Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024

CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Wakijiunga tu na CCM hapo hakuna Mkimbizi wala nini, ni Raia Mzalendo na wanapewa nafasi nyeti huku Watanzania wakibaki kupiga miayo.
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa maoni kwamba kuendelea kuwepo kwa muda mrefu kwa Wakimbizi na Waomba hifadhi Nchini Tanzania ni tishio la kiusalama kwani taarifa zilizopo ni kwamba wapo Wakimbizi na Waomba hifadhi ambao wameajiriwa Serikalini na wengine wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda amesema hayo mbele ya Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu leo January 22,2024 wakati wa Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda Jijini Dar es salaam.

“Changamoto kubwa katika Mikoa yetu ya magharibi kwa sasa ni uwepo wa Wakimbizi na Waomba hifadhi wa muda mrefu, Tanzania imekuwa ikipokea maombi ya Wakimbizi na Waomba hifadhi kutoka Burundi tangu mwaka 1972, Rwanda tangu mwaka 1994 na DRC tangu mwaka 1996, idadi ya Wakimbizi 27000 kutoka Burundi wa mwaka 1972 hawakuwekwa katika kambi za Wakimbizi badala yake Serikali iliamua kuwagawanya katika Vijiji 73 vilivyopo Mkoa wa Kigoma”

“Wakimbizi hawa na Familia zao bado wanaendelea kuishi katika Vijiji hivyo na kwa kutumia mbinu mbalimbali uhakikisha uzao wao unapata Uraia wa Tanzania bila kufuata Sheria, Serikali ya Tanzania na Burundi zimekuwa zikiwashawishi Wakimbizi hao kurejea Nchini mwao bila mafanikio

“Mh. Rais kuanzia January 01,2023 hadi December 31,2023 jumla ya Waomba hifadhi 138,149 walipokelewa Tanzania ambao sehemu kubwa ni kutoka DRC, Rwanda na Burundi, kutokana na mahojiano ya awali imebainika kuwa Waomba hifadhi wengi wamekuja Tanzania kwa sababu za kiuchumi kwani Tanzania imebainika kuwa na fursa nyingi za kiuchumi kuliko Nchi walizotoka, hata hivyo sababu hizo zinazowafanya Wakimbie Nchi zao zinawakosesha sifa sa kupewa hadhi ya ukimbizi”

“Ni maoni yetu kwamba kuendelea kuwepo kwa muda mrefu kwa Waomba hifadhi na Wakimbizi hawa Nchini ni tishio la kiusalama kwani taarifa zilizopo ni kwamba baadhi ya Waomba hifadhi hao au Wakimbizi au Familia zao wameajiriwa Serikalini kwa nafasi mbalimbali na wengine wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi”

Source - MillardAyo
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024

CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."

Rushwa ndio style ya utawala wa tz, watanzania wazariwa wa kweli. Wananyimwa uraia pacha wakimbizi wana Towa hela wanapewa passport na kazi serikalini wanapewa.
 
Wapo wengi Sana kuanzia bashe,mpango na dotto biteko
Kuna wahamiaji na wakimbizi jamani. Wanatofautiana. Na kuna watu wenye asili ya mahali fulani. Lakini Rais asipuuzie. Anaweza kulishughulia.
Hata MADED, DCs, CEOs na RCs ni nafasi za maamuzi. Msikimbilie kwa mawaziri tu. Kuna yule mama Irene Isaka aliwahi kuteuliwa na kutumbuliwa kwa tuhuma kuwa ni raia wa nchi nyingine. Lakn alikuwa ametolewa SSRA ambayo nayo asingeipata bila kuwa raia.
 
Hao Wahamiaji haramu wanajificha kwenye kivuli cha CCM. Hapo ndio tatizo kubwa lilipo. CCM wako tayari kufanya chochote ila sio kugusa maslahi Yao ndio maana Wana wanachama Hadi WA Kichina
Uko sahihi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024

CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."

Ila mimi bado nipo kwenye tafakuri ya speech ya CDF.
 
Yaani,haya ndio maoni ya CDF! Anasema kuna watu wanapata uraia, bila serikali kujua!? Kuna ubaya gani, MTU kutoka Rwanda, Burundi, Congo, kuomba uraia? Au kwa vile ni weusi? Mbona wa Asia, wazungu,wapo kibao tu,? Kama jeshi, na taasisi zake za, intelijensia, hawana, tskwimu, na wala hawajuhi hao watu, basi, huyu jamaa, ni kilaza kweli kweli, yaani na jwtz na wao wanalalamika! Kuhusu, wakimbizi haramu! Ingekuwa jeshi lenye weredi, angesema, wamekamata watu 3000+walioingia kinyemera! Fucking stupid
 
Hii statement kama haijatolewa kisiasa basi ni statement hatari Sana kwa usalama WA nchi! Je ni akina Nani hao?
Hapo sasa ni kina nani ? Na mimi najiuliza hili swali
 
Baada ya kupata taarifa iyo ulimreport kwenye mamlaka husika au na wewe ni sehemu ya kuficha na kulea uozo?
Na tufanye nini sasa kuondokana na hii kadhia? Maana wasije gusa unyeti wa Nchi tukangamia kama kuku hapa. Usalama kwanza Maslahi ya chapa na nmtu binafsi pembeni.
 
Back
Top Bottom