Ndi nkafu kikolo
 
Vote of confidence ni ubaguzi tu wa wachache. Hao marais wanaomteua awasaidie wanaujua uwezo wake kuliko sisi tunaotoa maoni tukisubiri tukio litokee kwanza.
 
Kinachoongelewa kinaweza kupambwa kwa lugha nzuri sana lakini ni ubaguzi unaofichwa kwa maneno matamu.

Vipi huyo Mbarawa kama angekuwa ni mtendaji mzuri katika hizo wizara, hizo fikra za kibaguzi zingezaliwa?, kuna mtu angekumbuka kuwa ni mzenji?.

Tutatue matatizo yetu bila ya kuitazama asili ya mtu. Ukibagua mtu leo ujiandae kesho kukabiliana na ubaguzi huo huo.
 
Akili zile zile zilizokemewa na Mwalimu Nyerere, akili za chuki dhidi ya wazanzibari. Tunasahau kuwa wakiondoka hao wazenji adui mpya wa kubaguliwa atakuwa ni wa kabila la jirani yako na jirani yangu.
 
..Katiba ndio iliyotenga yapi ya muungano, yapi ya Tanganyika, na yapi ya Zanzibar.

..Sasa labda useme Katiba ni ya kibaguzi. Lakini Wale tunaosisitiza sheria ifuatwe hatustahili lawama.
Katiba ni maandishi tu yanayofuatwa, tutumie na busara na hekima zetu katika kutafuta suluhisho.

JPM angeendelea kuwa hai mpaka baada ya 2025 hakuna mtu au taasisi ambayo ingeongelea suala la uzanzibari na utanganyika.

Kuna siasa za wivu zinazojificha katika huu msukumo wa chuki dhidi ya wazenji. Kuna watu wanaona kama vile wamenyang'anywa tonge mdomoni, ghafla tu mambo yote yamebadilika na zile fursa walizozizoea zimewakimbia.

Wanacheka mbele ya watu lakini mioyoni wanafuta machozi.
 
Akili zile zile zilizokemewa na Mwalimu Nyerere, akili za chuki dhidi ya wazanzibari. Tunasahau kuwa wakiondoka hao wazenji adui mpya wa kubaguliwa atakuwa ni wa kabila la jirani yako na jirani yangu.
Uzanzibar siyo kinga ya kufanyia uhalifu
 

..huwezi kuvunja katiba na sheria kwa kisingizio cha kutumia busara na hekima.

..katiba imeetenganisha mambo ya Tanganyika, Zanzibar, na muungano.

..Ni lazima tuyazingatie, na kama yanatukera suluhisho ni kwenda kwenye katiba ns kuyabadilisha, na si vinginevyo.

..chuki, ubaguzi, wizi, ukatili, na tabia nyingine za wanadamu, zote hizo zinapaswa kudhibitiwa na sheria zetu.
 
Wanaowachukua mawaziri kutoka huko Zenji wanatazama maslahi mapana ya nchi na wanaweza kuwa na uchungu na nchi hii kuliko mimi na wewe.
 
Wanaowachukua mawaziri kutoka huko Zenji wanatazama maslahi mapana ya nchi na wanaweza kuwa na uchungu na nchi hii kuliko mimi na wewe.

..inawezekana.

..shilingi ina pande mbili.

..hivyo wanaweza kuwa wamefanya kwa kuzingatia maslahi binafsi.

..again, huwezi kukiuka katiba na sheria, kwa madai kwamba unatazama maslahi mapana au una uchungu na nchi.
 
..inawezekana.

..shilingi ina pande mbili.

..hivyo wanaweza kuwa wamefanya kwa kuzingatia maslahi binafsi.

..again, huwezi kukiuka katiba na sheria, kwa madai kwamba unatazama maslahi mapana au una uchungu na nchi.
Katiba na sheria ni katika awamu ya sita inaonekana kuwa na umuhimu kwa sababu baadhi ya watu wa bara tunaishi na hasira mioyoni!.

Awamu ya tano na ya nne zilizoongozwa na watu wa bara hizi sheria na kanuni zilikuwepo, ila kwa makusudi tukaamua kuzifungia makabatini kama vile hazituhusu.
 

..tupinge uvunjifu wa Katiba na sheria bila kumuangalia mtu usoni.

..Mtanganyika akivunja Katiba akemewe na kuzomewa.

..Mzanzibari akivunja katiba na sheria naye akemewe na kuzomewa.

..Hatupaswi kuwa na muhali kwa wavunja katiba na sheria.
 
..tupinge uvunjifu wa Katiba na sheria bila kumuangalia mtu usoni.

..Mtanganyika akivunja Katiba akemewe na kuzomewa.

..Mzanzibari akivunja katiba na sheria naye akemewe na kuzomewa.

..Hatupaswi kuwa na muhali kwa wavunja katiba na sheria.
Huwezi kukiacha kipaji kimoja kipotee eti kwa kuogopa kuvunja katiba. Hizi ni sheria tu zinazoandikwa na sisi binadamu na siku zote zinaweza kuwekwa pembeni kulingana na mahitaji ya muda.

Charles Hillary yupo ikulu ya Zanzibar kwa kubebwa na uzoefu wake wa miaka 40 wa uandishi wa habari.

Mbarawa yupo katika baraza la mawaziri kwa elimu yake ya uhandisi na uwezo wake wa kazi.
 

..mambo hayaendi hivyo.

..kama kifungu cha katiba au sheria kinasababisha mkwamo fulani hatua sahihi ni kukibadilisha.

..Huwezi kusema Charles Hillary ana kipaji cha utangazaji hivyo asifuate sheria.

..Kila Mtanganyika na Mzanzibari anapaswa kufuata sheria.
 
napata wasiwasi kama hao waliopitisha walipata mafunzo ya JKTkuwafanya wawe wazalendo
 
Acheni kupotosha watu, Zanzibar ina utawala wake mambo yake hujadiliwa ndani ya baraza la wawakilishi, wana wizara yao ya mambo ya biashara sasa ni mwehu tu angetegemea bandari za Zanzibar zikajadiliwa ndani ya bunge letu. Siku wakiamua ziendeshwe kwa ushirikiano na mdau kutoka nje ni kimpango wao
 
Hii nchi i a viongozi wa hovyo sana, tusubiri baada ya hapo kifuatacho ni JK International Airport au KIA, badae sana SGR. n.k

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
mtabaki na mauwongo yenu hayo lakini mama anapiga kazi. Ni lini na kwa nani ATCL, TTCL, TRC zimebinafsishwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…