Morogoro ni Mkoa mzuri namba Moja wa kuishi Tanzania

Comments za humu ni za watu wa Dar. Tuliosomea Moro tunajua shida za Maji na typhoid. Ukihamisha SUA na MZUMBE ujue umeiua Morogoro.
Yawezekana Moro bado huijui vizuri Mzumbe ipo pembezoni kabisa Wilaya ya Mvomero , ina impact ndogo Sana kwa Moro town . Hebu taja mkoa wako hapa nisijekuwa nabishana na mlughalugha wa huko sitimbi
 
Morogoro ndio gateway place nikichoka na mihangaiko ya dar, sometimes naamua tu natoka dar asubuhi nafika asubuhi Moro, nakula na kunywa naweza nikalala au nikarudi usiku kuja dar na nina enjoy sana. It's a blessed city
Makao makuu ya nchi yalitakiwa kuwa morogoro,
 
Huu ndio mkoa wa hovyo kabisa nchini Tanzania maana maji ya kunywa ya mkoa huu yamejaa madini ya ulanga na kusababisha watu wengi wasiozaliwa mkoa huu kuugua magonjwa ya tumbo na wengi hupoteza maisha. Huu mkoa ni wa kingese sana.
 
Vyuo vya maana hapo ni viwili tu, SUA na Mzumbe, hivyo vingine ni zaidi ya vyuo vya Kata wanachuo wanachapwa bakora
 
ila namba 7 sidhani kama ni sahihi, huu mkoa maji yake hata sio ya kuringia na maji ya mito hayatumiki kwa huduma za kawaida kama kunywa na kuoga yako full typod. ukisema mkoa wentr mito nadhani ni kagera na moshi huko hawana shida wale ya maji kwa moro hapa hapana hapana nakataa.mengine yote uliyoelezea uko sawa mia mia ni mkoa mzuri sana na sasa majengo makubwa marrfu yanaanza kujengwa soon linakuwa jiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule pamezidi

Pamezidi sio kidogo inafika time hadi mabomba yanatoa maji machafu

Chakula, hali ya hewa, location na muonekano wa asili ni plus na kama mtu ana ndoto za kufanya kilimo, labda nuvu zimuishie mwenyewe

Ila Morogoro ni mini dar, watu wake na wa dar wametofautiana padogo sana maana hadi uswahili wa dar, moro umeshamiri kiasi kwamba mtu wa dar hawezi struggle kujichanganya

Overall bado sijaona mji ambao upo well balanced kama mwanza. Nimefika pengi Ila hapa ni pazuri zaidi kuishi
 
Morogoro tatizo la maji sio la mitaa flani ni tatizo la mji mzima

Dar kuna mitaa ina shida ya maji Ila Morogoro labda uvune maji ya mvua Ila kama unategemea maji ya hilo bwawa sahau.

Nilishuhudia maji machafu yanatoka bombani nikapanyooshea mikono
 
hapana hapana wa dar wamelegea saaaaaaana, na wanrembua mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukikaa na kijana wa dar na Morogoro, walichotofautiana ni location, ukikaa na mluguru na mzaramo walichotofautiana ni ukulima na uchakarikaji wa waluguru Ila vingine vyote ni sawa. Yaani nikimtoa mzaramo sijaona kabila lingine wanapenda ngoma kuliko waluguru, msimu wa mavuno hata birthday ya mtoto wataitisha ngoma ikeshe 😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…