Mkoa wa Pwani watoa Mawaziri watano kwenye baraza jipya; ni bahati mbaya au ndiyo tuseme sasa zamu ya watu wa Pwani?

Bora sisi Bukoba tunao Watatu
Kimataifa
Tamisemi
Nishati
 
Jaman c mnasema Pwani hakuna wasomi kaz yao kusoma din tu????ngoja tuwaoneshe na sisi tumo
Pwani oyeee

1. Dr. Jaffo - kisarawe
2. Mchengelwa - Rufiji
3. Ridhiwani - Chalinze
4. Ulega - Mkuranga
5.kipanga - Mafia

Hivi siku hizi uongozi wa nchi hakuna regional representation?

Rais Samia hapa washauri wamekubambika.
 
Onyesha basi hiyo National representation imekosekana wapi? Tuna mikoa 31, hebu tuonyeshe mapungufu yapo wapi?

Mbona kama umepanic sana,yani hujibu hoja ya [mention]masopakyindi [/mention] unaanza kumletea hadithi za yeye kuwa legendary tena,au ndiyo nyinyi wa Pwani mmeguswa kidogo tu mnacharuka kama mmetiwa ndimu.
 
Enzi zile sasa
1. Bitteko-home kabisa
2. Kalemani- Wa sebuleni
3. Mabula- wa nyumbani
Achana na hao wa Shinyanga sijataka kuwajumuisha.
Uongozi wa nchi toka Awamu ya 5 umeanza kukosa NATIONAL CHARACTER.
Tunaanza kuona uongozi kuwa zamu ya makundi ya watu wenye mtandao wao.
 
Kati yao wanashikilia nguvu kubwa kiasi gani ya kisiasa?

Wana maamuzi gani yanayoweza kutafsriwa kama upendeleo kwa mkoa wanaotoka dhidi ya mikoa mingine?

Kuna uzoefu wowote unaoonesha kuwa uwiano wa mawaziri na manaibu kimikoa una tija kwenye maendeleo ya mikoa hapo nchini?
 
Hebu tupe idadi ya kanda ya ziwa
Kanda ya kaskazini.
Kanda ya nyanda za juu kusini...

Hizi siasa za kifala, watoto wetu watakuja kutudharau sana
Kanda ya kaskazini bila Tanga; kuna waziri mmoja na manaibu watatu. Hiyo ni mikoa mitatu ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
 
Pwani haina airport, ngoja tuone nguvu zao
 
Mtamsingizia mengi ila yeye kama maji ni muhimu kwa uhai wa kila kiishicho.
Leo mtaimba kila aina ya nyimbo ila hazina stepu, akiweka mzanzibar semeni anachagua wa zanzibar, muisilamu semeni ana udini, na leo wa pwani mnahaki ya kusema kwa nn amewateua wa pwani. Ila uzuri tunajua hata asingeteua wa pwani Mngesema kwa nini hateui wa pwani. Mnarudia majalada yale yale kuyasoma endeleeni tu ila yeye anajenga nchi hivyo
 
Tuna mikoa 26!na wizara zaidi ya 30,na nafasi manaibu zaidi ya 30,kila mkoa ungeweza kuwa na nafasi za uwaziri kuanzia mbili.mama kachemka
 
Hebu tupe idadi ya kanda ya ziwa
Kanda ya kaskazini.
Kanda ya nyanda za juu kusini...

Hizi siasa za kifala, watoto wetu watakuja kutudharau sana
Wakati mwingine ni vyema ukaficha upuuzi wako! Mtu anazungumzia mkoa wewe unauliza Kanda! Tukueleweje?
 
Tuna mikoa 26!na wizara zaidi ya 30,na nafasi manaibu zaidi ya 30,kila mkoa ungeweza kuwa na nafasi za uwaziri kuanzia mbili.mama kachemka
Mikoa ya Rukwa na Morogoro haijapata waziri wala naibu hata mmoja. Kama yupo naomba nisahihishwe.
Unachukuaje mawaziri 3 kutoka mkoa wa Tanga, mawaziri na manaibu kutoka majimbo karibia yote ya mkoa wa Pwani
Lkn mikoa ya Morogoro na Rukwa haina hata naibu waziri?
Hilo baraza lina sura ya kitaifa kweli?
 
Jenister is the next PM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…