Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Sikupingi ila hiyo ni jeuri ya mtu ambaye ndiyo ameijua pesa jana. Yanga kwa ukaribu wake na CCM haina historia ya kuitunishia kifua Serikali. Kama Simba waliweza kufanya hivyo bila shida sioni Yanga atashindwaje.
Na kwa sababu hizo ndio maana hadi kesho Simba/Yanga hawana kombe la CAF hata la kunywea maji.
Mambo ya kuingiza ccm kwenye mpira wetu ndio kudumaa kunakuja.
 
Kama wanahusika kwanini walipendekeza timu ivae visit Tanzania? Kwanini wasingekomalia timu ivae hiyo hiyo sportpesa kifuani?
Ni kweli wagumu kuelewa au mnafanya makusudi? Mnasema Sportpesa hana kauli kwenye mashindano ya kimataifa, mlivyocheza na Al Hilal na African Club hayakuwa mashindano ya kimataifa yale?

Mnaona afadhali kuendeleza ubishi usio na maana kuliko kukubali ukweli ulio mbele yenu.
 
Na kwa sababu hizo ndio maana hadi kesho Simba/Yanga hawana kombe la CAF hata la kunywea maji.
Mambo ya kuingiza ccm kwenye mpira wetu ndio kudumaa kunakuja.
Ndiyo nchi yetu pendwa ya Tanzania. Kuziheshimu na kuzitukuza mamlaka ni jadi yetu kwa hiyo jeuri hiyo siitegemei kuiona kutoka kwa Yanga. Dewji alivyopotea uliona hata sisimizi ameingia mtaani kumtafuta?
 
Kweli upo serious unajumisha mapinduzi cup kwenye mashindano? usha wahi ona mashindano mchezaji anaweza cheza bila kusajiliwa? naomba unitajie qualifications za kucheza mapinduzi, upgrade your IQ please
Wachezaji kutosajiliwa ndio inapoteza maana ya mashindano?

Unaelewa maana ya mashindano?
 
Ni kweli wagumu kuelewa au mnafanya makusudi? Mnasema Sportpesa hana kauli kwenye mashindano ya kimataifa, mlivyocheza na Al Hilal na African Club hayakuwa mashindano ya kimataifa yale?

Mnaona afadhali kuendeleza ubishi usio na maana kuliko kukubali ukweli ulio mbele yenu.
Ungejibu kwanza swali nililokuuliza? Ndipo uulize swali lako ujibiwe
 
Sijajua unauelewa gani kwenye masuala ya masoko ila kwa uchache, uuzwaji wa jezi mpya zenye udhamini wa kampuni mpya unaweza kuathiri uvaaji wa jezi zenye nembo ya sportpesa mtaani. Wanunuzi na wavaaji wa jezi ni wale wale. Hilo ni moja tu.
Hata ingekuwa visit Tanzania si bado nayo ingeathiri maana Kuna watu hawaamini mambo ya betting walikuwa wametengwa
Nadhani hili suala linazungumzika ila ukweli ni kuwa kuendesha Simba na Yanga ambazo wanachama wake wanachangia kidogo sana unahitaji akili kupata vyanzo vya mapato.
Binafsi naona bado sana
 
Bonus ni kitu kidogo sana kwenye biashara au mkataba

Ni kitu ambacho kinatolewa kwa mapenzi kama motisha kuku encourage ili ufanye vizuri au hufanywa hivyo kama kivutio wengine waweze kuingia deal na hiyo kampuni

Bonus sio kitu cha lazima

Kwa upande mwingine ni kwamba SportPesa waliweza kusaini deal la mkataba na Yanga bila kuweka hizo bonus na bado wangeendelea kuhesabika kama wadhamini wakuu.

Na ndio maana ukiangalia katika mkataba waliokubaliana SportPesa na Yanga ilihusisha bonus ya ligi kuu na ASF, lakini hakukuwa na makubaliano yeyote ya maswala ya bonus kwenye mapinzduzi cup and still Yanga walivaa jezi yenye nembo ya SportPesa

Hiyo ni kwasababu

portPesa kanunua jezi, haijalishi ni mashindano gani Yanga anacheza lazima logo ya SportPesa iwekwe kiifuani, vinginevyo ni mpaka SportPesa mwenyewe aridhie

Mkuu, kwenye mkataba EVERY WORD COUNTS…!!!
Kila neno lina maaana KUBWA SANA kwani linaweza kufanya mkataba ukavunjika kijinga sana au ukasimama vizuri sana
 
Ni kweli wagumu kuelewa au mnafanya makusudi? Mnasema Sportpesa hana kauli kwenye mashindano ya kimataifa, mlivyocheza na Al Hilal na African Club hayakuwa mashindano ya kimataifa yale?

Mnaona afadhali kuendeleza ubishi usio na maana kuliko kukubali ukweli ulio mbele yenu.
Mkuu hivi unaelewa kwanini walitumia jezi za Sportpesa kwenye preliminary stage na sasa hawawezi kutumia?
 
Wewe itakuwa umebadili username. Kuna jamaa anaongeaga kama wewe ni mbishi kama shida zangu.

Kuna mnaosema Sportpesa hana mamlaka na Yanga kwenye mashindano ya CAF, mnakumbushwa mbona Yanga alikuwa wanavaa nembo yao kwenye hatua za awali, unarudi kuongelea sheria za hatua za makundi kama vile hakuna anayejua kuhusu sheria za CAF. Swali ni kama Sportpesa hausiki mashindano ya kimataifa kwenye mkataba na Yanga, mbona walivaa nembo yao hapo kabla?

Acha ubishi dogo.
1 Kwanza hilo swala la kubadili username utakuwa una nongwa zako tu. Tofautisha ubishi na ufafanuzi
2. Mwemye uelewa na jambo analeta hoja sio mihemko.
3. Yawezekan nikawa baba yako (kiumri) maana mkikaa nyuma ya keyboard ammakosa adabu.
4. Angalia profile yangu then uone mimi na ww nani dogo.
 
Duuh Ina maana hujui kuwa Hair na GSM ni kampuni mbili tofauti?

Hair ilishawahi kutaka kuweka mzigo man u lakini Dili liligoma tu sasa unaposema ni GSM hapo unakua unakosea
Mwenzio kaandika kampuni gani na wewe unaandika kampuni gani? Unavoambiwa pikipiki boxer ni Mo unazani anazalisha yeye? Dealer wa boxer tz nzima ni Mo
 
Wewe itakuwa umebadili username. Kuna jamaa anaongeaga kama wewe ni mbishi kama shida zangu.

Kuna mnaosema Sportpesa hana mamlaka na Yanga kwenye mashindano ya CAF, mnakumbushwa mbona Yanga alikuwa wanavaa nembo yao kwenye hatua za awali, unarudi kuongelea sheria za hatua za makundi kama vile hakuna anayejua kuhusu sheria za CAF. Swali ni kama Sportpesa hausiki mashindano ya kimataifa kwenye mkataba na Yanga, mbona walivaa nembo yao hapo kabla?

Acha ubishi dogo.
Huna uelewa wowote na hilo ulisemalo.

Nionyeshe wapi nimesema sport pesa hana mamlaka na Yanga?. Tumia akili kusoma na kuelewa kwanza bandiko la mtu kuliko kukurupuka kujibu usichokielewa.

MSAADA WAKO
Hatua za awali kila club inajitegemea kwa kila kitu ndio maana wanaenda na jezi zao za ligi.

Kuanzia makundi CAF inatoa pesa kwa clubs. Ili kufanya hivyo inatafuta mdhamini. Kama mdhamini wa club anafanya biashara sawa na wa caf ndipo sheria za caf zinaitaka club hiyo kutovaa jez za mdhamini huyo.

PUNGUZA NONGWA, NI SHIDA ZAKO TU
 
Back
Top Bottom