Mkataba wa Kanisa na Serikali waanikwa
Na Mwandishi wetu, Raia Mwema,
Julai 22, 2009
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imezidi kuingiwa na misukosuko inayogusa waumini wa dini mbali mbali, na sasa kumeibuliwa hati ya makubaliano (MoU) ambayo Serikali iliingia na makanisa nchini. Makabuliano hayo yalikuwa hayafahamiki kwa Watanzania wengi.
Hati hiyo ya makubaliano, ambayo ilisainiwa na Serikali wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, inaelezwa kuzipendelea zaidi taasisi za Kikristo zinazotoa huduma nchini.
Baadhi ya viongozi wa Kiisilamu nchini wameliambia Raia Mwema wiki hii kwamba mkataba kama huo waliouandaa ulipata kukataliwa na Serikali pamoja na kuwa ulifanana jkwa kila na huo.
Tayari mjadala wa serikali kujiingiza katika masuala ya dini unazidi kupamba moto ukihusisha uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya Waisilamu na kuwapo Waraka wa Kanisa Katoliki unaoelimisha waumini wake kuhusu uchaguzi.
Serikali uliutia rasmi hati ya makubaliano kati yake na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), huku serikali ikiwasilishwa na Edward Lowassa ambaye wakati huo alikuwa waziri mwandamizi.
Hati hiyo, ambayo Raia Mwema imepata nakala yake, iliandaliwa na Profesa Costa Mahalu aliokuwa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha dare s Salaam (UDSM).
Katika hati hiyo, iliyotiwa saini Februari 21, mwaka 1992, upande wa serikali uliwakilishwa na mmoja wa mawaziri wake waandamizi wa wakati huo.
Makubaliano hayo yalifanyika kwa kuzingatia mambo kadhaa, ambayo ni pamoja na hali ya uchumi nchini kutomudu kuiwezesha serikali kutoa huduma za elimu na afya kwa kiwango bora. Msingi mwingine wa makubaliano hayo ni makanisa kuhakikishiwa kuwa serikali itaweka mazingira mazuri kwao kutoa huduma za elimu na afya.
Makubaliano hayo yamegawanywa katika maeneo makubwa mawili, ambayo ni sekta ya elimu na afya na kila sekta ikiwa imetengenezewa bodi yake ndani ya mtandao wa makanisa kupitia CCT na TEC
.
Hati hiyo pia inaeleza kuwa wajumbe wa kamisheni hiyo watatoka katika CCT na TEC na mashirika wafadhili na kwamba ni lazima shughuli zote ziendeshwe kwa mujibu wa sheria za nchi
..
Vipengele vinavyoibana serikali katika hati hiyo ya makubaliano mbali na kutoa nafasi za mafunzo ya ualimu, ni pamoja na serikali kutotaifisha shule na taasisi za afya zinazomilikiwa na makanisa nchini.
Kiongiozi mmoja wa Kiisilamu aliyejitanbulisha kwa jina la Omar hassan, ameliambia Raia Mwema kwamba baada ya kuupata waraka wa makubaliano hayo kati ya Kanisa na Serikali, waliandaa waraka kwa ajili ya Baraza Kuu la Taasisi za Kiisilamu ambao ulikataliwa na Serikali.
Sisi tulichofanya ni kuandaa waraka kama huo kwa kunukuu kila kitu kama kilivyokuwa katika MoU yao na Kanisa, tukawapelekea wahusika wakatukatalia. Sasa tukasema kama ni suala la huduma na sisi tunazo shule na hospitali zinazoendeshwa na taasisi zetu, kwa nini tuymenyimwa, alisema Omar
..
Kwa upande wake, Sheikh Khamis Mataka, ambaye alisema waraka huo ambao uliandaliwa kwa siri hautendi haki, na kwamba unapaswa kufutwa na serikali ili uandaliwe waraka unaozihusu dini zote.
Ukiangalia sura ya mkataba una mapungufu makubwa sana kwani unatoa upendeleo wa upande mmoja kwa kuwapa fursa ya kufaidika na kutafutiwa pesa na serikali kwa ajili ya taasisi zao za kielimu na kiafya na kutenga nafasi za elimu kwa watumishi wa taasisi hizo kwa upendeleo, alisema.
Alisema anashangazwa na hoja kwamba uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi usuhusishwe na fedha za serikali wakati mahakama hiyo itakuwa inalenga kusaidia serikali kupunguza mzigo katika mahakama zake
.
Habari kamili angalia raia Mwema Uk wa Pili.
Yeyote mwana-JF mwenye kuwa na story hii kikamilifu aiweke hapa pamoja na waraka wenyewe.