Mlikaa muda gani baada ya kuoana kabla ya kupata mtoto?

Una hoja mkuu,usikilizwe
 
Miezi kadhaa tu, na hapo tulikuwa tumepanga tusipate, hivyo siku za kuruka majoka zilikuwa ni zile salama, ila tulivyoamua tusake mtoto, ni mwezi ule ule tu mungu akajalia mimba ikapatikana
 
Nitafute mkuu, jambo Hilo ni jepesi
 
Wakuu nina miezi miwili bila bila niko kwa ndoa. Niko na mashaka.
We miezi miwili tu tayari ushakuwa na stress!! Mbona wengine wana zaidi ya miaka miwili bado wanatafuta mtoto.

Hata hivyo hukupaswa kuoa kabla hamjatest mitambo na kumpa mimba. usifuate sana taratibu za dini kuwa sex ni baada ya ndoa, hiyo haipo na huo utaratibu una mapungufu makubwa sana.
 
Aisee,pole sana mkuu,nimesoma nimesikitika sana,kwanza nikupongeze kwa uvumilivu na uaminifu ulionao kwa mkeo,ni wachache sana wanaoweza kushinda hili karibu.

Kama ilivyozoeleka ni kwamba ndoa ni watoto,lakini wakati mwingine huja tofauti na matarajio yetu,hapo ndipo wakati wengi hukata tamaa.Nawashangaa sana baadhi ya wanaume wanaokataa watoto,au mimba au kuwadhihaki waliowabebea mimba na kuwazalia watoto,na kufanya waitwe baba. Mungu akusaidie mkuu,upate hitaji la moyo wako,usikate tamaa siku yako ya furaha inakuja.

Endelea kupiga goti wewe pamoja na mkeo,salini kwa pamoja Wala usifikirie kumuacha mkeo kwa sababu hiyo,wakati wa Mungu ndio wakati sahihi.
 
Mkuu mkeo alishawai kufanya kipimo cha mirija??
Ila usiwaze mtapata mtoto
 
Mkuu mkeo alishawai kufanya kipimo cha mirija??
Ila usiwaze mtapata mtoto
Kipimo kinauma hiki...

Nina miaka 4 ya ndoa yangu, sijapata mtoto, stress nilipitia ila uzuri mume na wakwe na wifi zangu wananitia moyo.

Mwanzo nilijipa stress sana, ila zikapoa ila Kuna wakati zinarudi...

Hakika kama kuna kitu nilipima nikaumwa na kulazwa emergency ni hiki kipimo cha mirija yaani balaa lake ni hatare...

Jamani usiombe, hadi damu inatoka, alafu majibu yanakuja yanasema upo sawa.

Mungu unikumbuke na wote ambao wanapitia hili la kuchelewa kupata mtoto.
 
Kiliuma kwa.sababu ilikuwa na uchafu.so kilisafisha safisha.pole
Baada ya hapo umecheki magari? Una miaka mingapi?
 
Kiliuma kwa.sababu ilikuwa na uchafu.so kilisafisha safisha.pole
Baada ya hapo umecheki magari? Una miaka mingapi?
Mbona hawakuniambia kama nilikuwa na uchafu, waliniambia kipimo kinaonyesha huna tatizo...

Ila Huwa hawasemi kile kipimo kinauma, maana baada ya kulazwa emergency, nikasikia wakisema mbona hamuwaambii Hawa wanawake kuwa kipimo kinauma...
 
Je katika zunguka kwa madaktari wife hana tatizo la uzazi?

Kama hana tatizo tumia mitishamba kuna mizizi naifahamu huwa haicheleweshi kabisa endapo tu vizazi vipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…