Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Lini watanzania waliacha kujituma na kufanya kazi kwa bidii?!!!

Unaongea kana kwamba uko ndotoni vile......
 
Tatizo ni kUtofanya yale tunayoyazungumza (we don't walk the talk).
Kweli tuaomba misaada tupunguze matumizi yanyosababisha kuongezeka kwa hewa ya ukaa, lakini wakati huo huo tunaruhusu watu kufyeka maeneo ovyo ovyo kwa kisingizio cha ufugaji! Afadhali mkulima anayefyeka eneo akapanda migomba na mikahawa maana hivyo vinasaidia kunyonya hewa ya ukaa.
Imefika mahali hata sheria za uhifadhi wa mabonde ya mnyweo hazifuatwi. Mtu anapewa na kufyeka eneo ambalo kwa sheria linatakiwa lihifadhiwe kwa kuacha mita 60 kila upande.
PAMOJA NA KUOMBA MISAADA, TUJIANGALIE NA SISI WENYEWE MATENDO YETU
 
Ebu tuambie utajiri wa magufuli ni upi!? Pesa pembe la ng'ombe ukiwa nazo hazifichi .ukikutana na mtoto mdogo wa mjini gari la kampuni fulani ya mafuta inapopita utasikia hiyo ya ridhiwani...kampuni gani ulishaisikia ya magufuli au mtoto wake ina trend mjini kabla na baada ya kifo chake[emoji2957]
 
Hao wazungu wali tupiga sana wana Gold Reserve nyingi ya Africa, ukipata nafasi wapige
Uwapige wazungu? Kinachofanyika ni wanakupa mikopo kwa riba kubwa na kwa masharti makubwa.
Rejea kauli ya Samia akiwa bagamoyo, mwenyewe alishangaa masharti anayopewa
 
Kuandika tu kiswahili fasaha hujui....utaweza kuwa na Weledi wa kumshauri kiongozi wa nchi ?!!! Khaaa 😲😲🤣
Ongera yako kwa kujua kuandika kiswahili fasaha na kuwa mshauri wa kiongozi wa nchi ambayo toka ijitawale bado inaangaika kutatua tatizo la maji ingawa maziwa yote makuu Afrika tunayo
 
Wena mkuu andiko lako mantiki ndani yake lakini mkuu, Nchi zetu nyingi za kiafrika , bila misaada unafikili itakuaje , nafikili maneno YAKO angeyaongea pia laki lazima mataifa yaliyoendelea yatusaidie , maana wao pia ni chanzo Cha matatizo aya
 
Yaani munaenda kujadili mambo ya mhimu afu anatokea mwingine kazi yake ni kuomba tu.

Hahahahah.. Omba omba..bahati mbaya hakuna cha bure.
 
Kubali hatima yako. Resign to your fate. Bila ya kuombaomba utawatesa watu tena utaua. Hakuna lolote utakalotoboa bila ya misaada zaidi ya nguo na viatu vyako kwa uchovu.
Kweli mchele mmoja mapishi mbalimbali kwa nini yule Mheshimiwa alikuwa na chuki nao sana hawa wazungu hadi TBC kila siku ni kuimba mabeberu kumbe bado utawala wa hangaya unatamani hela zao,!!makubwa haya!!
 
Let avitu vya maana si kutukana tu.

Nchi inaalikwa kwenye kikao afu inaebda kuwa ombaomba kila mara.

Wakati nyuma imeacha rasilimali za kutosha kabisa.

Nashauri siku nyingine wawe wanajikita kwenye agenda muhimu ili nchi iinuke na kuheshimika.
 
Mleta mada naomba ujielekeze kwa usahihi...
Lisemwalo lipo... Hizo nchi zilizoendelea "zinaiba" sana rasilimali za dunia kujiendeleza! Na pia katika mchakato wa kufanya hivyo zinafanya uzalishaji mkubwa wa gesijoto na kufanya uchafuzi mwingi unaosambaa ulimwenguni kote!
Sikia; kwamba nchi tajiri zilizoendelea zitoe fedha kusaidia nchi maskini na zinazoendelea ni suala la makubaliano rasmi yaliyokuwepo toka enzi za Kyoto Protocol na sasa Paris Agreement. Hivyo #SSH kuweka msisitizo huo kwenye hotuba zake ni kuwakumbusha hao wakubwa majukumu yao kwenye makubaliano rasmi yaliyopo.
Itakuwa ni ajabu kama unaona tatizo kwenye kuwadai uwekezaji wa fedha hizo!
Hiyo ndiyo climate politics! #SSH yupo sahihi!
Ni ujinga kuwakamua wananchi maskini wa Tanzania ili kutoka kwao fedha zipatikane za uwekezaji na ujenzi wa miundombinu (hizo akili zilizikwa pamoja na JPM).
Matajiri wa dunia hii wana pesa ambazo walizipora kutoka kwetu. Matajiri wa dunia hii wamesababisha mabadiliko ya tabianchi kwa viwango visivyomithilika! Matajiri wa dunia hii wanauwezo mkubwa wa kustahimili majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi tofauti na maskini wa dunia hii! HIVYO wanapaswa kubanwa wazirudishe kwa namna nzuri na endelevu ya kuzikwamua na kuziendeleza nchi maskini kujihimu na mabadiliko ya tabianchi!
Na huo ndo msimamo wa dunia kwa sasa unaoangazia masuala ya climate finance and adaptation fund kwa kuwataka nchi tajiri kutoa zaidi fedha na technolojia!
Kama unapingana nao basi huyajui vizuri mabadiliko ya tabianchi na madhara yake.

NB: Tafadhali rejea reports mbalimbali za UN, UNFCCC, IPCC, KYOTO PROTOCOL, PARIS AGREEMENT, n.k!
Mama #SSH hakwenda kutembeza mabakuli. Kwa muda mrefu mikutano ya UNFCCC COP imekuwa ni sehemu ya kuzibana nchi tajiri kutimiza makubaliano yaliyopo.
 
I hope hajasema "wanawake tunaweza kukabiliana na tabia nchi"👌
 
Hoja ya "balance" katika maendeleo, masilahi ya binadamu inaweza ikaongelewa na big potatoes tu Ile ya G8, na siyo shithole countries (kama alivyoziita Trump).

Wale emmitters wakubwa wa carbon dioxide yaani China, USA, European Union na China kupitia Greenhouse gas ndiyo wanapaswa kujadili hilo.

Namuona Rais SSH ame address real issue ambayo itatuongezea fedha za kuratibu mazingira kupitia COP 26 ambayo itatenga USD 19 Bilion kwa nchi 197 ambazo zimeridhia mkataba wa Paris juu ya mabadikiko ya tabia nchi.

Mara nyingine hata kimoyomoyo tukubali tu kuwa nchi iko kwenye reli sahihi mikononi mwa Rais SSH hata kama tuna tofauti za kiitikadi, kidini na kikanda
 
Sijui kwanini Trump alijitoa kwenye paris agreement. Ila kwenye hiyo hotuba mama anataka hela, sasa ndio watoto wa mjini tunavo ishi
Trump alijiondoa kwa mambo mengi.
1. Kama mzungu tajiri mwenye misimamo mikali (republican) asili yao ni ubinafsi na ukorofi
2. Alikuwa analinda maslahi ya nchi yake dhidi ya Uchina. Kwamba hawezi kutoa fedha kuwenda kusapoti competitors wake ambao vile vile ni major GHGs emitters japokuwa wapo kwenye index ya developing countries.
3. Hakuwa na imani kuwa maendeleo ya uchumi wa nchi yake yanahusiana moja kwa moja na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.

(Mengine wengine wataongezea)
 
Mama hana dira, na kwa bahati mbaya hata huko kwenye chama hakuna tena watu wanaotanguliza maslahi ya nchi hii mbele. Imebaki wachumia tumbo tu kama akina Majaliwa, Mwigulu, Januari na wengineo.
Hapo umepotosha. Dira ya Rais Samia iko wazi kabisa sema nyie mnaomuabudu yule DIKTETA mnabisha kama sehemu ya ibada.

Dira ya Samia ni kujenga uchumi utakaoleta financial inclusion kwa raia wake kupitia uwekezaji toka nje, biashara na nchi jirani huku tukizingatia utawala wa Sheria na haki.

Tanzania ilikuwa ni kisiwa wakati wa Mwendazake. Mama anafungua Tanzania kiuchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…