Mnaotumia Masaa Mengi Kujadili Mpira, Mnapata Dola Ngapi kwa Siku?

Kama jana maeneo tofauti nakutana na watu from nowhere wanajadiliana mpira wa Simba vs Yanga issue ya Derby.

Nikawa nawaza,hivi hawa mbona wamekazana sana?

Hivi hawa wangekuwa ndio kizazi cha miaka ya 1920+ hadi 1959+ hii inchi ingepata huu uhuru wa leo tulio nao?🤔

Imagine wazungu wangeweka mambo ya mpira redioni muda wote na kuruhusu pombe kwa wingi plus mademu kujiuza na udangaji hivi hili taifa lingepatikana.

Hiki kizazi ni cha hovyo kuwahi kutokea katika hii jamii ya muafrika tokea uhuru.
Hebu tembelea nchi za Wazungu, kuna channels nyingi za sports 24/7 zaidi ya nchi yoyote Africa, udangaji ni official na malaya wanaheshimika kama official profession na wanalipa kodi, udangaji Africa(hasa Tanzania) ni mdogo mno.
Kufanya kazi masaa mengi si kufanikiwa kimaisha, think,plan and strategize sensibly na utagundua masaa machache sana ya hustles yanatosha sana kwa mtu kufanikiwa kimaisha. Wasio na uwezo wa kufanya kazi zao wenyewe kuingiza kipato ndiyo hufanyishwa kazi kama punda na kipato portion kubwa ya kipato huenda kwa wanaowafanyia kazi ambao wana muda mwingi wa ku-relax.
 
Wenzako wanaozitafuta dola wakipumzika wanaenda kwenye hoteli za 5 stars Dubai. Hawa wenzetu watabishana wee, wanaondoka vichwa vinauma hata pesa ya kununua panadol hawana.
Kwani hao wanaobishana mpira wanakua hawana shughuli za kufanya zinazo waingizia kipata tukianza na ndugu zako?
 
Wana kazi zinazowawezesha kula mlo mmoja tu kwa siku! Ndio sababu najaribu kuwafumbua macho, watumie muda mwingi zaidi kubuni njia za kujiongezea kipato.
 
Jitu linatoa nauli kutoka s/Wanga hadi dar kuangalia mpira!
Kufika dar ananiomba 20,000 ya kula?
Huyu ana akili au matope?
 
Dah, asante, mkuu. Hiyo kwangu ni BREAKING NEWS
 
Wembe wangu nautumia kukata kamba zilizowafunga wanaojadili mpira bila kuongeza kipato
Kwa hio hapo ulipo hio mimaji uliyojimwagia ndio itakuaje itakukaukia tu au una mpango gani na hio minywele?
 
Mpira wa miguu ni burudani inayowachangamsha wengi, lakini je, umewahi kujiuliza thamani ya muda unaotumia kujadili mpira? Wengine hutumia saa nyingi kubishana kuhusu wachezaji, timu, na matokeo, lakini je, mijadala hiyo inazalisha kipato chochote?

Katika ulimwengu wa sasa, muda ni rasilimali muhimu. Wale wanaonufaika zaidi na mpira ni wachezaji, makocha, watangazaji, na wadhamini—si mashabiki wanaopoteza masaa kwenye mabishano yasiyo na tija.

Biblia inasema: “Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.”(Waefeso 5:16-17 BHN). Badala ya kutumia muda mwingi kuzungumzia mpira bila faida, ni vyema kufikiria jinsi unavyoweza kutumia muda wako kwa njia yenye manufaa zaidi, kama kujifunza ujuzi mpya, kuwekeza, au kuunda fursa za kipato. Hebu jiulize tena:

👉Baada ya kubishana kuhusu mpira, akaunti yako ya benki itaongezewa pesa?
👉Je, mjadala wako wa mpira utalipia bili zako za mwezi huu?
👉Dakika unazotumia kubishana kuhusu mpira zingekuletea faida gani kama ungezitumia kwa kazi inayokuongezea kipato?
👉Wachezaji unaowatetea wanajua hata jina lako?
👉Kama ungetumia muda huo kujifunza ujuzi mpya, ungekuwa mbali kiasi gani sasa?

Si afadhali hata ungetumia muda mwingi kujadili mambo ya rohoni ili ujizoeze kuwa na utauwa? Utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye(1 Timotheo 4:7-8).
Mbona wewe unaingia kanisani na kukaa masaa 5, huwa unapata kiasi gani? Unaingia saa 3 asubuhi unatoka saa 8 mchana, faida yake nini?
 
Bongo nyosso,,,,agenda za mpira zinateka watu kiasi kwamba wanashindwa kuhoji na kujadili ishu za msingi kwa maslah mapana ya nchi
Unataka tuhoji nini.... Umeme tumeambiwa Rufiji ni mbali umeme unapotea njiani... Tutanunua wa Ethiopia ... Nadhani ni karibu zaidi... Ukihoji si unaambiwa uhamie Burundi.
 
Mbona wewe unaingia kanisani na kukaa masaa 5, huwa unapata kiasi gani? Unaingia saa 3 asubuhi unatoka saa 8 mchana, faida yake nini?
Kukaa kanisani masaa mengi ni kujizoeza utauwa.
1 Timotheo 4:8
"...utauwa una faida kwa mambo yote, una ahadi ya uzima wa sasa na ule ujao."

Wanaotumia muda mwingi kujadili mpira, mara nyingi wanaishia kujaa hasira, ghadhabu, kutukanana na kudharauliana. Hayo mambo yanaweza kuwapeleka motoni.

Waefeso 4:31
"Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila uovu."
 
Unataka tuhoji nini.... Umeme tumeambiwa Rufiji ni mbali umeme unapotea njiani... Tutanunua wa Ethiopia ... Nadhani ni karibu zaidi... Ukihoji si unaambiwa uhamie Burundi.
Usiingize siasa hapa. Hapa tunaangazia hasara za kutumia muda mwingi kujadili mpira bila kuingiza kipato.
 
Mpira wa miguu ni burudani inayowachangamsha wengi, lakini je, umewahi kujiuliza thamani ya muda unaotumia kujadili mpira? Wengine hutumia saa nyingi kubishana kuhusu wachezaji, timu, na matokeo, lakini je, mijadala hiyo inazalisha kipato chochote?

Katika ulimwengu wa sasa, muda ni rasilimali muhimu. Wale wanaonufaika zaidi na mpira ni wachezaji, makocha, watangazaji, na wadhamini—si mashabiki wanaopoteza masaa kwenye mabishano yasiyo na tija.

Biblia inasema: “Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.”(Waefeso 5:16-17 BHN). Badala ya kutumia muda mwingi kuzungumzia mpira bila faida, ni vyema kufikiria jinsi unavyoweza kutumia muda wako kwa njia yenye manufaa zaidi, kama kujifunza ujuzi mpya, kuwekeza, au kuunda fursa za kipato. Hebu jiulize tena:

👉Baada ya kubishana kuhusu mpira, akaunti yako ya benki itaongezewa pesa?
👉Je, mjadala wako wa mpira utalipia bili zako za mwezi huu?
👉Dakika unazotumia kubishana kuhusu mpira zingekuletea faida gani kama ungezitumia kwa kazi inayokuongezea kipato?
👉Wachezaji unaowatetea wanajua hata jina lako?
👉Kama ungetumia muda huo kujifunza ujuzi mpya, ungekuwa mbali kiasi gani sasa?

Si afadhali hata ungetumia muda mwingi kujadili mambo ya rohoni ili ujizoeze kuwa na utauwa? Utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye(1 Timotheo 4:7-8).
Wewe kutojadili Mpira inakuingizia Dola ngapi kwa siku?
 
Back
Top Bottom