Mke adai talaka na kugawana mali kwa kumzuia kutoenda msibani Hadi nitakapo rudi, nimemwambia chukua Kila kitu

Mke adai talaka na kugawana mali kwa kumzuia kutoenda msibani Hadi nitakapo rudi, nimemwambia chukua Kila kitu

Hapo umezingua!
Kuna situation ubabe inabidi uwekwe kando.
Kwamfano wewe ndo ungekuwa umefiwa na mkeo yupo mbali je, mngefika huko?

Acha ubabe mkuu mambo mengine humalizwa kwa maongezi tu.
Kauli ya mke wake haikuwa ya kiungwana.

"Naenda, nikirudi tuachane na tugawane mali"

KAULI GANI HIYO?
Mleta uzi ana akili nyingi sana. Baada ya kujua mkewe anatishia mali ndio kaamua kumpa vyoooote hata hela za bank. Ili ajue kuwa mwanaume hayuko after mali.

Mleta uzi kama ni kweli WEWE KIDUME.
 
Kichwa mchumba box kbs maana hata insurance, alikuwa haangalii. Hivi mtu akisema card feki ina maana jina la aliyenunua.
Maana ile card ina jina, type, colour,And ...... so inakuwaje?
nd hivo sas jamaa alitengenez fake isiyokuw na full info.....kujihami pia dem hajawah kumilik gar na hatimilik ya gar hajawah ona ( alikuw na mihemko tu )
 
Hapo umezingua!
Kuna situation ubabe inabidi uwekwe kando.
Kwamfano wewe ndo ungekuwa umefiwa na mkeo yupo mbali je, mngefika huko?

Acha ubabe mkuu mambo mengine humalizwa kwa maongezi tu.
Kauli ya mke wake haikuwa ya kiungwana.
"Naenda, nikirudi tuachane na tugawane mali"

KAULI GANI HIYO?
Mleta uzi ana akili nyingi sana. Baada ya kujua mkewe anatishia mali ndio kaamua kumpa vyoooote hata hela za bank. Ili ajue kuwa mwanaume hayuko after mali.

Mleta uzi kama ni kweli WEWE KIDUME.
Hujawahi kugombana na mkeo akatamka maneno tu kwa hasira au wewe ukatamka tu? Huo ni msiba lazima umemgusa na ndio akaongea kwa ukali! Unafikiri hayo maongezi ndio Yameishia hapo kwenye huo ujumbe? Huwezi jua wamevutana muda gani mpaka kaongea vile! Mtu una watoto wa tatu unataka uachike ili ukafanye nini? Mbona hata kama huna ndoa hapa unatumia akili kufikiria!
Usitetee ujinga.

Ameomba akirudi waachane na wagawane mali pasu kwa pasu.
Kauli nzito sana hiyo. Na inaonyesha ipo kichwani mwake siku nyingi. Ameomba nusu ya mali, mwanauume kaamua amuachie vyoooooote. Kuna ubaya gani?
 
Hapa kajitumisha sms kujirudi,maana nilikua nimemtumia sms ya kumsisitiza achukua Kila asiache chochote
Kaeni kikao chenu wawili, serious cha utulivu. Muwekee misingi yako awe anaishi katika hiyo misingi. Tayari ishakuwa siyo jambo jema sana kuachana mna watoto watatu na kuna kugawana mali hapo jambo ambalo ni hasara. Mfanye aishi katika misimamo yako, asikupande kichwani.
 
“kumzuia” tatizo liko kwenye lugha mnazotumia sasa sijui kama pia zinaendana na matendo yenu, hauwezi kumzuia mtu mzima, unaweza kumzuia mtoto mdogo na labda mtumwa unayemliki sasa mke kwa from a Christian perspective atleast siyo mtoto wala mtumwa wako …
Naomba tafsiri ya UTII....
 
Habar wakuu nima mke na watoto 3Niko safarini kikazi,gafla ikatokea dharura nyumbani mke Wangu kafiwa na bibi yake mkoa mwingine akanitaarifa,nikamsihi asubiri ndani ya siku3 ntakua nimerud ila watoto wawe salama,

Mke akagoma akasema hawezi akasubiria Hadi nije haiwezekani lazma ataenda na kama akasema sitaki basi atakaporudi tuachene na tugawane mali kila mtu aendelee na maisha yake,

Nikamwambia kama umenikaidi amri yangu we chukua Kila kitu safisha nyumba nzima usiacha kitu chochote,chukua hati zote za viwanja usiache hata kimoja nkaenda mbali Zaid nikamuonesha nakadi ya bank ilipo inakiasi Cha pesa kidogo kama 10m nikampa namba ya Siri akatoe nazo aende nazo
duh
au mlikua mnategeana
kila mtu alikua anasubiri mwenzie aanze
 
mkuu nyuzi zako zimekuwa zikionyesha unapitia mengi sana magumu pole sana


Dah...
 
Malizia uzi mzee

Unamuachaje mtu kizembe ivyo , unampekekea mwanaume mwenzako utamu na mtaji juu acha ufala

Kama ni msibani angeenda tu ungemsihi aende na watoto kwani msibani wanaua watoto, usalama gani unautaka kwa watoto

Mimi ndugu zangu wajinga wajinga nawapigaga vibao kwa maamuzi yao ya kijinga…

Mjinga wew
 
Gentleman,
ukiona mke wako anakuonyesha kiburi hivyo, ujue nyuma ya hicho kiburi kuna mchepuko unakipa nguvu na jeuri zaidi.

In fact,
umetumia surrender tactic vizuri sana gentleman, na umempa ushindi utakaomtikisa kisaikolojia na kujitafakari zaidi juu ya jeuri hiyo ya kulazimisha kwenda kuzika mkoani hali yakua msiba hua hauishi, anaweza kwenda kuhani hata mwaka ujao.

Hivi kweli kufiwa na bibi tu , kunaweza kumsababisha afosi kuiacha nyumba yake na watoto wadogo na kulazimisha kwenda kuzika tu? Hakuna kitu behind the scene kinachomfosi?

No, kuna kitu kingine gentleman ,amepanga kwenda kufanya huko kwa kisingizio cha kwenda kuzika ndio maana analazimisha hivyo.

Na,
Gentleman,
hebu jaribu kama vile nawe unataka kuambatana nae kumsindikiza kwenda huko mkoani mazishini kumzika huyo bibi yake, halafu utagundua kitu, anaweza kuahirisha, kwasababu utakua tayari umeinterfear mipango yake ovu alikua ameikusudia katika ipindi hicho cha msiba.

Pole sana gentleman na hongera kwa ujasiri,
Kumbuka,
wanamke mjinga anaivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Tuishi nao kwa akili 🐒
Mkuu nilijua unaleta masiara kwenye siasa tu.

Kumbe hadi kwenye ndoa 😂
 
Hapo mwanamke kusema muachane sio hiyo sababu ya kwenda msibani tu

Kwasababu hata kama umekaataa angeweza kulazimisha kwenda bila kusema talaka

na baadae mngejadili issue ya utii kwa mkeo kwa nini amekukaidi
Mpka hapo mkeo ana kinyongo na wewe ila hujui anakutafutia sababu

Na kwanini wewe umkataze kwenda sasa?
Yaan mkeo unamuona ni hopeless kiasi hawezi kuhakikisha usalama wa watoto?

Wewe unaonekana una gubu hutaki mke wako akutii na kukuheshimu unataka kuogopwa na kutetemekewa
Issue inayo sound kama utumwa

Mpka hapo mlipo fika hakuna mapenzi wala heshima
Achaneni kwa amani tu
 
Kwakua umeshindwa kujibu swali langu naomba tuishie hapa.

sawa haina shida, ila take home message kwako, jifunze kuheshimu binadamu wengine, kila mtu mzima na mwanamke ni mtu mzima ana mahitaji yake pia kama wewe ambavyo ulivyo na yako na sidhani kama ungekubali mtu yoyote “ akuzuie” bali ungependa mtu akuheshimu na kuongea na wewe kwa kujadili lkn siyo “kukuzuia”, hilo la kuzuia ni wewe mwenyewe ndiyo unaweza kufanya kujizuia …
 
Back
Top Bottom