TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Halafu usiku wa manane. Madereva nao ni watu, wana usingizi.
Pia wengine hawana uwezo wa kuendesha safari ndefu sana

Binafsi mfano nina uwezo wa kuendesha safari ndefu masaa 14 mfululizo mchana bila kupumzika lakini maximum.mwisho saa mbili usiku

Ila huwa sili chakula kabisa nikila kikianza kusagika huwa nasikia usingizi wa hapa na pale Nashtuka gari inahama hama kwenye barabara sababu ya usingizi wa kustukiza
Nakuwa natumia tu maji ya kunywa kidogo kidogo ya moto sio baridi nikiendesha

Safari ndefu zaidi ya saa mbili usiku hata kama ya masaa sita hata niwe nimepumzika sitaki kuendesha Kuna kausingizi kakustukiza hapa na pale huhitaji madereva wazoefu hasa wa uendeshaji usiku

Hata marubani wa ndege huhitaji marubani wazoefu wenye night rating kubwa kuendesha ndege usiku
 
Kuna barabara ya Njombe Songea kwa kweli Ile barabara inaangusha magari sana....kwa mara moja trip ya kwenda huko hivi majuzi nikihesabu malori zaidi ya manane yameanguka. Halafu barabara inamiti mirefu inaning'ining'inia kwenye kingo za barabara. Udongo ulioishika miti hiyo ukilowa sana lazima idondoke barabarani. Nashauri ifanyiwe usafi barabara hiyo.
 
Watu dizain ya huyu dereva ndiyo wale huwaambii kitu kuhusu CCM
Wakati mwengine kuna ajali zinatokea kwa sababu tu serikali haijawajibika kujenga barabara pana lakini ukiikosoa hiyo serikali inayomlipa wanakuona kama kisirani.
 
safari kama hiyo lazima iwe imeandaliwa kitu kinaitwa Journey Management Plan na watu wa logistics & safety wa Tanesco
unasema? yani umuamulie mkurugenzi mkuu aka direkta jenero asafiri saa ngapi na wapi apumzike?🤔hiyo ni bongo hii au?
 
Mm usiku hapana kwa kweli. Hata kupata msaada ni ngumu sana.
 
Ajari za barabara zetu ni ufinyu wa barabara hakuna lengine
Pia mwendo wa madereva wa taasisi za Serikali ni wa hatari sana, huwa hawajali sheria wala alama za tahadhari wawapo barabarani.
RIP kwa wote.
 
Tena siku hizi watu wengi wanapozungumza kiswahili wanaweka dhafuli ya kizungu na kukosea maneno mengine kwa makusudi wakidhani ni ujanja. Mzungu akikosea kiswahili ni vizuri lakini mswahili akikosea kiingereza ni mshamba.
Ila hilo neno dhafuli linachekesha sana
 
Kwa hivyo kama wangepanga mipango yote hiyo ndio wasingekufa? Siku yako ya kufa ikifika utatoka ulipokuwa uende ukakifate kifo. Yaani utakufa pale pale ulipoandikiwa.
Hata kama wangefanya kama ulivyosema wao wangefuatwa na dereva mwingine wakagongwa wao bila ya wao kuwa na makosa na wakafa. Haya mambo ya kifo ni siri kubwa na ndio tunapoona uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Hapo ahadi imetimia kama ilivyopangwa. Kwa sisi waislamu tunasema Inna Lillah wainna ilaihi rajiun (sisi ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Yeye tutarejea).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…