Mkataba wa kuendesha Bandari za Tanzania wa DP WORLD ya Dubai hautazihusu Bandari za Zanzibar
Wakati mwingine siasa ni kama mwanamke Malaya!

Ili ampate mwanaume aliyemwacha kwa kumfumaniwa na mwanaume mwingine, hutumia njia nyingi hata wapambe ili tu aendelee kuaminiwa!

Hapa, vijana wa ccm Zanzibar, kuna mdomo wa mbinafisishaji kuwahamasisha kudai na bandari za Zanzibar zingewekwa humo ili sisi tuwe wajinga zaidi ya vijana ccm Zanzibar!

Mbinu zote bado ni za kijinga kutwaminisha ubovu wa mkataba wa DO kuwa unafaa
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia soma > Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

---
MAONI YA WADAU
Bandari ya Zanzibar haina tija yoyote , haina muunganisho na nchi za barani Africa.
DPW hawaihitaji zanzibar kabisa.
 
Mwinyi hakuuza Lliondo? Kaandika kitabu akisikitika baada ya kutoa sadaka rasilimali za Tanganyika.

Huo ni wizi hata kule Zbar CAG kaonyesha

Ni hawa hawa Wanaodai mambo ya muungano yameongezwa na hawataki. Wanasema kuongeza mambo hayo kunawanyima fursa. Leo wanatumikia nafasi za mambo yale yale wasiyoyataka. Mbarawa na Shaka DC ni mifano tu. Huwezi kuwa na Tanganyika ya yote halafu Zanzibar yao.
Chuki zinazoenezwa na Wazanzibar ndizo chanzo , Watanganyika walikuwa kimya muda mrefu sana na kuonekana Wajinga. Hiyo Wizara si ya muungano, Mbarawa anasaini mikataba isiyomhusu, hatuna imani naye

Wazanzibar hawautaki. Othman Masoud Othman(OMO) juzi kasema muungano si '' Faradhi au Suna'' wanaweza kuvunja tu. Kila siku akina Jussa na OMO wapo majukwaani kuwaalani Watanganyika. Hakuna adui yao mkubwa zaidi ya Tanganyika. Tunawasikili tunawasoma. Tunawasikia tunawasoma .
Leo wakimbize gesi na mafuta kwao, halafu bandari za Tanganyika ni za wote! nope, ujinga huo utabaki na wachache wanaolamba asali

Hoja hapa ni kuwa Rais SSH yupo kikatiba. Huyu anaye negotiate na kusaini yupo kikatiba tu lakini anashughulikia jambo lisilo la muungano. Mwinyi aliuza Loliondo kwasababu hakuwa na uchungu na Tanganyika .
Kuvuja kwa document kunaonyesha kitu! fikiria

Waambie wazanzibar wanaoneza chuki. Mwambie Makamu wa Rais na Makamu wa ACT bwana OMO na akina Jussa waache chuki. Huwezi kuwa na chuki halali akisema mzanzibar, haramu akisema Mtanganyika

Waombe kura ya maoni, wakifanikiwa waondoke tu salama !

Ufanisi unaujua wewe, sisi tunaangalia rasilimali na tushaumwa na nyoka kupitia AH Mwinyi.
Pole sana kaka mkubwa.
 
Ubaguzi huo tumeanza sisi au wao.
Katika Mambo ,22 ya muungano, moja Ni la bandari. Hawa wazanzibari kwa makusudi kabisa wanauza bandari za Tanganyika na kuacha za Zanzibar. Kwa maana hiyo Sasa hivi Mambo ya muungano yatakua 21 badala ya 22.
Kwanza ujue hapo katiba pia imevunjwa.
Anyway, inahitaji upeo mkubwa na MTU anae ijua katiba ya nchi kuyaona haya Mambo.
Ushahidi wa tuhuma za kuuza bandari unao?, hii biashara ya DP World ilianza kufuatiliwa tangu enzi za JPM hayati.

Mbarawa na SSH ni watekelezaji tu wa sera za CCM. Mnaitaka roho ya Mbarawa, mngeanza kwanza na ile ya hayati JPM.

Wakati wa awamu yake mliufyata kimyaaa leo mnaanza kuchonga na kupiga makelele ya kinafiki.
 
Hii haimpi fursa 'kuuza nchi' . Kama kafanya hivyo alilipwa mshahara na ni makosa kwasababu hayakuwa mambo ya muungano. Tunasema sasa kwamba inatosha, tuheshimu maamuzi ya Wazanzibar wanaolalamika kuongezwa mambo ya muungano. Katika yasiyo ya muungano waondoke kama ambavyo hakuna Mtanganyika ndani ya SMZ. Unabisha nini wakati katiba inasema kuna ya muungano na yasiyo ya muungano.

Hatuna imani naye, tutasema. Ataendelea kuwepo pale lakini ajue watu hawana imani na yeye!
Amekuwa distractions katika mambo muhimu, akae pembeni kama Job Ndugai.
Hili si jambo la muungano, hatuna upungufu wa watu wenye uwezo na uchunguna Tanganyika.
Mbarawa ajiuzulu ili kuondoa mijadala hii, akae pembeni hili ni la Tanganyika na Wazanzibar wanasema hivyo

Wazanzibar hawataki kuitwa Watanzania leo unasema si ubaguzi huo. Yasiyo ya muungano wakae pembeni
Akae pembeni kama Job Ndugai!, kumbe wewe ni Sukuma Gang wale wale kina Luhaga Mpina. Mnaumia sana awamu hii.
 
Ushahidi wa tuhuma za kuuza bandari unao?, hii biashara ya DP World ilianza kufuatiliwa tangu enzi za JPM hayati.

Mbarawa na SSH ni watekelezaji tu wa sera za CCM. Mnaitaka roho ya Mbarawa, mngeanza kwanza na ile ya hayati JPM.

Wakati wa awamu yake mliufyata kimyaaa leo mnaanza kuchonga na kupiga makelele ya kinafiki.
Pamoja na ukorofi wake wote lakini Kwa miaka yake yote 5 JPM hakuthubutu kucheza na Mali zetu Kwa kushirikiana na watu wa nje. Tuliufyata Kwa sababu ni kweli pia kwamba Yale yote aliyokuwa anayafanya yalikuwa ni Kwa faida ya nchi. Sema ni wapi JPM alipandisha twiga wetu kupelekwa nje, ni wapi alipauza Kwa yeyote Toka ughaibuni. HAPAPO.
 
Hakuna anayeweza kucheza na mali zetu hata leo hii haya maneno ni matunda ya chuki za kisiasa zinazosambazwa na maadui wa SSH, haswa hawa wanaotaka nafasi ya urais 2025.

Hakuna anayeweza kuja na hoja yenye kueleweka yenye kuonyesha namna mali zetu zinavyoweza kuuzwa. Uwekezaji sio sawa na uuzaji.

Mmepandikiziwa chuki na mmeingia mazima katika hizi akili za kibaguzi. Unaweza hata kunionyesha picha ya Twiga wetu akipandishwa ndege zaidi ya kuwa ni maneno ya kimbea tu?.
 
Hizi ni Mali za Watanganyika, watu hawako tayari kuona zinagawiwa ovyo Kwa waarabu, walianza na Loliondo, Bandari za bara na baadaye hatujui kinachofuata. Haiwezi kuwa coincidence, Mwinyi Loliondo na huyu naye Bandari na pia kuhamisha watu wetu Loliondo. Niambie Mwalimu, Mkapa, JK na JPM Hawa hawakuhitaji kutuendeleza?
 
Akae pembeni kama Job Ndugai!, kumbe wewe ni Sukuma Gang wale wale kina Luhaga Mpina. Mnaumia sana awamu hii.
Akae pembeni kwa maana kwamba hakuna tatizo na umahiri wake. Ndugai alikaa pembeni akiwa Spika, seuse Mbarawa , waziri tu

Phillipo, chuki ya Wazanzibar wameipanda siku nyingi . Mlikuwa kimya mkidhani ni maua ya Waridi
Kuita Watanganyika wakoloni ni chuki iliyotitia
Mikutano ya hadhara kuwasumanga Watanganyika ni chuki liyo furuta
Kudharau katiba ya JMT ni chuki iliyokithiri

Leo Mbarawa kuambiwa wizara anayotumikia si ya muungano, ukweli, eti ni chuki !

Wazanzibar taratibu watavuna mbegu ya chuki, walidhani Watanganyika wamelala. Ukimya ilikuwa hisani na uungwana, sasa dude limeamka . Tunataka kura ya maoni Wazanzibar waamue hatma yao
Kama watahitaji muungano, uwe ule wa Mzee Warioba , Tanganyika ikiwa na mtetezi

Kwasasa hivi Tanganyika, inayoitwa Tanzania bara kwa mujibu wa katiba ya 1977 haina mtetezi
Ndiyo maana Wazanzibar wanakaa na kumaliza kero za muungano wenyewe, wanafuta bili za umeme ili mbeba mizigo wa Buguruni awalipie. Wanalipa pensheni wazee kwasababu hawajui gharama za taasisi za muungano. Sasa wanampango wa kulipa wahjumbe wa nyumba kumi! Kwa uchumi upi!
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia soma > Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

---
MAONI YA WADAU
Hii ni nchi ya kipumbavu sijawahi kuona. Ipo siku tutapigana vita ya wenywewe kwa wenyewe na kufanya genocide kama ilivyotokea Rwanda na Burundi. Hawa wapumbavu wataipeleka hii nchi jehanamu.
 
sasa mkataba sio wa miaka 100 ni miaka mingapi wengine wanasema mkataba wa milele au mpaka kiama
 
Tuliwaambia wamama sawa wanataka ila hawawezi. Tukaonekana tuna nongwa. Nyumba toka lini ikaendeshwa na mwanamke!
 
Hizi ni Mali za Watanganyika, watu hawako tayari kuona zinagawiwa ovyo Kwa waarabu, walianza na Loliondo, Bandari za bara na baadaye hatujui kinachofuata. Haiwezi kuwa coincidence, Mwinyi Loliondo na huyu naye Bandari na pia kuhamisha watu wetu Loliondo. Niambie Mwalimu, Mkapa, JK na JPM Hawa hawakuhitaji kutuendeleza?
Tanganyika kabla ya sitini na nne hivi sasa ni Tanzania. Kuuza wanyama ni biashara ya dunia nzima haijaanza na Loliondo na hataimalizika na eneo hilo, hao ni viumbe wanaozaliana na hata wasipouzwa zaidi ya kuona ufahari wa kuwa nao kipi cha ziada tulichonacho kutokana na uwepo wa wanyama hao!? yale yale ya roho za choyo.

SSH ni rais wa Tanzania yote anayoyafanya ni kwa kofia hiyo. Na Mungu ni fundi kweli kweli akaamua kutukumbusha kuwa zamu ya wazenji kuongoza TZ ilishafika kitambo kwa kumchukua kipenzi chetu JPM ili SSH aongoze nchi akiwa mzenji wa pili kufanya hivyo.

Ukikubaliana na upuuzi wa humu jukwaani utaamini kabisa kwamba nchi imeuzwa, ukikosa akili ya kujiuliza yale ya msingii utakubaliana na hoja hizi nyepesi.
 
Akae pembeni kwa maana kwamba hakuna tatizo na umahiri wake. Ndugai alikaa pembeni akiwa Spika, seuse Mbarawa , waziri tu

Phillipo, chuki ya Wazanzibar wameipanda siku nyingi . Mlikuwa kimya mkidhani ni maua ya Waridi
Kuita Watanganyika wakoloni ni chuki iliyotitia
Mikutano ya hadhara kuwasumanga Watanganyika ni chuki liyo furuta
Kudharau katiba ya JMT ni chuki iliyokithiri

Leo Mbarawa kuambiwa wizara anayotumikia si ya muungano, ukweli, eti ni chuki !

Wazanzibar taratibu watavuna mbegu ya chuki, walidhani Watanganyika wamelala. Ukimya ilikuwa hisani na uungwana, sasa dude limeamka . Tunataka kura ya maoni Wazanzibar waamue hatma yao
Kama watahitaji muungano, uwe ule wa Mzee Warioba , Tanganyika ikiwa na mtetezi

Kwasasa hivi Tanganyika, inayoitwa Tanzania bara kwa mujibu wa katiba ya 1977 haina mtetezi
Ndiyo maana Wazanzibar wanakaa na kumaliza kero za muungano wenyewe, wanafuta bili za umeme ili mbeba mizigo wa Buguruni awalipie. Wanalipa pensheni wazee kwasababu hawajui gharama za taasisi za muungano. Sasa wanampango wa kulipa wahjumbe wa nyumba kumi! Kwa uchumi upi!
Mtu aliyekomaa kabisa kichwani halipi visasi eti kwa sababu fulani na fulani walifanya hivi basi na sisi lazima tufanye vile.

Ni fikra zenye ukosefu wa ustaarabu ndani yake.
 
Back
Top Bottom