Ninajua wewe ni mwepesi wa hoja na una mihemko ya ksiasa. Kwa taarifa yako serekali ndio inafaidika sana na MoU kuliko hata hilo kanisa linavyofaidika. Hiki kitisho ulichosema ni kweli kinaweza kutumika, kwani hata kwa Kakobe tumeona hiyo hali. Lakini kwa haraka haraka hata serekali ikifuata huu utashi wako wajiandae na matokeo yake. Nilichogundua serekali hii inafanya baadhi ya mambo bila kupima matokeo yake, na hili ndio linaitesa serekali hii ya awamu ya tano hadi dakika hii.
Nitakupa mifano michache. Wakati awamu hii imeingia madarakani ilikuwa kama Tanzania kashuka malaika, mbwembwe zilikuwa nyingi, kila siku ikawa taarifa mubashara kuhusu majipu na miradi ya maendeleo. Hata nyie wapiga debe mkawa mnashambulia ile mbaya. Saa hii ili mubashara zinazidi kukata pumzi, tukiwaambia mlete updates za ujenzi wa SGR tunapoteana, tukiwaambia mlete updates za viwanda mnaishia kuleta vihoja. Jaribu kuangalia mnaoitetea hii awamu toka mwezi uliopita ni lini mmeanzisha mada za viwanda, SGR, au mradi wowote mkubwa wa maendeleo. Nyuzi zenu sasa hivi zimegeuka ni hila dhidi ya watu walioamua kutetea demokrasia, vitisho, kejeli na kiburi cha madaraka. Kwa ufupi hamna jipya. Tulitarajia wangalau mngeleta mada hapa jukwaani kuhusu matokeo baada ya sheria mpya za madini