TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Ile barabara wala sio finyu. Labda dereva kuchoka maana Tanzania ukiwa chini ya amri ya MTU cha moto unakiona
Kwani Pro Ngowi alivyopata ajali kwani Kilimanjaro kulikua hakuna Airport au Professor Ngowi alikua hana pesa za kupanda ndege?
 
Looh, ajali mbaya sana hii Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu! Gissima alikuwa anajua kuchapa kazi, nilifanya naye kazi kwa ukaribu kabisa kipindi akiwa mkurugenzi wa ufundi pale REA kabla hajawa DG wa REA!
Looh, ajali mbaya sana hii Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu! Gissima alikuwa anajua kuchapa kazi, nilifanya naye kazi kwa ukaribu kabisa kipindi akiwa mkurugenzi wa ufundi pale REA kabla hajawa DG wa REA!
Pole sana mhandisi msomi.

MUNGU amrehemu
 
Gari za kijapani huwa ni nyepesi sana, bodi inanyambuka kama karatasi, nyepesi huwa zinapea na kukosa balance ukiwa high speed.
Defensive driving ni muhimu sana kwenye haya magari na barabara zetu pia.
 
Mkuu kutembea na gari kuna raha yake, Mbona Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani utakuta wana safari kwa Gari kuto Dar mpaka Iringana wengine mpaka Kigoma, kusafiri kwa Gari binafsi kuna raha yake.
Angalia kampani yao ,wengi tunapenda road trip ila kuharakisha kazi zaidi bora ya ndege.

Mwongozo wa malipo ya posho kwa wakuu kuanzia wakuu wa idara na ndege ,huyo kwa cheo chake ni daraja la juu kabisa hata kukodi kama kuna kazi ya umuhimu anaweza.
 
Je ni kweli alikuwa anaenda kuchukua fomu ya kugombea jimbo la bunda?
Ninavyofahamu kama sijakosea lakini, Gissima Nyamo-Hanga alikuwa kati ya Mzanaki au Mngoreme! Labda kama alikuwa anaenda kuchukua fomu ya jimbo la Serengeti au Butiama! Lakini hiyo ajali itakuwa imesababishwa na uzembe wa madereva wengine wa serikali kama kawaida yao! Mwendo kasi bila kuchukua tahadhari! Ukiangalia jinsi gari ilivyoharibika na jinsi lile lori lilivyohamishwa barabarani obvious ni mwendo kasi!
 
Wewe unajidai unaijua Serikali na Watumishi wake, hivi kwa akili yako MD wa TANESCO perdiem ya siku mbili ni issue kweli hadi imuweke barabarani siku mbili? 🤣🤣🤣

Jamaa alimaliza kikao Dom akaona aunganishe Musoma.
 
This is not true cheif

Level ya nyamohanga siyo ya kutegemea tena per diem

I feel bad jinsi mnavyochukulia watu poa

Huyu BWANA kamaliza meeting, kaanza safari usiku ilo awahi jumapili kwao na Jumatatu awe amerudi…. Hakuna muda wa kupumzika

Tuwaonee huruma hawa watu
 
Poleni sana wafiwa, watu wazuri hawadumu,
Yule wa Tume naye asome alama za Nyakati, Aacha kuwakandamiza Wapinzani,
 
Nchi inatakiwa iwe na reli, safari ndefu kama hizo watu wasafiri kwa treni, ila bado ni jambo la ajabu kwa CEO wa TANESCO kusafiri umbali mrefu hivyo kwa gari.
Sidhani kama ni jambo la ajabu hasa kama mtu umewahi ku-experince maisha ya mataifa mengine. Ndege nazo zinachosha kuna wakati utataka kuangalia mazingira ya chini. Kwa watu wengi, kusafiri kwa barabara nako ni burudani na kujifunza. Sema watanzania huwa tuna tabia ya kukwepa kushughulika na vyanzo vya matatizo na badala yake tunayafukia. Kama ni hatari au siyo vizuri kusafiri umbali mrefu wa gari, watu wengine i mbona wanasafiri? Wao wana miili ya vyuma? Kama ni hatari kwa sababu ya barabara basi tunatakiwa tujenge barabara nzuri na siyo kuweka classes za huyu anatakiwa kusafiri hivi na yule vile.
 
Mkuu hapa madereva utawalaumu bure tu. Kiuhalisia ni vigogo ndio wanaowaua madereva!

Hawa wanaojiita vigogo hua ni wakali sana wanapotaka kuwahi sehemu. Wengi huwalazimisha madereva "kukanyaga" na ikionekana dereva huwezi kwenda na kasi ya bosi anayotaka usishangae ukaanza kunyimwa safari kwa kuonekana "huwezi kazi".
 
Umeyasema hayo kwakuwa ni yeye. Vip kuhusu mabasi yanayosafiri usiku??? Au kwako yale mabasi hayaendesgwi na binadamu?? Ajali haina kinga. Hata angepanda ndege ile anachukuliwa uwanjani kuelekea anakokwenda angekumbana nayo tu.
 
Wewe unajidai unaijua Serikali na Watumishi wake, hivi kwa akili yako MD wa TANESCO perdiem ya siku mbili ni issue kweli hadi imuweke barabarani siku mbili? 🤣🤣🤣

Jamaa alimaliza kikao Dom akaona aunganishe Musoma.
Sidhani kama umenielewa ,mkuu wa kitengo anapata posho ya Ndege ...unataka kusema anapata chini ya 250k kwa siku?
 
Mtanzania ana kawaida ya kulaumu pasipotakiwa na panapotakiwa akakaa kimya. Ingekuwa amefariki kwa ajali ya ndege bado wangesema haya ni mafisadi yanayoshindwa kusafiri kwa barabara wacha yafe.
 
Pumziko La Amani Wapate hao Marehemu. Huenda ni matokeo ya kutokupumzika.Gari ni mashine tu inayokufuatisha wewe Binaadamu unaitumiaje,haitakwambia sasa umechoka na unaanza kusinzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…