoe kwenye aibu ya kuangukia pua kwani siku zao zahesabika ni bado kitambo kidogo tu. Lisu ni shujaa wetu, mtamwachia tu hamna namna.

Robo Tatu ya siasa na yaliyo ndani ya katiba sio Utamaduni wetu kama Waafrika.

Wewe kama mtu wa culture elewa
a) Kiafrika hakunaga Demokrasia hasa ya vyama vingi.

b) Kiafrika hakuna nchi inaitwa Tanzania wala Tanganyika. Bali kuna wasukuma, wanyamwezi, yao, Chagga, Zulu n.k.

Kwenye masuala ya ushauri nitakuweka wewe uwe mshauri wangu. Maana kazi hii umeiweza hapa. Umetoa ushauri kwa kujiamini. Na hilo limenifanya nikukubali bila wewe kuomba
 
Hamjambo!

Naona hasimu wa Lissu wanachokifanya kutumia mbinu ya kumchosha na kumpotezea Muda wake.
Mbinu hii kisiasa hasa zile siasa chafu inafanyaga kazi hasa kwa watu wenye misimamo mikali kama aina ya Tundu Lisu.

Kuna watu huwezi kuwashinda kwa kifo. Na hawaogopi kufa. Lakini mbele ya muda kila mtu hujikuta akijisalimisha.

Lisu anachoshwa na kupotezewa muda huku wafuasi na wanachama wake wakiwa hawaelewi mpango wa adui ukoje.

Mbinu hii inafanya kazi zaidi pale ambapo wale wanaomdhamini Tundu Lisu wakiwa wanafuatwa na Adui za Lisu kisha mazungumzo yakiendelea huku Lisu akiwa gerezani.

Katika ugomvi wa kisiasa, hakuna mtu atamjali Lisu zaidi ya mkewe na watoto. Na bahati mbaya ilioje. Wadhamini na wazungu wanaomsapoti Tundu Lisu sio familia ya Lisu na hawachangii damu.

Kumaanisha, katika ulimwengu wa maslahi, adui za Lisu watatumia muda huo Lisu akiwa Gerezani kuwekana sawa na wadhamini wake. Huku lisu akiendelea kusota.

Hatari sana.

Tundu Antipas Lissu ni mtu mwenye utulivu wa nafsi kuweza kuwashughulikia wanasheria wote wa serikali waliotumwa na Samia kwa sheria hizi hizi za katiba mbovu, kuliko colonel (rtd) Besigye wa Uganda ambaye juzi alionekana mahakamani akionesha kuathirika na mbinu za utawala wa jenerali Yoweri Kaguta Museveni ..

Samia na utawala wa CCM jiandaeni na nyie kama mnavyo fanya mateso mkitegemea dunia inawachekea.

Huko Uganda, kiongozi mkongwe wa upinzani, Kizza Besigye, anayezuiliwa jela kwa muda mrefu, alianguka siku ya Jumatano akiwa mahakamani na baadaye kulazwa hospitalini akiwa katika hali mbaya.

Soma pia: Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye aanguka ghafla mahakamani, akakimbizwa hospitalini

LIVE MUBASHARA MFUMO WA HAKI JINAI ULIVYOTEKWA NA DOLA - BESIGYE AFOKA VIKALI KABLA YA KUANGUKA

29 July 2026
Kampala, Uganda

Chaotic scenes: Colonel (rtd) Dr Besigye collapses in the dock as he tried to oppose trial without his legal team

View: https://m.youtube.com/watch?v=8iy7HHG-1rg
Today prosecution brought an American security expert Andrew Wilson aka Orlando as its first witness against Besigye. He (Orlando) started providing evidence to court on how Besigye contacted him seeking fire arms and other military support and guidance to overthrow gov't
 
Tundu Antipas Lissu ni mtu mwenye kuliko colonel (rtd) Besigye wa Uganda ambaye juzi alionekana mahakamani akionesha kuathirika na mbinu za utawala wa jenerali Yoweri Kaguta Museveni

LIVE MUBASHARA MFUMO WA HAKI JINAI ULIVYOTEKWA NA DOLA - BESIGYE AFOKA VIKALI KABLA YA KUANGUKA

29 July 2026
Kampala, Uganda

Chaotic scenes: Colonel (rtd) Dr Besigye collapses in the dock as he tried to oppose trial without his legal team

View: https://m.youtube.com/watch?v=8iy7HHG-1rg
Today prosecution brought an American security expert Andrew Wilson aka Orlando as its first witness against Besigye. He (Orlando) started providing evidence to court on how Besigye contacted him seeking fire arms and other military support and guidance to overthrow gov't

Besigye ana muda gani korokoroni kwa kesi hizo za kubumba?
 
Ni mara yake ya kwanza Besigye kupambana na mbinu za mtawala Museveni, Tundu Lissu amepambana na tawala za CCM tangu enzi za Mkapa, Kikwete, Magufuli hadi Samia anaendelea kuwashughulikia mahakamani mfumo mbovu wa chama dola kongwe unaokuja kwa mbinu tofauti katika kila awamu.
 
Je washirika wa Lisu watakuwa wavumilivu?
 
Acha uovu wao utimie kwanza na kikombe kijae na kufurika.
 
Back
Top Bottom