Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

duh! kwa sababu Halisi kpoint out ukweli kwenye hili keshakuwa hafai...kazi kweli kweli

Imagine angisifu hii MoU mngemuona ana maana sana siyo?

Ameongea ukweli gani hapo? Yaani kuhusisha Lowasa na Mahalu na MoU? Wewe kweli akili yako haijai kisoda..!
 
..mara baada ya Raisi Mwinyi kuingia madarakani kuliibuka kikundi cha wahubiri[matata,ngariba,mazinge] wa Kiislamu ambao walikuwa wanatumia muda mwingi kuikosoa Biblia kuliko kuelekeza mema yaliyo katika Kuran.

..Wakristo walipeleka malalamiko yao serikalini lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali kusitisha mahubiri yale ya kichochezi na kashfa dhidi ya Ukristo.

..kana kwamba masuala ya mahubiri dhidi ya Ukristo hayatoshi Prof.Kighoma Malima akiwa waziri wa elimu akaibuka na kuandika barua kwenda kwa Raisi Mwinyi akidai kwamba Wakristo wanapendelewa ktk kupewa nafasi za kuendelea na elimu ya sekondari.

..utawala wa Alli Hassan Mwinyi ulijijengea mazingira ya kuonekana kwamba unachukia na kukandamiza Ukristo na Wakristo Tanzania.

..mazingira hayo ndiyo yaliyomuweka ktk "corner" na akalazimika kusaini hii MOU na mashirika ya Kikristo.

..matokeo yake ni serikali kupoteza shule na hospitali ilizokuwa imetaifisha toka mashirika ya Kikristo.

..ndiyo maana nikasema hii MOU was a CHESS MOVE. Mzee Mwinyi had to appease Chritian Organisations so that he could regain their trust and support.
 
Kuna baadhi ya watu humu wako so indulged into religious differences than facts.
Kuna IDs ambazo nikiziona tu basi wao ni mambo ya mafarakano ya dini.
Mimi sijui wenzangu kama mmesha kuwa na diversity na mambo mbalimbali kama dini, nchi, makabila. Nadhani ni vizuri ukajichanganya ktk dini au imani mbalimbali ndipo utaweza kua-apreciate the difference. Haya malumbano ya utofauti wa kidini to me ni non sence. I believe kila mtu katika dini yake akiwa muadilifu na mwema atakwenda mbinguni if at all kuna mbinguni.

So chill out guys acheni mambo inginge ya ku-argue vitu ambavyo sometimes havijengi. Lets discuss about the issue lakini tusiingie kwenye kuingilia uhuru wa imani za watu wengine. It is all about respect.

Tuwaweke hapa majina yao ili ijulikane HAAMBILIKI hapa ni nani:-
1. Game Theory,
2. Tumain,
3. MaxShimba
4. X-Plaster
5. ....................... (Ongezeeni)
 
GT,

..kazi gani tena?

..kila kwenye jina la taasisi ya Kikristo unaweka jina la Bakwata au Shura ya Maimamu.

..this is a chess game my friend.

..serikali imejiingiza "mkenge" kusaini MOU na taasisi za Wakristo, now they have to do the same kwa Waislamu,Mabohora,Baniani etc etc.

NB:

..naona umemtupia kidongo Edward Lowassa kuwa ndiye signatory kwa niaba ya serikali.

..kukumbusha tu, hiyo MOU ilisainiwa wakati ambapo Alhaji Mwinyi, na Alhaji Prof Kighoma Malima[r.i.p], wakiwa kwenye baraza la mawaziri.

..haiyumkini serikali kuingia mkataba mzito kama huo bila BARAZA LA MAWAZIRI kutaarifiwa.

teh teh teh !
 
Mh JF bwana we don't have great thinkers. Wanajiita great thinkers lakini the puppet master anavuta kamba zao kama watoto wadogo. I can see now that any fool can cause trouble for peace in Tanzania. Now I see why even our leaders take us for a ride. Endeleeni kukubali kutumika na kama by now hamjamjua huyo puppet master ni nani basi akili zimelala kuliko nilivyo dhani.
 
4.jpg


Pamoja na kukupongeza kwa ujasiri wako, tafadhali scan all these pages and make them into a PDF and attach it here.. THANK YOU!
 
Mh JF bwana we don't have great thinkers. Wanajiita great thinkers lakini the puppet master anavuta kamba zao kama watoto wadogo. I can see now that any fool can cause trouble for peace in Tanzania. Now I see why even our leaders take us for a ride. Endeleeni kukubali kutumika na kama by now hamjamjua huyo puppet master ni nani basi akili zimelala kuliko nilivyo dhani.

Mkuu.....huku ndio kumkoma nyani Giladi......na hapo tupo ukurasa mmoja.......maneno mazito kabisa...........na ni wachache sana wanaolielewa hilo............asante sana mkuu kwa kuliweka wazi namna hiyo.........I love JF wallah..............!!
 
Kuna msemo kuwa wakati mwingine mtu anatengeneza kimbunga kwenye kikombe cha chai. Ukishasoma hiyo MOU unatakiwa ufikie mahitimisho gani?

a. Serikali imesaini mkataba na taasisi ya kidini
b. Kutia sahihi huko ni kinyume na sheria
c. Ni kinyume cha sheria kwa sababu ni dini ya taasisi ya dini ya kikristu.
d. Hivyo, serikali imeipendelea taasisi hiyo na hivyo imeupendelea Ukristu.

Well.. ni kweli?
 
Hivi hizi shule na hospitali ndugu zetu waislamu wanazozipigia kelele..ingekuwa kweli haziruhusu kutoa huduma kwa waislamu..hawa ndugu zetu wangekuwa wapi kielimu au kihuduma nyinginezo? Jamani tuache kuangalia maendeleo katika mwanga wa wao na sisi. Mimi sioni tatizo kama waislamu na wao watakubaliana na serikali yetu kutoa huduma. Ukweli ni kwamba kwa sasa mambo yamebadilika..waislamu hawawezi kuwa na network thabiti ya kutoa huduma nchi nzima kama wakristo..its historical. na inabidi walikubali tuu. Huo uwezo na network haipo!

Maendeleo ya muislamu hayatatoka Saudia wala Iran..yatatokana na muslam mwenyewe..ndo maana siku hizi wakristo wana-insist kwenye self help projects..hata makanisa tunajenga wenyewe..hatutegemei pesa ya vatican...sasa wakubwa mkianza kusema kwamba huduma za kijamii ni za kikristo..nadhani ni kupotosha ukweli..mimi nimesoma shule ya mission...na tulikuwa na waislamu kibao! na kila Ijumaa walikuwa hawafanyi kazi..wakati wengine tunaenda kulima....so is wasabato kila Jmosi walikuwa off....na hii ilikuwa shule ya Kikatoliki kweli kweli..Yaani unajua ninaposoma comments za wanaojiita waislamu humu..naona kama vile ni watu wanaoongozwa na fanaticism tuu..kwa sababu they are out of touch with reality! Hizi huduma ni muhimu kwetu sote. Na serikali inalijua hili. Au watu mnataka wote tusilimishwe ndo mjue kwamba Tanzania waislamu wanathaminiwa?

Watu tunaongelea swala la kadhi..lakini, wengi wanaolipinga ni kwa sababu..hii mahakama itaendeshwa nchi nzima kwa kodi za watanzania wote..sasa kama mpaka leo hatujaweza kuzihudumia mahakama zetu..ndo tutaweza kuhudumia kadhi`s court? Ndo maana wengine wanasema hili swala libaki huko huko..na hakuna atakayenyoosha kidole..The opposition ni tax implication kwa mwananchi..na hata ikianzishwa...malalamiko yataendelea kama wakikosa pesa za kutosha..watasema wananyimwa pesa kwa sababu mahakama ni za waislamu.....and on and on...

You dont need a PhD from Mzumbe to know kwamba huduma za wakristo zinatunufaisha watanzania wengi..sema tuu kuna ambao hawataridhika hata kama ungetusilimisha watanzania wote..

So stop whining! Lets do what we can do to uplift ourselves.
 
ama kweli waislam wa tanzania wavumilivu

duh!

Ulitaka wafanye nini, washike bakora? Ni vyema basi uwahamasishe wazichangamkie huduma hizo, kuliko kung'ang'ania mahakama ya kadhi ambayo bado haitawakomboa kielimu na kiafya.
 
Hii MoU haina uhusiano na kitu kama mahakama ya kadhi. Hii MoU inaonesha tu kuwa serikali inaweza ikajadiliana na kukubaliana na taasisi yoyote ya kidini katika mambo ambayo hayana uhusiano moja kwa moja na mambo ya kiimani.

MoU inazungumzia social services ambazo makanisa yanaisaidia serikali kuzitoa. Sasa kuna mtu anaamini kuwa hii MoU inajustify kuwepo kwa mahakama za kidini serikalini?? Kichekesho!
 
Mkataba wa Kanisa na Serikali waanikwa

Na Mwandishi wetu, Raia Mwema,

Julai 22, 2009



Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imezidi kuingiwa na misukosuko inayogusa waumini wa dini mbali mbali, na sasa kumeibuliwa hati ya makubaliano (MoU) ambayo Serikali iliingia na makanisa nchini. Makabuliano hayo yalikuwa hayafahamiki kwa Watanzania wengi.

Hati hiyo ya makubaliano, ambayo ilisainiwa na Serikali wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, inaelezwa kuzipendelea zaidi taasisi za Kikristo zinazotoa huduma nchini.

Baadhi ya viongozi wa Kiisilamu nchini wameliambia Raia Mwema wiki hii kwamba mkataba kama huo waliouandaa ulipata kukataliwa na Serikali pamoja na kuwa ulifanana jkwa kila na huo.

Tayari mjadala wa serikali kujiingiza katika masuala ya dini unazidi kupamba moto ukihusisha uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya Waisilamu na kuwapo Waraka wa Kanisa Katoliki unaoelimisha waumini wake kuhusu uchaguzi.

Serikali uliutia rasmi hati ya makubaliano kati yake na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), huku serikali ikiwasilishwa na Edward Lowassa ambaye wakati huo alikuwa waziri mwandamizi.

Hati hiyo, ambayo Raia Mwema imepata nakala yake, iliandaliwa na Profesa Costa Mahalu aliokuwa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha dare s Salaam (UDSM).

Katika hati hiyo, iliyotiwa saini Februari 21, mwaka 1992, upande wa serikali uliwakilishwa na mmoja wa mawaziri wake waandamizi wa wakati huo.

Makubaliano hayo yalifanyika kwa kuzingatia mambo kadhaa, ambayo ni pamoja na hali ya uchumi nchini kutomudu kuiwezesha serikali kutoa huduma za elimu na afya kwa kiwango bora. Msingi mwingine wa makubaliano hayo ni makanisa kuhakikishiwa kuwa serikali itaweka mazingira mazuri kwao kutoa huduma za elimu na afya.

Makubaliano hayo yamegawanywa katika maeneo makubwa mawili, ambayo ni sekta ya elimu na afya na kila sekta ikiwa imetengenezewa bodi yake ndani ya mtandao wa makanisa kupitia CCT na TEC………….

……Hati hiyo pia inaeleza kuwa wajumbe wa kamisheni hiyo watatoka katika CCT na TEC na mashirika wafadhili na kwamba ni lazima shughuli zote ziendeshwe kwa mujibu wa sheria za nchi……..

………Vipengele vinavyoibana serikali katika hati hiyo ya makubaliano mbali na kutoa nafasi za mafunzo ya ualimu, ni pamoja na serikali kutotaifisha shule na taasisi za afya zinazomilikiwa na makanisa nchini.

Kiongiozi mmoja wa Kiisilamu aliyejitanbulisha kwa jina la Omar hassan, ameliambia Raia Mwema kwamba baada ya kuupata waraka wa makubaliano hayo kati ya Kanisa na Serikali, waliandaa waraka kwa ajili ya Baraza Kuu la Taasisi za Kiisilamu ambao ulikataliwa na Serikali.

‘Sisi tulichofanya ni kuandaa waraka kama huo kwa kunukuu kila kitu kama kilivyokuwa katika MoU yao na Kanisa, tukawapelekea wahusika wakatukatalia. Sasa tukasema kama ni suala la huduma na sisi tunazo shule na hospitali zinazoendeshwa na taasisi zetu, kwa nini tuymenyimwa,” alisema Omar………..

……Kwa upande wake, Sheikh Khamis Mataka, ambaye alisema waraka huo ambao uliandaliwa kwa siri hautendi haki, na kwamba unapaswa kufutwa na serikali ili uandaliwe waraka unaozihusu dini zote.

“Ukiangalia sura ya mkataba una mapungufu makubwa sana kwani unatoa upendeleo wa upande mmoja kwa kuwapa fursa ya kufaidika na kutafutiwa pesa na serikali kwa ajili ya taasisi zao za kielimu na kiafya na kutenga nafasi za elimu kwa watumishi wa taasisi hizo kwa upendeleo,” alisema.

Alisema anashangazwa na hoja kwamba uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi usuhusishwe na fedha za serikali wakati mahakama hiyo itakuwa inalenga kusaidia serikali kupunguza mzigo katika mahakama zake…….


Habari kamili angalia raia Mwema Uk wa Pili.

Yeyote mwana-JF mwenye kuwa na story hii kikamilifu aiweke hapa pamoja na waraka wenyewe.
 
MoU kati ya Kanisa na Serikali ilishawekwa hapa jamvini kwa mapana yake, na member mmoja, nadhani ni X-Paster au somebody.
Hii ni ufupisho tu, lakini thanks kwa niaba ya wale wenzangu na mimi ambao labda katka ile original copy lugha iliwapiga chenga kidogo.
 
Duh…! Mambo hayo. Lakini nataka tu kuelimishwa iwapo kiko kipengele katika Katiba yetu kinachoruhusu serikali kuingiliana mikataba na taasisi za dini.

Kama kipo, ni kweli kipengele hicho kinaruhusu tu mikataba ya kutoa misaada ya kipesa kwa taasisi za dini fulani tu na kuzibagua zingine?
 
Huu makataba uliandikwa sana na Magazeti (An-nnur na Mizani) ya Kiislam wakati huo kuwa sio haki kufanywa na Dini moja tu. Lakini Serikali pamoja na jamaa walitia pamba masikioni kama kawaida yao.
 
I dont think we want to go where we are going.
The reason for this country to be neutral in the first place was to avoid these kind of discussions.
The government should not involve itself with any religion.
 
Mkataba wa Kanisa na Serikali waanikwa

Mwandishi Wetu - Julai 22,
SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete, imezidi kuingiwa na misukosuko inayogusa waumini wa dini mbalimbali, na sasa kumeibuliwa hati ya makubaliano (MoU) ambayo Serikali iliingia na makanisa nchini. Makubaliano hayo yalikuwa hayafahamiki kwa Watanzania wengi.

Hati hiyo ya makubaliano, ambayo ilisainiwa na Serikali wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, inaelezwa kuzipendelea zaidi taasisi za Kikristo zinazotoa huduma nchini.

Baadhi ya viongozi wa Kiislamu nchini, wameliambia Raia Mwema wiki hii kwamba mkataba kama huo waliouandaa ulipata kukataliwa na serikali pamoja na kuwa ulifanana kwa kila kitu na huo.

Tayari mjadala wa serikali kujiingiza katika masuala ya dini unazidi kupamba moto ukihusisha uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya Waislamu na kuwapo Waraka wa Kanisa Katoliki unaoelimisha waumini wake kuhusu uchaguzi.

Serikali iliutia saini rasmi hati ya makubaliano kati yake na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Tanzania (CPT), huku Serikali ikiwakilishwa na Edward Lowassa ambaye wakati huo alikuwa waziri mwandamizi.

Hati hiyo, ambayo Raia Mwema imepata nakala yake, iliandaliwa na Profesa Costa Mahalu alipokuwa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Katika hati hiyo, iliyotiwa saini Februari 21, mwaka 1992, upande wa serikali uliwakilishwa na mmoja wa mawaziri wake waandamizi wa wakati huo.
Makubaliano hayo yalifanyika kwa kuzingatia mambo kadhaa, ambayo ni pamoja na hali ya uchumi nchini kutomudu kuiwezesha serikali kutoa huduma za elimu na afya kwa kiwango bora.

Msingi mwingine wa makubaliano hayo ni makanisa kuhakikishiwa kuwa serikali itaweka mazingira mazuri kwao kutoa huduma za elimu na afya.
Makubaliano hayo yamegawanywa katika maeneo makubwa mawili, ambayo ni sekta ya elimu na afya na kila sekta ikiwa imetengenezewa bodi yake ndani ya mtandao wa makanisa kupitia CCT na TEC.

Kwa mfano, sehemu ya kwanza ya hati ya makubaliano hayo, kifungu cha kwanza, kinaeleza kuwa makanisa yataanzisha kamisheni ya uratibu wa utoaji huduma hizo.

Katika kifungu hicho cha kwanza, sehemu ‘a’ hati hiyo inaeleza kuwa jukumu la kamisheni hiyo ni kuandaa sera zinazohusiana na huduma za afya na elimu zinazotolewa na makanisa.

Kifungu kidogo cha nne, sehemu hiyo ya kwanza ya hati hiyo, kinaeleza kuwa kamisheni hiyo itakuwa ikiratibu na kusimamia matumizi ya fedha, mikopo kwa ajili ya kuboresha huduma za elimu na afya.

Hati hiyo pia inaeleza kuwa wajumbe wa kamisheni hiyo watatoka katika CCT na TEC na mashirika wafadhili na kwamba ni lazima shughuli zote ziendeshwe kwa mujibu wa sera na sheria za nchi.

Serikali kupitia hati hiyo pia imekubaliana na makanisa kuanzishwa kwa Mfuko wa Huduma za Kijamii ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kupokea mikopo na misaada.

Pia kwa upande wa elimu, serikali ilikubali kutoa nafasi za masomo ya mafunzo wa ualimu kwa wanafunzi wa ualimu.

Kwa upande wa afya, hati hiyo ya makubaliano inaridhia kuanzishwa kwa Bodi ya Tiba, ambayo jukumu lake la msingi ni kuratibu na kupanua huduma za afya zinazotolewa na makanisa nchini.

Vipengele vinavyoibana serikali katika hati hiyo ya makubaliano mbali na kutoa nafasi za mafunzo ya ualimu, ni pamoja na serikali kutotaifisha shule na taasisi za afya zinazomilikiwa na makanisa nchini.

Kiongozi mmoja wa Kiislamu aliyejitambulisha kwa jina la Omar Hassan, ameliambia Raia Mwema kwamba baada ya kuupata waraka wa makubaliano hayo kati ya Kanisa na Serikali, waliandaa waraka kwa ajili ya Baraza Kuu la Taasisi za Kiislamu ambao ulikataliwa na serikali.

“Sisi tulichofanya ni kuandaa waraka kama huo kwa kunukuu kila kitu kama kilivyokuwa katika MoU yao na Kanisa, tukawapelekea wahusika wakatukatalia. Sasa tukasema kama ni suala la huduma na sisi tunazo shule na hospitali zinazoendeshwa na taasisi zetu, kwa nini tumenyimwa,” alisema Omar.

Kwa upande wake, Sheikh Khamis Mataka, ambaye alisema waraka huo ambao uliandaliwa kwa siri hautendi haki, na kwamba unapaswa kufutwa na serikali ili uandaliwe waraka unaozihusu dini zote.

Sheikh Mataka, ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na kiongozi mwenye kuheshimika, ameliambia Raia Mwema kwamba kimsingi MoU hiyo ya Kanisa na Serikali ilipaswa kuzihusisha dini zote na si kupendelea dini moja.

“Ukiangalia sura ya mkataba una mapungufu makubwa sana kwani unatoa upendeleo wa upande mmoja kwa kuwapa fursa ya kufaidika na kutafutiwa pesa na serikali kwa ajili ya taasisi zao za kielimu na kiafya na kutenga nafasi za elimu kwa watumishi wa taasisi hizo kwa upendeleo,” alisema.

Alisema anashangazwa na hoja kwamba uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi usihusishwe na fedha za serikali wakati mahakama hiyo itakuwa inalenga kusaidia serikali kupunguza mzigo katika mahakama zake.

Kwa upande wake, Askofu Dk. Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, ameliambia Raia Mwema kwamba MoU hiyo hailengi kusaidia dini moja na kwamba hadi sasa imekuwa ikitumika kwa hospitali teule pekee zilizoombwa na serikali.

“Mpaka sasa kipengele cha mashule hakijatekelezwa na hakuna shule hata moja ya kanisa inayopokea misaada toka serikalini. Lakini hata kama itatekelezwa ilikuwa kwa mashule yote bila kujali dini zao, ni kwa madhehebu yote na hadi sasa haijatekelezwa, kama na ndugu zetu nao (Waislamu) wana mashule inawahusu,” alisema.

Dk. Bagonza ambaye amekuwa na msimamo wa kati katika mambo mengi ya msingi ya kijamii na mwenye mahusiano ya karibu na madhehebu yote, alisema serikali ndiyo inayoomba kutumia hospitali teule maeneo ambayo hakuna huduma hiyo.

“Kuhusu hospitali teule, Kanisa huwa haliombi serikali bali serikali kama haina hospitali mahali inaliomba kanisa kuomba kutumia facilities kwa kuchangia gharama ili wananchi wake wapate huduma. Na huduma pale huwa hazibagui mtu yeyote kwa dini yake,” alisema

Wakati hayo yakiendelea, wiki hii viongozi wa dini ya Kiislamu waliokutana katika kongamano lililofanyika katika Msikiti wa Kichangani, Magomeni Dar es Salaam, walitangaza kuzinduliwa kwa chama cha siasa cha kimataifa kijulikanacho kama Hizb-ut-Tahrir.

Kuzinduliwa kwa chama hicho kilicho na mtandao sehemu mbalimbali duniani na kupamba moto kwa mijadala yenye muelekeo wa kidini, kunazidi kuiweka serikali ya Kikwete katika wakati mgumu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Pamoja na kuelezwa kwamba hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa dini kutoa elimu ya uraia kwa waumini wake, hali ya sasa ni ya pekee tokea kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995, jambo ambalo linakiweka Chama cha Mapinduzi (CCM) katika wakati mgumu zaidi.
hs3.gif
 
Nilifikiri ni mkataba wa serikali na dini katika kutoa huduma za kiroho.......kumbe katika kutoa huduma za elimu na afya......mbona kwenye shule hizo za dini na hospital au vituo vya afya wananchi wote wanaruhusiwa kupata huduma? Hapo kuna ubaya gani sasa wakubwa? acha kuchanganya mambo hapa!
 
hakuna SHULE HATA MOJA INAYOPOKEA PESA TOKA KWENYE SELIKALI.kama ipo semeni. humu ndani kuna wakurugenzi wa shule wengi watawaambia. na kama huo mkataba mnaona unawadhuru waislam, upigeni chini, hata sisis wakristo hatuutaki. tunataka kuchangia sisi wenyewe kwenye mashule yetu, tujenge mashule yetu nk. hatutaki waislam watujengee shule, kwasababu hawawezi, uwezo huo hawana hata zao hawajaweza.

kuhusu chama cha kisiasa pale magomeni kichangani kwenye msikiti, hilo halitutii shaka wakristo, ila watz wote ndo liwatie shaka. kwasababu the more you people mnajitenga, the more mtatengeka kikwelikweli katika shule, huspitali na maendeleo mengine. mtabakiwa tu na maendeleo ya kununua mabasi ya kwenda mkoani peke yake. shule hamtaenda, na hospitali mtanyanyapaliwa. ni bora muache tu huo mpango wenu wa kuingiza vyama vya kigaidi tz. HAMNTISHI MTU KWA TAARIFA YENU, NDO MAANA TOKA AWALI WAKRISTO HAWAOGOPI. hawatishiki, ni tishio la watz wote sio wa dini moja tu.
 
Naona huyu mwandishi ameandika kwa mapungufu fulani , anapo linganisha huo mktaba wa wakatoliki na ule ambao wenzetu wanadai ulikataliwa alitakiwa aweka na huo wa wenzetu na ikiwezekana barua ya serikali ya kukata mapendekezo yao na ikiwezekana sababu za kuwakatalia, ama sivyo hii habari inakuwa ni sawa na kulinganisha Andazi na kitumbua, vyote ni vitafunio lakini ladha ni tofauti.
 
Back
Top Bottom