Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

cover.jpg

quote_icon.png
By Dr.W.Slaa

Wana JF,

Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika
. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

1)
Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2)
Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili :
a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii,
b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.
Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando).

Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo.
Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.

thanks Dr! no more noise about MOU!
 
Mali zipi wewe mkoloni mweusi? ebu tuonyeshe shule iliyojengwa kwa nguvu za wakristo serikali ikapora.

Fikiria shule yoyote iliyotaifishwa (au kuwahi kutaifishwa na baadae kurudishwa kwa kanisa -- mf. Forodhani Sec.) na Serikali, utapa jibu.
 
Dr slaa na urais ni mbingu na ardhi take my words

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
tofautisha ukoloni(serikali)na wamisionari..usitake kupotosha,lini wakoloni walijenga makanisa?
Wamisionari ndio waliotumwa kuja kuuanzisha ukoloni na kuliibia bara la Afrika.Dini ilitumika kama kigezo tu lakini lengo kubwa lilikuwa ni kutawala na kuiba rasilimali.
 
Dr umetoa historia lakin hata Mwl Nyerere alikuwa na sababu zake za msingi kabisa kuanzisha AZIMIO LA ARUSHA. lakin kwa sasa hakuna tena nafasi ya kuendelea kuwa na Azimio hilo.

Kwa upande wangu Dr nakushauri kwa wakti huo kulikuwa na kila sababu kama ulivyobainisha. Sasa nikuulize je Sababu hizo mpaka leo zipo? Je kwanini Serikali yenu isijenge za Kwake yenyewe kuepukana na hizo za Kukodi kwa kanisa? Je unajua Kanisa wanachukua kiasi gani kutoka Serikalini kila mwaka?

Mkuu Barubaru,

Hebe funguka kidogo kuwafahamisha pesa wanazopewa kanisa na serikali.
 
Last edited by a moderator:
Mimi labda sijaelewa Slaa anatolea ufafanuzi kama msemaji wa kanisa au kiongozi wa chadema.Babu mbona unatuchanganya uko upande upi
unachotakiwa kujua ni kwamba, Slaa anawaelewesha wasiotaka kujua kwa vile yeye anajua zaidi kuliko mnavyoimanishwa wengine. sasa hayo ya usemaji wa kanisa yametoka wapi...?
 
You are missing the point. Huwezi kutuambia kwamba wakristo wana elimu sana kwa vile waliumbwa hivyo! Ni set up tu ambayo serikali kwa kushirikiana na makanisa waliamua kufanya makusudi kwa misingi ya kibaguzi. Hili lazima lijadiliwe katika national level kama ambavyo tuanjadili ufisadi mwingine.
huelewi kiswahili bro?cjasema wakristu waliumbwa kuwa na elimu nilichosema wewe na wazee wako wenye mawazo ya kukataa kusoma shule za kanisa ndo wanaorudisha nyuma maendeleo ya waislamu...
 
Wamisionari ndio waliotumwa kuja kuuanzisha ukoloni na kuliibia bara la Afrika.Dini ilitumika kama kigezo tu lakini lengo kubwa lilikuwa ni kutawala na kuiba rasilimali.

Na Warabu je? wao shida yao ilikuwa ni watumwa tena kwa kuwafunga minyororo, tena wana roho mbaya hata shule na hospital mnazotolea povu hawakuwajengea.
 
huu ni mtazamo tu,..
 
cover.jpg

quote_icon.png
By Dr.W.Slaa

Wana JF,

Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika
. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

1)
Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2)
Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili :
a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii,
b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.
Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando).

Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo.
Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.

Sasa mbona Dr amesahau kuelezea ilikuwaje mpaka serikali inakuwa inachota hazina fedha na kuyapatia makanisa peke yake? hiyo moja ama pili nasema ivi kwanini suala hilo halikupita bungeni? Mwisho ningepend kuchangia kuwa kama kweli Dr mlikuwa na nia safi isiyo ya kibaguzi kwa jamii nyingine na mkaona kwa kipindi kile kuwa yale yalikuwa mawazo mazuri je kwa sasa kutokana na hali ya jamii ilivyo na malalamiko yaliyopo ktk jamii mliojikita kuitenga mnaishauri vipi serikali juu ya kuuvunja huo mkataba? au ili kuweka usawa ktk lasilimali za nchi the same mkataba mnauotumia kuchotea pesa za watanzania wote utumike kwa jamii nyingine?
 
we mweh* nini?reje swali lako la awali kwangu linajibu swali lako hili la kipuuzi!!!!!!!!

Umetaja Forodhani,ndio maana ninakuuliza tena ilijengwa lini na nani? ninauliza ili uthibishe kuwa ni sehemu ya mali ya wakristo kwa maana walijenga na si kujengewa na wakoloni wezi waliotawala Tanganyika na dini ikitumika kama daraja.
 
Na Warabu je? wao shida yao ilikuwa ni watumwa tena kwa kuwafunga minyororo, tena wana roho mbaya hata shule na hospital mnazotolea povu hawakuwajengea.

pole sana kaka inaonekana historia yak ni ile ya sisi binadamu tumetokana na manyani. sikushangai sana kwa mawazo yako. Muulize mwna historia yeyote unayemuamini wewe kuwa je katika picha za watumwa kuna picha hata moja ambayo ni ya kupigwa?)I mean photog). ukimuuliza aliyebobea kusoma na kufuatilia isue ya watumwa kwenye vitabu vya historia atakuambia kuwa picha zote za waarabu ni za kuchorwa yaani ni taswira iliyotengenezwa na watu ili kuwapaka matope waarabu, ama picha za watumwa zinazoonesha wazungu utazikuta ni za kupigwa (photog). Ndugu yangu nakushauri fatilia juu ya hili ili uone mwenyewe.
 
Sasa mbona Dr amesahau kuelezea ilikuwaje mpaka serikali inakuwa inachota hazina fedha na kuyapatia makanisa peke yake? hiyo moja ama pili nasema ivi kwanini suala hilo halikupita bungeni? Mwisho ningepend kuchangia kuwa kama kweli Dr mlikuwa na nia safi isiyo ya kibaguzi kwa jamii nyingine na mkaona kwa kipindi kile kuwa yale yalikuwa mawazo mazuri je kwa sasa kutokana na hali ya jamii ilivyo na malalamiko yaliyopo ktk jamii mliojikita kuitenga mnaishauri vipi serikali juu ya kuuvunja huo mkataba? au ili kuweka usawa ktk lasilimali za nchi the same mkataba mnauotumia kuchotea pesa za watanzania wote utumike kwa jamii nyingine?

Mkuu kwani utaifishaji ulipita Bungeni? Then lasilimali nadhani msimamo wako ungeuelekeza kwenye gesi,dhahabu,pembe za ndovu zinazoibiwa kila kukicha kuliko kupingana na MoU ambayo inabaki kuwa na manufaa kwa Watanzania wote pasipo kubagua.
 
Back
Top Bottom